Waziri wa Kaskazini
JF-Expert Member
- Dec 12, 2015
- 8,714
- 19,297
Iran imeikamata meli nyengine ya mafuta katika Ghuba, kulingana na vyombo vya habari vya Iran . Kamanda wa Jeshi la Iran la Revolutionary Guard alinukuliwa akisema kuwa wanamaji wa taifa hilo waliikamata meli ya kigeni ya mafuta katika Ghuba la Persia ambayo ilikuwa ikiyasafirishia baadhi ya mataifa ya Kiarabu mafuta kwa njia ya magendo . Imesema kuwa meli hiyo ilikuwa ikibeba 700,000 za mafuta akiongezea kuwa mabaharia saba wanazuiliwa.
Kisa hicho kinajiri huku kukiwa na hali ya wasiwasi baada ya Marekani kuiongezea vikwazo Iran katika sekta ya mafuta. Vikwazo hivyo viliwekwa tena baada ya Washington kujiondoa katika makubaliano ya kinyuklia ya Iran yalioafikiwa 2015. Hii ni mara ya pili Iran imeishutumu meli ya kusafirisha mafuta kinyume na sheria. Mnamo mwezi Julai , walinzi wa pwani ya Iran waliikamata meli iliokuwa ikipeperusha bendera ya Panama MT Riah.
Jeshi la Revolutionbary Guard , kwa mujibu wa mtandao wa Sepah News lilisema kuwa meli hiyo ilikamatwa wakati wanamaji wake walipokuwa wakipiga doria zenye lengo la kuwatafuta wale wanaofanya biashara haramu ya mafuta. Pia mwezi uliopita , Iran iliikamata meli iliokuwa ikipeperusha bendera ya Uingereza kwa jina Stena Impero katika mkondo wa Hormuz ikidai kwamba meli hiyo iligongana na meli ya wavuvi wa samaki na kutoroka.
Marekani imeilaumu Iran kwa mashambulizi mawili ya kutumia vilipuzi katika Ghuba ya Oman mnamo mwezi Mei na Juni madai ambayo Tehran imekana.
Source Bbc