Ishara za serikali hii kutokuwa na mipango endelevu

1954tanu

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
1,038
487
Serikali hii inaonesha dalili kwamba haina sera na mipango endelevu kwa ustawi wa watu wake, dalili mojawapo ni hii hapa:

- Ni pamoja na wananchi wake kutokusikia na kuona mjadala wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa baina ya wawakilishi wa wananchi (wabunge) na serikali.

Wananchi hawaujui mpango wenyewe ukoje,unasema nini,utatekelezwaje.

- Mijadala ya bungeni ilisaidia kukuza na kuinua kiwango cha uelewa wa somo la uraia, utawala bora na demokrasia miongoni mwa wananchi wa jinsia na marika yote.
Pasipo elimu ya uraia Mipango ya Maendeleo huonekana ni ya serikali zaidi na si ya wananchi.

Imedaiwa kuwa serikali haina fedha za kugharamia matangazo ya vikao vya bunge kupitia TBC. sawa. Lakini wapo watu binafsi na taasisi binafsi wanaweza kurusha matangazo hayo. Hao pia serikali imewakataza. Serikali inaficha nini?

- Kwa weledi wachache na hao wanaokumbuka maneno ya Mwl.Nyerere kwamba kinachoitwa "Siri ya serikali" si kingine ila UZEMBE wa serikali hiyo. Je! Kwa mantiki hiyo, serikali hii ina UZEMBE kiasi gani hata izuie masuala yake yasioneshwe hadharani?

ANGALIZO:
Hata yaliyodarini yatashushwa na kuwekwa peupe pee!
 
hii serikali inaweza kuwa ya kijamaa mambo leo, haieleweki kwa kweli! hamna sera rasmi.
 
Humu kuna watu kazi yao kutwa kucha ni kusifia tu na ukiwauliza toka jpm aingie madarakani kuna mabadiriko yoyote kwenye mahitaji ya mtanzania
kama vile.mchele.sukari.maharagwe.mahindi na nk?
Utajibiwa hapa kazi tu"
 
Mimi mpaka sasa hivi bado sijaelewa serikali hii inasimamia Sera gani kwa maslahi mapana ya wananchi?zaidi ya hapa kazi na majibu!bado kuna mambo mengi ktkt serikali hii hayako sawa..!inaitaji jicho LA tatu kuliona hili.
 
Back
Top Bottom