Is Tanzania a "Mineral Republic"?

Is Tanzania a "Mineral Republic"?

Utaliita ndiyo sekta inayongoza kuchangia pato la taifa kwa around 17% ikifuatiwa na mawasiliano, kilimo na viwanda, madini yanachangia kiasi kidogo sana.

Kwa sababu 75% ya Watanzania wako vijijini na wanategemea kilimo, nilitegemea serikali ingewekeza zaidi kwenye sekta ya kilimo ambacho wengi wanakimudu, sekta ya madini wachache sana wanaomudu kufanya biashara hiyo.
Wao wako bize na makinikia tu

Ova
 
It could be “mhemko na mihasira republic”, mhemko kwa sababu mashauri na mipango inafanywa bila mipango na mwelekeo na mihasira kila wakati watu wamenuna kila kiongozi ana foka foka kwenye majukwaa.

If you don’t like the system change it, if you don’t like the results, you are probably a clueless, need to look at the mirror, the inadequacy is on you rather than the hay sayer, I’m just saying.

Tusianze kurushiana madongo!
 
Waziri aliyekua analeta habari ya mafuta na gesi ametemwa naona ndo mana usikii kingine chenye nguvu subiri tuone aliyepewa sekta ya utalii na maliasili nae ataweza kutupa uimara wa sekta ikaonekana inaweza kutupa pato kubwa kama madini au ndo tutasikia kamata kamata majangili nani jangili yule fukuza weka huyu simamisha yule miaka inaenda basi ndo ivo
 
Kulikuwa na nchi moja huko Amerika ya Kati ambayo ilikuwa inajulikana kama 'Banana Republic', ilijulikana hivyo kwa sababu asilimia kubwa ya mapato yake na uchumi wake ulitegemea zao moja tu la ndizi.

Nina wasiwasi na nchi yetu ya Tanzania inaelekea kujulikana kama 'Mineral Republic'.

Nasema hivyo kwa sababu sioni mipango mikakati yeyote 'tangible' ambayo serikali yetu imedhamiria kuifanya au inaifanya kuimarisha sekta zingine zaidi ya sekta ya madini. Nchi imegubikwa na suala moja tu la madini madini utadhani Watanzania hawawezi kuishi bila madini.

Kipindi cha Mwalimu Nyerere kulikuwa na mikakati ya kitaifa ambayo ilitekelezwa kwenye sekta mbalimbali. Tulizoea kusikia serikali ikihamasisha, Elimu Ni Msingi, Kilimo ni Uti wa Mgongo, Misitu ni Mali, 'Kilimo cha kufa na kupona', Maji ni Uhai, nk.

Kwa mfano, mkakati wa serikali ya Nyerere wa 'kilimo cha kufa na kupona' mwitikio na hamasa ilikuwa mkubwa, huko vijijini ilikuwa ni lazima mtu angalau awe na ekari moja ya shamba, na ilikuwa marufuku kuonekana ukizurula nyakati za asubuhi. Upandaji miti vile vile kila mjumbe wa Shina alitakiwa awe na mti wake wa mfano. Leo sioni mikakati yeyote ya maendeleo kuhamasisha wananchi zaidi ya kuhamasishwa kufanya usafi mara moja kwa mwezi.

Hata awamu zilizopita tuliona, mikakati mbalimbali ya maendeleo kitaifa kwenye sekta mbalimbali kama mipango ya , MKURABITA, MKUKUTA, SHULE KILA KATA, KILIMO KWANZA nk ambayo ilikuwa ni mipango ya serikali kuhamasisha wananchi kujihusisha na uzalishaji na maendeleo ya jamii katika maeneo tofauti.

Kipindi cha awamu hii sijasikia wala kuona waraka wowote wa serikali ukisambazwa kuhamasisha azimio au mkakati wowote wa kitaifa, labda nisiwe mchoyo wa fadhila kwenye mpango wa madawati ingawa sijui project hiyo imefanikiwa kwa asilimia ngapi.

Sioni mikakati ya Kilimo, sioni mikakati ya Maji na Uvuvi, Elimu, Misitu, sijaona press conference ya rais kuzungumzia mikakati ya umwagiliaji kila siku madini na miundombinu tuuu.

Naona ni kama serikali imepigwa na ganzi iko 'stagnant' isijue ni vitu gani vya msingi vinavyogusa maisha ya familia moja kwa moja badala ya kusubiri faida ya Madini ambayo wananchi wa kawaida wanaweza wasiipate wala kuiona kwa kipindi cha uhai wao.
Mzandiki mbobezi katika ubora wako.
 
Miezi sita sasa nchi imejikita katika makinikia na kuishia kupeana vyeti mbele ya TV huku tukiambulia Bil 700 za ahadi ya mashaka mapato ambayo yako chini ya makusanyo ya TRA ya mwezi. Bado tunaambiwa tunadai kodi ya Trilioni 425. Yaani ni drama kwenda mbele. Serikali yote imehamishia macho, masikio na mawazo yote huko kwenye madini na huku nyuma lazima utasikia watu wamepiga mahela kwa kuleta mbegu mbovu, mbolea isiyo viwango nk maana hakuna mwenye udhati kwenye mengine zaidi ya makinikia kunakotolewa vyeti kama sherehe ya kitaifa.
Tunaimbishwa wimbo "vita ya kiuchumi" nasi tunaitikia tuu kama tulivyokuwa tunaitikia wimbo wa "ccm mbele kwa mbele" bila hata kujiuliza hiyo vita mikakati yake ikoje? Mbona kamanda mkuu akihojiwa mkakati wa vita au akikosolewa anakuwa mkali? Hiyo vita anapigana kamanda au yeye anaongoza hivyo lazima mikakati iwe wazi kwa wapiganaji?
Mkuu Quinine hii ni Publicity Republic
 
Kulikuwa na nchi moja huko Amerika ya Kati ambayo ilikuwa inajulikana kama 'Banana Republic', ..
Nasema hivyo kwa sababu sioni mipango mikakati yeyote 'tangible' ambayo serikali yetu imedhamiria kuifanya au inaifanya kuimarisha sekta zingine zaidi ya sekta ya madini. Nchi imegubikwa na suala moja tu la madini madini utadhani Watanzania hawawezi kuishi bila madini.
......
Sioni mikakati ya Kilimo, sioni mikakati ya Maji na Uvuvi, Elimu, Misitu, sijaona press conference ya rais kuzungumzia mikakati ya umwagiliaji kila siku madini na miundombinu tuuu.

Naona ni kama serikali imepigwa na ganzi iko 'stagnant' isijue ni vitu gani vya msingi vinavyogusa maisha ya familia moja kwa moja badala ya kusubiri faida ya Madini ambayo wananchi wa kawaida wanaweza wasiipate wala kuiona kwa kipindi cha uhai wao.
Barrick wakitoa 300milioni dola walizoahidi, Mkulu atanunulia yale "meno" ili watu wapate vitendea kazi.

Hapana kazi tu! Watu watalimia meno!

Waambie wakulima waanze kujitetemesha, meno yanaletwa kwa hisani ya "mzungumzo makanikia".

Lakini nilimsikia Mkulu akisema pesa hizi anazihitaji haraka kwa matumizi ya treni na .......
 
Jana nlichangia uzi mmoja humu nliuliza madini yanachangia asilimia ngapi kwenye pato la Taifa?sikupata jibu....
Nkasema tanzania isitegemee hata Siku moja wananchi wake wata toboa kwenye sekta ya madini,lakini serikali ingeweka nguvu zaidi kwenye kuinua kilimo,kilimo ndiyo Mlango mzima madini hayo dhahabu,almasi,tanzanite n'a madini mengine ya vito ni anasa tu Ktk matumizi(mimi naitaka hivyo)
Nashangaa awamu hii kilimo wao wamezidi kukitupa Mkono hawafikiri kbao gani ya kumuinuaa mkulimaa
Sekta ya utali tu pato lake Siku zote linazidi madini Ktk mchango wake
Kuna nchi moja afrika Jina nmesahau wao pato lao kuu wanategemea utaliii,sisi ni makinikia tu inawasumbuaaa Mpaka sasa je Hzo zingone wataweza
Asante kwa kuleta uzi huu kamanda

Ova
In kweli kilimo ndio itakayoleta mapinduzi katika maendeleo ya watu. Ni ukweli usiopingika pia kwamba mapato yapatikanayo ktk kilimo sasa hayatoshi kabisa kuimarisha kilimo chenyewe.
Ili kilimo kiimarike lazima serikali iwekeze huko
He serikali itawekeza itapata wapi hela!?
Ukijiuliza hayo utajua kwa nini in muhimu kupata hela kutoka madini, utalii mitandao nakadhalika ili kuja kuinuia kilimo
Kumbuka kwenye madini au utalii haruwekezi kwa gharama kubwa lakini kuna mapato makubwa tofauti na kilimo
 
Nina wasiwasi na nchi yetu ya Tanzania inaelekea kujulikana kama 'Mineral Republic'.
Wasiwasi wako wa nini?ni dhambi?
Kama madini tulio nayo tukiyatumia kwa faida ya nchi ili yatuvushe kuna ubaya gani?
Umekasirika nchi kusimamia rasilimali zake?
 
Kama huelewi hoja bora upite tu nani kakasirika rasilimali kusimamiwa, tatizo lenu mmejenga hisia mtu fulani akisema lazima atakuwa anaipinga serikali, Zitto akishauri kitu huyu lazima atakuwa amehongwa, Lissu akisema kitu hata kama ni cha maana huyu sio mzalendo, upuuzi kabisa.
 
Punguza povu dada.Umesema wasiwasi wako nchi isiwe mineral republic!Je ni dhambi tukiwa mineral republic?
 
Elewa madini siyo biashara ya kudumu madini hayazai kuna siku yatakwisha.

Hoja yangu ni kukumbusha kuwa kuna sekta zingine ni za kudumu ni muhimu zinahitaji kufanyiwa mikakati kama anavyofanya kwenye madini, tatizo liko wapi.

Sekta ya kilimo kwa mfano ndiyo sekta inayoweza kumuinua mwananchi kwa muda mfupi, utalii ni sekta unaoongoza kuchangia pato la taifa wala siyo madini, lakini kila siku press conference za makinikia tu, ndio hoja yangu, wewe ukisema eti nimekasirika maliasili kulindwa unamaana gani.
 
Kulikuwa na nchi moja huko Amerika ya Kati ambayo ilikuwa inajulikana kama 'Banana Republic', ilijulikana hivyo kwa sababu asilimia kubwa ya mapato yake na uchumi wake ulitegemea zao moja tu la ndizi.

Nina wasiwasi na nchi yetu ya Tanzania inaelekea kujulikana kama 'Mineral Republic'.

Nasema hivyo kwa sababu sioni mipango mikakati yeyote 'tangible' ambayo serikali yetu imedhamiria kuifanya au inaifanya kuimarisha sekta zingine zaidi ya sekta ya madini. Nchi imegubikwa na suala moja tu la madini madini utadhani Watanzania hawawezi kuishi bila madini.

Kipindi cha Mwalimu Nyerere kulikuwa na mikakati ya kitaifa ambayo ilitekelezwa kwenye sekta mbalimbali. Tulizoea kusikia serikali ikihamasisha, Elimu Ni Msingi, Kilimo ni Uti wa Mgongo, Misitu ni Mali, 'Kilimo cha kufa na kupona', Maji ni Uhai, nk.

Kwa mfano, mkakati wa serikali ya Nyerere wa 'kilimo cha kufa na kupona' mwitikio na hamasa ilikuwa mkubwa, huko vijijini ilikuwa ni lazima mtu angalau awe na ekari moja ya shamba, na ilikuwa marufuku kuonekana ukizurula nyakati za asubuhi. Upandaji miti vile vile kila mjumbe wa Shina alitakiwa awe na mti wake wa mfano. Leo sioni mikakati yeyote ya maendeleo kuhamasisha wananchi zaidi ya kuhamasishwa kufanya usafi mara moja kwa mwezi.

Hata awamu zilizopita tuliona, mikakati mbalimbali ya maendeleo kitaifa kwenye sekta mbalimbali kama mipango ya , MKURABITA, MKUKUTA, SHULE KILA KATA, KILIMO KWANZA nk ambayo ilikuwa ni mipango ya serikali kuhamasisha wananchi kujihusisha na uzalishaji na maendeleo ya jamii katika maeneo tofauti.

Kipindi cha awamu hii sijasikia wala kuona waraka wowote wa serikali ukisambazwa kuhamasisha azimio au mkakati wowote wa kitaifa, labda nisiwe mchoyo wa fadhila kwenye mpango wa madawati ingawa sijui project hiyo imefanikiwa kwa asilimia ngapi.

Sioni mikakati ya Kilimo, sioni mikakati ya Maji na Uvuvi, Elimu, Misitu, sijaona press conference ya rais kuzungumzia mikakati ya umwagiliaji kila siku madini na miundombinu tuuu.

Naona ni kama serikali imepigwa na ganzi iko 'stagnant' isijue ni vitu gani vya msingi vinavyogusa maisha ya familia moja kwa moja badala ya kusubiri faida ya Madini ambayo wananchi wa kawaida wanaweza wasiipate wala kuiona kwa kipindi cha uhai wao.
ahaaaa, ndo umekaa ukafakari na kuishia hapo,ungemtafuta bavicha mwenzio mjadiliane hilo
 
Sekta ya kilimo kwa mfano ndiyo sekta inayoweza kumuinua mwananchi kwa muda mfupi,
Tulishafanya kilimo kwanza kwa miaka 10,tumeona wapi turekebishe na ndio maana kila siku manakuja na vitisho vya njaa kisa serikali haiweki chakula cha akiba,akiba ya chakula inaanza nyumbani kwako kwanza acha kupikia pombe nafaka
utalii ni sekta unaoongoza kuchangia pato la taifa
kwenye utalii tumeshafanya marekebisho mengi ya msingi ikiwemo kuleta ndege mpya sita ili kuongeza idadi ya watalii watakuwa wanakuja moja kwa moja lakini ndege mnazibeza na kusaidia watu watu zizuiwe.
lakini kila siku press conference za makinikia tu
Madini ndio sekta ilioikua imeoza kuliko zote na ndio nyie mlikua mnapiga kelele kila siku ajabu kwa sasa unaskia kichefu chefu yakiongelewa mambo mazuri kuhusu madini
 
Tulishafanya kilimo kwanza kwa miaka 10,tumeona wapi turekebishe na ndio maana kila siku manakuja na vitisho vya njaa kisa serikali haiweki chakula cha akiba,akiba ya chakula inaanza nyumbani kwako kwanza acha kupikia pombe nafaka

kwenye utalii tumeshafanya marekebisho mengi ya msingi ikiwemo kuleta ndege mpya sita ili kuongeza idadi ya watalii watakuwa wanakuja moja kwa moja lakini ndege mnazibeza na kusaidia watu watu zizuiwe.

Madini ndio sekta ilioikua imeoza kuliko zote na ndio nyie mlikua mnapiga kelele kila siku ajabu kwa sasa unaskia kichefu chefu yakiongelewa mambo mazuri kuhusu madini
Kama Kilimo kwanza kiliwashinda na serikali inajua ilikosea wapi mbadala wake ni nini, mnaleta matrekta eti ya bei nafuu kwa mkulima halafu mnauza mil. 60 nani atanunua, leo yamejazana pale Mwenge Suma JKT yamekosa mnunuzi.

Hatuoni mikakati yeyote au press conference kama za makinikia kuongelea kushuka kwa biashara ya zao la mbaazi ambalo bei imeshuka toka sh 2,500 hadi 200 kwa kilo.

Kwenye utalii wakati washindani wenu Kenya wakiondoa VAT kwa watalii sisi tunaongeza ushuru na VAT juu.
 
unataka trekta liuzwe kwa milioni mbili?
Kujaa kwa matrekta kusikubabaishe,mengine yamelipiwa nusu na mengine yanasubiri kuchukuliwa na kwa kua yanafanana ndio maana unaona yamedoda kumbe kila yakichukuliwa yanaletwa mengine
Hatuoni mikakati yeyote au press conference kama za makinikia kuongelea kushuka kwa biashara ya zao la mbaazi ambalo bei imeshuka toka sh 2,500 hadi 200 kwa kilo.
Kuhusu Mbaazi Mwijage alienda India na ameshalizungumzia hilo
Kwenye utalii wakati washindani wenu Kenya wakiondoa VAT kwa watalii sisi tunaongeza ushuru na VAT juu.
Sio kila kitu lazima tufanane na wakenya,na kwa taarifa yako pamoja na uwepo wa vta,watalii wameongezeka sana 2016/2017
 
Kulikuwa na nchi moja huko Amerika ya Kati ambayo ilikuwa inajulikana kama 'Banana Republic', ilijulikana hivyo kwa sababu asilimia kubwa ya mapato yake na uchumi wake ulitegemea zao moja tu la ndizi.

Nina wasiwasi na nchi yetu ya Tanzania inaelekea kujulikana kama 'Mineral Republic'. A country whose economies largely dependent on single commodity.

Nasema hivyo kwa sababu sioni mipango mikakati yeyote 'tangible' ambayo serikali yetu imedhamiria kuifanya au inaifanya kuimarisha sekta zingine zaidi ya sekta ya madini. Nchi imegubikwa na suala moja tu la madini madini utadhani Watanzania hawawezi kuishi bila madini.

Kipindi cha Mwalimu Nyerere kulikuwa na mikakati ya kitaifa ambayo ilitekelezwa kwenye sekta mbalimbali. Tulizoea kusikia serikali ikihamasisha, Elimu Ni Msingi, Kilimo ni Uti wa Mgongo, Misitu ni Mali, 'Kilimo cha kufa na kupona', Maji ni Uhai, nk.

Kwa mfano, mkakati wa serikali ya Nyerere wa 'kilimo cha kufa na kupona' mwitikio na hamasa ilikuwa mkubwa, huko vijijini ilikuwa ni lazima mtu angalau awe na ekari moja ya shamba, na ilikuwa marufuku kuonekana ukizurula nyakati za asubuhi. Upandaji miti vile vile kila mjumbe wa Shina alitakiwa awe na mti wake wa mfano. Leo sioni mikakati yeyote ya maendeleo kuhamasisha wananchi zaidi ya kuhamasishwa kufanya usafi mara moja kwa mwezi.

Hata awamu zilizopita tuliona, mikakati mbalimbali ya maendeleo kitaifa kwenye sekta mbalimbali kama mipango ya , MKURABITA, MKUKUTA, SHULE KILA KATA, KILIMO KWANZA nk ambayo ilikuwa ni mipango ya serikali kuhamasisha wananchi kujihusisha na uzalishaji na maendeleo ya jamii katika maeneo tofauti.

Kipindi cha awamu hii sijasikia wala kuona waraka wowote wa serikali ukisambazwa kuhamasisha azimio au mkakati wowote wa kitaifa, labda nisiwe mchoyo wa fadhila kwenye mpango wa madawati ingawa sijui project hiyo imefanikiwa kwa asilimia ngapi.

Sioni mikakati ya Kilimo, sioni mikakati ya Maji na Uvuvi, Elimu, Misitu, sijaona press conference ya rais kuzungumzia mikakati ya umwagiliaji kila siku madini na miundombinu tuuu.

Naona ni kama serikali imepigwa na ganzi iko 'stagnant' isijue ni vitu gani vya msingi vinavyogusa maisha ya familia moja kwa moja badala ya kusubiri faida ya Madini ambayo wananchi wa kawaida wanaweza wasiipate wala kuiona kwa kipindi cha uhai wao.
Kwenye madini kulikwa kumekufa, kwa hiyo jitihada zilizopo sasa ni za kupafufua ili pakishafufuka basi patembee kwa pamoja na sekta zingine kv kilimo, na matarjio ni kwamba sekta hii itakuja kuongeza push kwa sekta zingne ambazo zenyewe zimekuwa LIVE tangu huko nyuma. Kama zote kwa ujumla bila sekta ya madini tuseme zilikuwa zinaenda kwa mwendokasi wa wastani wa 50 km kwa saa, tunatarajia kuwa mwendokasi utanongezeka kufikia tuseme wastani wa 75 km kwa saa ikiwemo sekta ya madini yenyewe. Jamani tuwaombeeni hawa watu Mungu aendelee kuwa pamoja nao, wa-Tanzania wapate neema.

Siku alikuja Obama hapa mwaka 2013 alilakiwa na wa-Tanzania wengi sana toka U/Ndege hadi mjini, si kwamba walikuwa wanataka kumuona Obama, ila ni kwamba wengi wao hawakuwa na kazi ya kufanya, yaani haswakuwa na ajira, wakaona bora kwenda kujumuika kwenye msafara wa kumuona Obama kuliko kukaa sehemu bila kazi!
 
Back
Top Bottom