Iran yajenga kiwanda cha tatu cha makombora chini ya ardhi

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,784
20,155
Iran imejenga kiwanda cha tatu cha makombora chini ya ardhi
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imejenga kiwanda cha tatu cha chini ya ardhi cha kuzalisha makombora ya kujihami.
Hayo yamedokezwa na Brigedia Jenerali Amirali Hajizadeh, kamanda wa kitengo cha anga cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH ambaye ameongeza kuwa, Iran itaendelea kuimarisha uwezo wake wa kujihami kutokana na vitisho vya maadui vinavyoikablia nchi hii.
Akizungumza jana Alkhamisi katika mji wa Dezfoul wa kusini magharibi mwa Iran, Hajizadeh amesema, uwezo mkubwa wa viwanda vya makombora wa Iran ni jambo ambalo limepelekea maadui wadhihirishe wazi upinzani wao kwa hatua ya nchi hii kumiliki teknolojia ya kujiundia makombora ya kila namna.
Kamanda huyo wa ngazi za juu amesema vifaa vyote vya kimsingi vya kuundia makombora vinategenezwa na wataalamu wa Iran. Aidha amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina azma ya kuimarisha uwezo wake wa makombora na kuongeza kuwa: "Ni jambo linalotarajiwa kwa Marekani na Israel kuingiwa na wasi wasi na kiwewe kutokana na uzalishaji wetu wa makombora na kuyafanyia majaribio na pia kuwepo miji ya chini ya ardhi iliyojaa makombora." Amesema, Wamarekani na Wazayuni daima wamekuwa wakitamani kuiona Iran ikiwa ni nchi dhaifu.
Brigedia Jenerali Amirali Hajizadeh alisema: "Natangaza hapa kuwa, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran limeshazindua kiwanda chake cha tatu cha chini ya ardhi cha kuzalisha makombora.
Mwezi Januari mwaka 2016, Shirika la Utangazaji la Iran IRIB lilirusha hewani mkanda wa video wa ghala kubwa la chini ya ardhi ambalo lilikuwa limejaa makombora ya balisitiki ya Imad yaliyoundwa na wataalamu wa Iran. Kiwanda cha kwanza cha chini ya ardhi cha makombora cha SEPAH kilizinduliwa Oktoba 14 mwaka 2015.
My take; Jamaa wamejipanga haswa sio wa kisport sport
source: Parstoday
 
Tehtehteh maIRAN kiboko. C ajabu zaidi ya vitatu wanavyo,, haya maji2 yamesoma bwana.
 
Wacha wamiliki silah kikiripuka wajuwe kutumia wamezungukwa na maadui wengi tu
 
Jambo la kushukuru siku irani ikiweza kumsambaratisha wakala wa ugaidi duniani saudi Arabia kwa udhamini wa marekani dunia itakuwa salama maana!!!
Ima saudi isambaratishwe au marekani ndio ugaidi na vikundi vya kigaidi vitaisha na dunia kuwa salama
 
Iran sio Libya wala Syria..ilishajijenga kikamilifu kijeshi ndio mana Israel hasogei pale kienyeji kama anavyopiga syria kila ujao..
 
Iran sio Libya wala Syria..ilishajijenga kikamilifu kijeshi ndio mana Israel hasogei pale kienyeji kama anavyopiga syria kila ujao..
Yaani Huyo Iran, Israel ndiyo hana wasiwasi naye kabisa.
Kingine unachopaswa kufahamu ni kwamba hats huo mfumo wa jamhuri ya kiislam wala so matakwa ya wa Iran Bali ni matakwa ya Marekani maana ndiyo wameuuweka pale. Na wakichoka nayo wataufagia tu na hakuna wa kuwazuia
 
Sisi wataalamu wetu wanabishana kama mafuta yaliyo bandarini ni crude au ni semi refined!! hahahaaahaha sizonje tupeleke baba
 
Jambo la kushukuru siku irani ikiweza kumsambaratisha wakala wa ugaidi duniani saudi Arabia kwa udhamini wa marekani dunia itakuwa salama maana!!!
Ima saudi isambaratishwe au marekani ndio ugaidi na vikundi vya kigaidi vitaisha na dunia kuwa salama
Utajiri wa mmarekani unatokana na mauaji yake anayoyafanya duniani, aidha kwa kuwapa silaha magaidi au vikundi vya waasi au kusambaza virusi mbalimbali na tiba inapatikana America tu Kama Ebola...
 
Back
Top Bottom