IRINGA UNIVERSITY WASALITI.

Hahaha Maisha Ya Siku Hizi Yanatawaliwa Na watu Kujianika Mitandao Kila Kinachotokea Wanataka Kupost fb Na Instagram Ss Hv M2 Na Akili timamu Unaweza Vp kupost Video Kama Ile
Huo utimamu wa akili unao uzungumzia wewe unapimwa kwa misingi ipi hasa!?
Yaani Unaona mtu aliyejitolea kufichua uovu siyo timamu kiakili kweli!!?
You can't be serious. Na Kama walichofanya kilikuwa sahihi Mbona walikimbia na kuondoka shuleni hapo!?
Waalimu katiri kiasi hicho unategemea akabidhiwe wanafunzi na kuishi nao Kama mlezi wao!? Binafsi nampongeza aliye chukua hatua ya kuanika uovu wao Maana yawezekana amewanusuru wengine wengi kwa sasa na hata baadae. Kama makosa ya darasani adhabu inatolewa hivyo Je akitaka mahusiano ya kingono na mwanafunzi akaonyesha kutokukubaliana itakuwaje Si ananyonga kabisa.
 
Hii ni serikali ya MATUKIO, na bado inaendelea kuonesha udhaifu wa maprofesa tulionao. Kafukuza wale madogo chuo kwa TARATIBU ZIPI? Siafiki kipigo lakini suala hili lichunguzwe upande wa pili na haki itolewe kwa wote, kwanza dogo mwenyewe inasemekana ni bange kashashindikana hadi kwao. Halafu yule mwalimu aliyepata tuhuma za KULAWITI wanafunzi iliachiwa mahakama ikafanya kazi yake na hatukusikia tamko la Mwigulu wala Ndalichako?
 
Somo la professional ethics and conduct hajalielewa vizuri huyo denti wa Iringa uni. Hata kama alitaka kuwa whistle blower, its better ile video angeipeleka sehemu husika na si kuisambaza ovyo. Watanzania wengi kwa ujumla wanahitaji semina elekezi katika matumizi ya teknolojia hizi mpya.
Wasalaam
Mkuu wewe alshabab au boko haram?
 
Wanakijiji waliouwa Watafiti ingetokea Mzalendo mmoja akachukua Clip nadhani Mawaziri na Manaibu wote na Makatibu Wakuu kila mmoja angetolea Tamko
 
Tukisema vyuo vikuu vinavyojitambua vip DAR NA MORO TU mnapinga, IPO SIKU MTAKUBALI!!,.
 
Hivi nyinyi vijana mnaojiita walimu mnawatoto kweli huko majumbani kwenu?
Tukio kama lile ilibidi apongezwe huyo aliyerekodi kwa kufichua huo ukatili nyinyi mnamuona msaliti!!! Msaliti ni wewe ambaye unamtetea muovu bila sababu ya msingi.
 
Hiv ww unavyoona ameisaidia jamii katka kuyatambua haya makosa au usaliti.
Usisitutukane wanafunz wa pale nyambafu.
Japokua first year
Ameisaidia katika lipi kwa kuumiza wengine? Unafikiri pale shuleni muda huu panakalika akili ndogo tu. Angekuwa na mapenzi mema si angempelekea hiyo video mkuu wa shule… hata huyo mwanafunzi anamtatizo yake
 
Hivi nyinyi vijana mnaojiita walimu mnawatoto kweli huko majumbani kwenu?
Tukio kama lile ilibidi apongezwe huyo aliyerekodi kwa kufichua huo ukatili nyinyi mnamuona msaliti!!! Msaliti ni wewe ambaye unamtetea muovu bila sababu ya msingi.
Sana kabisa mimi nimeona Ile clip niliis napigwa mimi
 
Huyo aliyechukua video mpeni muda tuu halafu mfatilie maendeleo yake, mtajua mshahara wa alichokifanya.
 
Mh kwa ambao tumesoma miaka ile… sikuona ajabu sana japo inaumiza lakini yapasa hasa kujua tabia ya mwanafunzi, kosa lake siku hiyo na historia yake kinidhamu. Nakumbuka mwl. Wangu alimpiga mwanafunzi mwenzetu na upanga kichwani kwa upaba baada ya dk. Kumi jamaa alivimba hatari.
 
Mh kwa ambao tumesoma miaka ile… sikuona ajabu sana japo inaumiza lakini yapasa hasa kujua tabia ya mwanafunzi, kosa lake siku hiyo na historia yake kinidhamu. Nakumbuka mwl. Wangu alimpiga mwanafunzi mwenzetu na upanga kichwani kwa upaba baada ya dk. Kumi jamaa alivimba hatari.
Unakoment nini mbona atukuelewi unaopose au una argue?
 
Polisi alidakwa anapokea rushwa yaliyomkuta twayajua na wengi walishangilia. Leo walimu wanafunzi wamedakwa naona kuna utetezi wa kutosha. Aliyerekodi ametuwezesha kuona tukio hili. Hii iwe fundisho kwa wengine. Waliohusika lazima wawe accountable kwa vitendo vyao.
Pia ichunguzwe kama kijana anakosa lazima na yeye awajibishwe. Kila mtu ahukumiwe kwa kosa lake.
Kuwafukuza vyuo wale vijana sio maamuzi ya serikali labda watumie mabavu. Waziri angeweza kushauri vyuo ku tathmini kama vijana hao wanastahili kuendelea kuwa wanafunzi. Vyuo kupitia mamlaka yao vichukue hatua stahiki. Waziri asiamulie vyuo.
Kama walifanya ni makosa ya jinai mahakama inawahusu.
 
Maticha wamemind wenzao kutumbuliwa


Hii profession ina tabu sana
 
zezeta vip mbona una tabia za ukawa,najua kuacha ni ngumu jitahidi labda kuongeza elimu
 
Back
Top Bottom