kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 9,784
- 20,155
Bunge la Iraq limejibu hatua ya serikali ya Rais Donald Trump wa Marekani ya kuwazuia Waislamu kuingia nchini humo kwa kupasisha sharia inayowapiga marufuku Wamarekani kuingia nchini Iraq.
Ripoti zinasema, katika kikao chake cha kawaida, Bunge la Iraq limepasisha maagizo ya Kamati ya Masuala ya Kigeni yanayoitaka serikali ya nchi hiyo kujibu hatua ya Donald Trump inayowazuia raia wa nchi kadhaa za Kiislamu wakiwemo Wairaq kuingia Marekani kwa kupasisha sheria inayowazuia Warekani kuingia Iraq iwapo Washington haitabadili uamuzi wake.
Sheria ya Bunge la Iraq pia imeutaka Umoja wa Mataifa na jumuiya za kimataifa kama Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kukabiliana ipasavyo na uamuzi wa Rais wa Marekani. Vilevile imeitaka Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) kuitisha kikao cha dharura kwa ajili ya kujadili uamuzi wa Trump ikisisitiza kwamba uamuzi huo unazihusu nchi za Kiislamu.
Bunge la Iraq pia limeitaka Marekani kutengua uamuzi wa kuwazuia Waislamu kuingia nchini humo likisisitiza kuwa unakanyaga na kudharaua mahusiano ya kimataifa.
Baadhi ya Wabunge wa Iraq pia wameitaka serikali ya Baghdad kufuta mikataba yote ya kibiashara na makampuni ya Marekani.
Wakati huo huo Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imetoa taarifa ikisisitiza kuwa, hatua ya Rais wa Marekani ya kuwazuia Waislamu kuingia Marekani ni ubaguzi ambao utayanufaisha makundi ya kigaidi na waungaji mkono wa makundi yenye misimamo mikali.
Ijumaa iliyopita Rais Donald Trump wa Marekani alitia saini amri ya kuwazuia Waislamu kuingia nchini humo kwa kisingizio cha kukabiliana na ugaidi.
Uamuzi huo wa kibaguzi wa Rais Donald Trump wa Marekani umelaaniwa na shakhsia na jumuiya mbalimbali za kimataifa kama Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya, Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis na nchi za Ujerumani, Ufaransa, Canada, Uswisi, Italia na kadhalika.
source:Irib