Shadida Salum
Journalist at JamiiForums
- Sep 11, 2020
- 69
- 104
Iran imemnyonga bingwa wa kupiga filimbi ambaye alidai kuwa aliteswa kwa kuchukuliwa video akilazimishwa kufanya maungamo ya uongo kwenye kesi ambayo iliibua kilio cha kimataifa.
Navid Afkari 27, alinyongwa katika gereza la Adelabad lililopo Shiraz nchini humo baada ya kuhukumiwa kwa kosa la kumchoma na kifaa chenye ncha mpaka kufa mlinzi wa kampuni ya maji wakati wa maandamano ya kupinga Serikali mwaka 2018, kilisema chombo cha habari cha serikali siku ya Jumamosi ya tarehe 12 Septemba 2020.
Afkari ambaye ameangukia kwenye hukumu ya kifo, alisema kuwa alishinikizwa kufanya maungamo ya uongo, kwa mujibu wa familia yake, wanaharakati na mwanasheria wake wanasema hakuna ushahidi wa makosa yake. Watu walio upande wake wanamtaja kama ‘ Mfungwa wa kisiasa ‘.
Mwanasheria wake, Hassan Younesi alishutumu mamlaka kwa kumkatalia mteja wake kutembelewa na familia yake kabla ya kunyongwa kama sheria inavyotaka.
Mahakama ya Iran imekanusha madai ya kumtesa, na mahakama kuu nchini humo ilikataa tahakiki ya kesi hiyo mwishoni mwa mwezi wa nane.
Kaka zake Ifkari, Vahid na Habib walihukumiwa kifungo cha miaka 54 na 27 jela kwa kesi hiyo hiyo, hii ni kwa mujibu wa wanaharakati wa haki za binadamu nchini humo.
Mama yao amesema kuwa watoto wake walilazimishwa kutoleana ushuhuda kwa kuteswa.
Shirika la Amnesty International lilisema siku ya Ijumaa ya tarehe 11 Septemba 2020 kuwa Afkari alikua karibu kunyongwa kwa siri , kwenye kuongezea hilo Afkari alipigia simu familia yake tarehe 6 Septemba akisema anapelekwa katika gereza la Adelabab ambalo lina ulinzi wa juu na masharti magumu.
Champion wrestler executed by hanging after being 'tortured into confession'