JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 706
- 1,230
Kukosa hamu ya chakula, kichefuchefu na kutapika.
Kuwa mdhaifu, mwili kuchoka na kupungua uzito.
Kuvimba miguu,mikono au/na usoni karibu na macho.
Shinikizo la damu lisilozuilika hasa kwa umri mdogo.
Kukosa nguvu kunakosababishwa na upungufu wa damu mwilini (anaemia), hali inayosababishwa na figo kutotengeneza homoni ya erithropoyetini inayosaidia kutengeneza chembechembe za damu.
Kushindwa kulala,kizunguzungu na kushindwa kuwa makini.
Kukosa nguvu, kukosa hamu ya chakula, kichefuchefu na kuvimba ni dalili za mapema za ugonjwa wa figo.
Kujikuna, mkakamao wa misuli ( muscle cramps), kuhisi uchovu kwenye miguu na kushindwa kufikiria kitu kwa makini.
Maumivu mgongoni hasa chini ya mbavu.
Kuhisi kutaka kukojoa mara kwa mara hasa wakati wa usiku (nocturia).
Maumivu, Urahisi wa kuvunjikavunjika mifupa kwa watu wazima na watoto kutokukua kwa sababu ya upungufu wa vitamini D inayotengenezwa na figo.
Kukosa hamu ya kufanya mapenzi kwa wanaume na kukosa hedhi kwa mwanamke.
Ugonjwa wa figo huhusishwa na ongezeko la vifo vinavyotokana na ugonjwa wa moyo.