Iran yatengeneza kifaa cha kupima kirusi cha Corona

Iran yatengeneza kifaa cha kupima kirusi cha Corona

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
11,190
Reaction score
24,620
Wataalamu Wairani wamefanikiwa kutengeneza kifaa maalumu cha kupima kirusi cha Corona. Kifaa hicho ni cha kwanza cha aina hiyo kuundwa nchini Iran.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Fars, kifaa hicho cha kupima kirusi cha Corona kimeundwa na wataalamu Wairani katika Wizara ya Ulinzi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Kifaa hicho kilichoundwa nchini Iran kina uwezo wa kubaini iwapo mwanadamu ana kirusi cha Corona mwilini na hivyo kutoa mchango mkubwa katika kukabiliana na kirusi cha Corona ambacho pia kinajulikana kama COVID-19.

Tangu kuthibitishwa kwa visa vya kwanza Desemba 2019, homa ya COVID -19 ya kirusi cha Corona ilisambaa na kuwa dharura kuu ya kiafya duniani, na kuua mamia ya watu na kuambukiza maelefu ya wengine.

Homa hiyo iliripotiwa mara ya kwanza katika mji wa Wuhan mkoani Huabei mashariki mwa China na sasa mbali na kuenea katika mikoa 30 nchini China homa hiyo ya Corona imeenea katika zaidi ya nchi 30 zikiwemo Iran, Marekani, Uingereza, Australia, Italia, Thailand, Korea Kusini, Japan, Canada, Ufaransa, Umoja wa Falme za Kiarabu au Imarati.
Kwa mujibu wa takwimu, hadi sasa watu wasiopungua 79,000 wameambukizwa kirusi cha Corona duniani, aghalabu wakiwa nchini China na miongoni mwao 18,000 wamepata nafuu na kuruhusiwa kuondoka hospitalini huku wengine 2, 400 wakipoteza maisha.

4bv5cde9a7bef41l6zv_800C450.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yule naibu waziri anaendeleaje?
 
Ni binaadamu kama mm na ww, au ulitaka kwakua anatoka Iran asiumwe, nyinyi ni waajabu sana
Yule naibu waziri anaendeleaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na hio nyengine umia
Zasingine mtu unaweza kuonekana limbukeni, nchi kibao zinapima korona na hazitangazi kama zimepata wapi vipimo.
Italy, China, misiri, na nyingine zote vipimo wamepata wapi.

Anyway mapenzi ni upofu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Iran’s Nahid 1 satellite ready for launch: ICT minister @azarijahromi

#Iran



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zasingine mtu unaweza kuonekana limbukeni, nchi kibao zinapima korona na hazitangazi kama zimepata wapi vipimo.
Italy, China, misiri, na nyingine zote vipimo wamepata wapi.

Anyway mapenzi ni upofu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kipimo chakupimia korona kimepatikana wapi ?!
Kiufupi mpaka sasa hakuna kipimo maalum chakupimia korona



Kama kipo kinaitwaje ?!

Sent from my SM-G531H using JamiiForums mobile app
 
Kwani China wao wanapima na Nini Corona? Hawa Iran wanatafuta tu kiki Kama wasanii vile.
Mpaka sasa Corona Haina Kipimo Maalum Nandio Maana Kuna Watu Walipimwa Zaidi Yanara Nne Wakawa Hawana Kumbe Wana Maradhi Ila Hakuna Kipimio Maalum

Kama kipo kinaitwaje na huko ulipo taja wametengeneza lini ?!

Maana hili gonjwa nila Mripuko.....

Sent from my SM-G531H using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom