hamis77
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 18,254
- 26,642
Baghdad inaendelea kunawiri, sio ile Iraq ya mwaka 2003 tena. Miundombinu inarejea, miradi inaongezeka, na mwelekeo wa nchi umebadilika kuelekea maendeleo ya ndani.
Kwa upande wa Wakurdi, Erbil (moja ya jimbo la Iraq) nako kumejengwa kwa kasi. Kuna kauli kwamba kufikia mwaka 2027 hakutakuwa na barabara hata moja ya vumbi. Ni eneo lenye uwekezaji mkubwa na pia kuna kambi/uwepo mkubwa wa kijeshi wa Marekani.
Miaka miwili tayari imepita, na sasa Iraq ipo kwenye miradi mikubwa ya kuifanya iwe nchi ya kisasa, kuanzia barabara, nishati, huduma za miji hadi ajira.
Katika muktadha huu, Muqtada al-Sadr, kiongozi mashuhuri wa Kishia nchini Iraq, alikataa kuiunga mkono Iran katika harakati zake za kijeshi. Alisisitiza kuwa vipaumbele vya Iraq ni kuwapatia wananchi maisha bora, si kuyarudisha maisha ya vita. Ujumbe wake ulikuwa wazi, kwamba,
"Kujenga uchumi na ustawi wa Wairaq ndio kipaumbele cha kwanza."
Je, hali ikoje katika nchi zenu ambazo hazina vita, zinatumia amani hiyo kujenga maisha bora ya wananchi, au zinapoteza fursa hiyo?