"Iringa hakuna ngoma !!" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

"Iringa hakuna ngoma !!"

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ngoshwe, May 9, 2010.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  May 9, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  MKOA WAREJESHA sh.milioni 300 bila kutumia

  Katika hali ya kushangaza na isiyo ya kawaida hata kidogo, Halmashauri za Wilaya Saba za Mkoa wa Iringa zimeshindwa kutumia zaidi ya shilingi milioni Milioni miatatu (300) zilizotolewa na mradi wa Tunajali, kwa ajili ya huduma ya matunzo na matibabu kwa watu wenye virusi vya UKIMWI.

  Fedha hizo zimeshindwa kutumika huku takwimu za Kitaifa zikionesha kwamba mkoa wa Iringa ndio unaoongoza kwa kasi kubwa ya maambukizi ya ugonjwa huo kwa asilimia 15.7 na wakati huo huo, mkoa ukiwa katika utekelezaji wa mkakati wake mpya wa kukabiliana na janga hilo unaolenga kupunguza maambukizi ya ugonjwa huo kwa asilimia hamsini katika kipindi cha miaka minne ijayo.

  Aibu ya kutozitumia fedha hizo ilibainika juzi mjini Iringa kwenye kikao cha Ushauri cha Mkoa wa Iringa (RCC) kilichofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo baada ya Meneja Mipango wa Tunajali mkoani Iringa, Dk. John Kahemele kutoa taarifa hiyo ya kusikitisha.

  Source: Lukwangule Ent.
   
Loading...