The guy is a pure jerk and a joker of laughable proportions! Nafikiri issue sio raisi peke yake tatizo ni sisi ambao tuko tayari kuburuzwa huku tukichekelea na kulalamika chini chini. Hii tabia ya ukondoo naona ni hulka yetu na imeanza siku nyingi sana. Nakumbuka wakati wa maisha magumu miaka ya tisini (ya kupanga foleni kwa mgao wa unga na uhaba mkubwa wa bidhaa na pesa) mtu unamwuliza habari gani anajibu nzuri sana tena bila hata kusita huku yeye na familia yake hawajala siku mbili. Nadhani hii dhana ya amani imekosa mshiko na imepotoshwa maana yake kwa maslahi ya walaji, walafi, mafisadi na watawala Amani haihusiani tu na hali ya kutokuwapo na vurugu; amani inahusiana na kiwango gani mtu yuko kwenye hali ya equilibrioum...hali ya kutulia kimwili, kiakili, kisaikolojia, kiafya, kilishe, kukubalika na familia na jamii etc. Ukipata vitu vyote hivyo ndio unaweza kusema naishi kwa amani. Inapotokea nyumbani hakuna chakula watoto wamelala na njaa, hawana access ya elimu bora, hatuna access kupata haki, viongozi tuliowachagua hawawajibiki etc, huwezi kusema nchi hii au watu wanaishi kwa amani kwani wanaishi katika state ya anxiety.
Process yoyote inayotumika katika kurudisha amani ya kweli (kama nilivyoainisha hapo juu yaani kurudisha hadhi ya mtu kimwili, kiakili, kisaikolojia, kihaki n.k) hata kama itahusisha maandamano, mijadala ya kukosa imani na raisi na serikali yake na hata watu kuchukua destiny ya nchi yao kimabavu kutoka kwa manyang'au yaliyoipora, hiyo inakubalika kabisa. Sometimes the end justifies the means. Ipo mifano mingi tu amabapo wananchi wa nchi mbali wamechukua hatua dhabiti za kupambana na ubeberu wa watawala wao (recent cases za arab uprising, etc) na kuchukua wenyewe destiny ya nchi yao.
Imefikia wakati watu waache kuogopa kuzungumzia amani kwa upana huu na kuangalia hizi options za kuleta amani ya kweli and not just scratching the surface!