Isaidie Same ishinde uchaguzi wa 2015

Fue Fue

Senior Member
Jan 6, 2013
107
128
Mkoa wa Kilimanjaro ni mkoa amboa unaoonekana ngome ya Chadema. Mkoa huu umekuwa mstari wa mbele kujiletea maendeleo kwa wananchi wake kushiriki kushiriki shughuli mbalimbali za maendeleo. Kama biashara, kilimo, viwanda, ufugaji, huduma mbali mbali za jamii, usafiri, nk.

Wilaya ya same ndio pekee imeathirika sana kiuchumi na kielimu kwa sasa. Wilaya hii iliwahi kufanya vizuri sana kwenye elimu kipindi cha nyuma ila sasa inatisha sana.

Ili tuweze kupiga walau hatua moja inatupasa kupata viongozi ambao wako makini na fedha za kodi za wananchi kuanzia makusanyo ya halmashauri na mgao wa serikali kuu kutoka dodoma. kutumia vizuri vyanzo vya mapato vya wilaya na kuvutia wawekezaji kutoka sehemu mbalimbali nchini.

Wilaya hii inaathiriwa kwa kiasi kikubwa na giografia yake ya milima na mabonde mengi sana. Milima hii ni vivutio vikubwa sana kwa watalii wa ndani na nje kama itatumiwa vyema.

Milima hii husababisha miundo mbinu ya barabara kuwa migumu sana. Ila wakipatikana madiwani wenye uelewa na wabunge ambao wanajali maendeleo ya watu wao tutapiga hatua kubwa sana.

Isaidie Chadema kushinda 2015 kwenye wilaya ya same. peleka ujumbe wa ushindi na uunana nami kuhakikisha Same inakwenda Chadema 2015.

Nguvu ya umma ni nguvu ya Mungu
 
Naam kesho kutwa napita kwenda Usangi tutawasiliana
 
Hivi mbunge wake ni lini anakuwa Same na ni lini anakuwa Dodoma kwa John former Jumanne?
 
Back
Top Bottom