Iran yakataa kukabidhi Black Box kwa Boeing

Mkuu ebu fikiria vizuri, kama alikuwa hamaanishi hivyo asingeleta mambo ya 1988, tena matukio yanayofanana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani wampe manufacturer achunguze madhaifu ya apichokitengeneza? Inayofautiana VP na polisi waliochunguza kifo cha Akwilina na Mwangosi?
Hicho unachojaribu kukifananisha na kinachoendelea kuhusiana na hiyo ndege havifanani kabisa.

In fact, katika hali ya kawaida tu, mwenye kuunda ama kukitengeneza kifaa husika ana nafasi kubwa zaidi ya kuyajua madhaifu au mapungufu ya kifaa chake alichokiunda yeye mwenyewe.
 
Uko sahihi kiongozi, tatizo linakuja kutokana na hali ilivyo kwa sasa.Sio ajabu Iran ikakosa imani na Boeing.

Sent from my TA-1024 using Tapatalk
 
waanogopa boeing wasije wakapika data
Data zinaweza "kupikwa" hata hapo hapo Iran na hili si jambo ambalo Ukraine ingependa litokee.

Ukraine imeonesha wasi wasi wao juu ya hilo ndiyo maana imetuma kikosi chao kwa ajili ya kufanya uchunguzi juu ya hilo maana hata taarifa za awali za Iran kuhusiana na sababu za ndege hiyo kuanguka zinatia wasiwasi mkubwa.

Ukraine, hata ile taarifa yao ya awali kwamba tukio hilo halikuwa na uhusiano wowote na ugaidi waliifuta haraka hivyo inaonesha dhahiri kwamba kuna sintofahamu hapo.

Hii ndege ilifanyiwa service tarehe 6 mwezi huu wa kwanza, kipindi kifupi kabisa kabla ya ajali hii kutokea na ilionesha kuwa ilikuwa katika hali nzuri tu pia kampuni ya ndege hii inadai kuwa hivi karibuni haikuwahi kuwa na shida zozote za kiufundi.
 
Basi heri wapike wao kuliko Boeing kuja kuwapikia data waonekane wameitungua ndege kama walivyofanya sept 11
 
Taarifa zinasema ndege ilidelay one hour kwa sababu ya mechanical default zilizotekea, wakafanya marekebisho.
Taarifa zisiwe za upande mmoja tuuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Mazingira ya kuanguka kwa hii ndege bado yanatia shaka sana.

Hata kama ilikuwa na hitilafu na ikarekebishwa kabla ya kuondoka kwake, kwanini kuwe na kukatika kwa mawasiano tena kwa ghafla sana?

Kikawaida inapotokea hitilafu katika ndege inapokuwa hewani marubani huwasiliana na kupeana taarifa mara kwa mara na viwanja vya ndege kuhakikisha kwamba usalama unakuwepo.

Taarifa za awali zilidai kuwa ni kufeli kwa engine lakini kilichotokea ghafla ni kukatika kwa mawasiliano. Ni engine failure ya namna gani inayoweza kusababisha kitu cha namna hiyo?
 
Basi heri wapike wao kuliko Boeing kuja kuwapikia data waonekane wameitungua ndege kama walivyofanya sept 11
"Heri wapike wao" ili iweje?

Kumbuka kuwa madhara ya hii ndege hayajaikumba Iran peke yake, kuna raia wa mataifa mengine waliokufa katika ajali ya ndege hiyo isitoshe ndege hiyo si mali yao hivyo uchunguzi makini na wa uhakika unahitajika kufanywa ili kuweza kupata ufumbuzi juu ya chanzo cha ajali hii.
 
Uko sahihi kiongozi, tatizo linakuja kutokana na hali ilivyo kwa sasa.Sio ajabu Iran ikakosa imani na Boeing.

Sent from my TA-1024 using Tapatalk
Ajali hii haijaiathiri Iran pekee. Mataifa mbalimbali yamepata athari kutokana na kuanguka kwa ndege hii.

Sasa, Iran peke yake inapokosa imani na chombo husika kilichounda ndege hiyo na kuifanyia ukaguzi wa kiusalama ina maana gani?
 
Huwezi kumuamini adui yako Iran yuko sawa maana hawakawii kuja na uongo Wamarekani siyo wa kuwaamini
 
Ndege aikufika mbali taarifa zilizopo baada ya dakika mbili tu kuacha runway ikalipuka.

Ilichelewa kwa lisaa limoja au mawili kupaa depending on the source kwa sababu ya technical issues

Ukraine wanadai ndege bado nzuri ndio kwanza ina miaka minne ya operation na imetoka full service sio muda mrefu aikuwa na shida.

As a model ni moja ya ndege yenye record nzuri duniani when it comes to safety

Raia waliokufa wengi ni wa Iran kuliko nchi nyingine

Iran aitaki kutoa blackbox

Hizo ndio habari za ajali anyone can fill the box to what actually happened based on those facts.
 
Victoireeeeee.......................


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasaivi Iran inaonekana chungu sana aiseee kwa mataifa ya magharibi, Umoja wao ndio ulipowafikisha apa, hongera sana Iran kwa ujasiri uliouonesha, hapa nimejifunza ktk maisha apana kukata tamaa licha ya changamoto unazopitia


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…