Iran yazindua mitambo mipya kabisa ya makombora

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
11,190
Reaction score
24,620
Iran yazindua mitambo mipya kabisa ya makombora katika gwaride la "Siku ya Jeshi"

Mitambo mipya kabisa ya makombora ya vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imezinduliwa katika gwaride maalum lililofanyika mapema leo kwa mnasaba wa "Siku ya Jeshi".

Maadhimisho ya Siku ya Jeshi yamefanyika mapema leo nchini kote, ambapo sambamba na gwaride maalum lililofanyika kwa mnasaba huo, mitambo mipya kabisa ya aina mbalimbali za makombora imezinduliwa pia.

Mitambo ya makombora iliyoundwa na wataalamu wa hapa nchini ya Sayyad 3 na 4, makombora ya Juhudi, kombora la kistratejia la S300 na S200 pamoja na mtambo wa kombora la Mirsad ilizinduliwa katika gwaride hilo lililofanyika leo.

Viongozi na wakuu wa jeshi na wa serikali walihudhuria hafla hiyo iliyofanyika kwa kuzingatia miiko na miongozo ya kiafya.

Baadhi ya askari walioshiriki katika gwaride la Siku ya Jeshi

Kama ilivyokuwa katika mwaka uliopita wa 1399 Hijria Shamsia, gwaride la mwaka huu pia limefanyika katika vituo vyote vikuu vya Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kote nchini kutokana na mazingira ya maambukizi ya virusi vya corona yanayotawala.

Tarehe 29 ya mwezi wa kwanza wa Farvardin, inayosadifiana na tarehe 18 Aprili inaadhimishwa hapa nchini Iran kuwa ni "Siku ya Jeshi".

4by09a898207011utv5_800C450.jpeg
 
Kwani hawajafunga Ramadhani? Naona tunatishiana kuuana.
 
Wafanye kama wamekosea wapige Israel..... [emoji1787][emoji1787]
 
Kwani hawajafunga Ramadhani? Naona tunatishiana kuuana.
Watu wengine huswali/ sali katika nyumba za Ibada Hari wamejifungasha silaha na mabomu wakitoka Hapo kuuwa, kuswali/.sali na kuuwa saa nyingn huwa haviendan au havizuii mipango ya mauaji
 
Mikwala tu hii wenyesilaha kali hawasemi wako kimya! hata uwezo wake unatia shaka kwani shujaa hana huu ujinga,
 
Some of Israel's Offensive and Defensive Weapons:

1618848809365.png
 
Licha ya ya silaha zote hizo za kisasa tena zenye weledi lkn bado rocket za Hama's zilizotengenezwa kienyej zinapenya kwenye ardhi taka tifu
Rocket hizo hazina madhara ukiona zinadondoka ujue ni maeneo ya wazi ambayo hakuna watu wala mali.Hamas ,Syria,Hezbullah na babao Iran,wangekuwa na uwezo na kuishambulia Israel na kuiondoa wangefanya hivyo kitambo,jinsi walivyo na chuki mbaya dhidi ya Israel!
 
Iran yazindua mitambo mipya kabisa ya makombora katika gwaride la "Siku ya Jeshi"

Mitambo mipya kabisa ya makombora ya vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imezinduliwa katika gwaride maalum lililofanyika mapema leo kwa mnasaba wa "Siku ya Jeshi".

Maadhimisho ya Siku ya Jeshi yamefanyika mapema leo nchini kote, ambapo sambamba na gwaride maalum lililofanyika kwa mnasaba huo, mitambo mipya kabisa ya aina mbalimbali za makombora imezinduliwa pia.

Mitambo ya makombora iliyoundwa na wataalamu wa hapa nchini ya Sayyad 3 na 4, makombora ya Juhudi, kombora la kistratejia la S300 na S200 pamoja na mtambo wa kombora la Mirsad ilizinduliwa katika gwaride hilo lililofanyika leo.

Viongozi na wakuu wa jeshi na wa serikali walihudhuria hafla hiyo iliyofanyika kwa kuzingatia miiko na miongozo ya kiafya.

Baadhi ya askari walioshiriki katika gwaride la Siku ya Jeshi

Kama ilivyokuwa katika mwaka uliopita wa 1399 Hijria Shamsia, gwaride la mwaka huu pia limefanyika katika vituo vyote vikuu vya Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kote nchini kutokana na mazingira ya maambukizi ya virusi vya corona yanayotawala.

Tarehe 29 ya mwezi wa kwanza wa Farvardin, inayosadifiana na tarehe 18 Aprili inaadhimishwa hapa nchini Iran kuwa ni "Siku ya Jeshi".

View attachment 1755441
Mkuu nakukubali upo mstari wambele kutupa habari za wa Persian hata kama hazina manufaa kwetu na njaa zetu
 
Back
Top Bottom