Iran wazindua submarine mpya yenye uwezo wa kubeba makombora ya Cruise

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
5,205
2,000
Iran yazindua nyambizi mpya yenye makombora ya cruise
Feb 18, 2019 02:33 UTC
Rais Hassan Rouhani wa Iran amezindua nyambizi ya kisasa iliyoundwa hapa nchini ambayo ina uwezo wa kusheheni makombora ya cruise.
Nyambizi hiyo iliyopewa jina la Fateh imezinduliwa katika sherehe iliyofanyika Jumapili katika mji wa bandarini wa Bandar Abbas.
Nyambizi ya Fateh ambayo kwa asilimia 100 imeundwa kwa kutegemea teknolojia iliyobuniwa na wataalamu Wairani inaweza kuenda mita 200 katika kina cha bahari kwa muda wa wiki tano mfululizo.
Nyambizi hii ambayo ni ya kwanza ya aina yake inayomilikiwa na Iran ina uwezo wa kubeba na kufyatua makombora ya cruise ikiwa chini ya maji.
Aidha nyambizi hiyo yenye uzito wa tani 527 ina silaha nyingine za kisasa kama vile torpedo na mabomu ya chini ya maji.
Hali kadhalika nyambizi ya Fateh ina mfumo erevu wa kuongoza makombora na rada ya kisasa aina ya Sonic ambayo inaweza kutambua haraka manowari za kivita za adui.
Mwezi Novemba mwaka 2018 pia Iran ilizindua nyambizi mbili za daraja la Ghadir ambazo zina uwezo wa kurusha makombora kutoka chini ya bahari.
Katika miaka ya hivi karibuni Iran imeweza kuzindua nyambizi kadhaa za kisasa zilizoundwa humo nchini kama vile Qaem, Nahang, Tareq na Sina.
 
Janken jr

JF-Expert Member
Sep 14, 2016
1,128
2,000
tanzania inazindua kampeni bungeni ya kukabiliana na mkono wasweta kwa wabunge wanaume,hii ni naada ya mbunge mmoja wa kike kula tunda na baadhi ya wabunge wa kiume na kugundua wana mkono wa sweta.
 
profesawaaganojipya

JF-Expert Member
Apr 21, 2015
512
1,000
Iran yazindua nyambizi mpya yenye makombora ya cruise
Feb 18, 2019 02:33 UTC
Rais Hassan Rouhani wa Iran amezindua nyambizi ya kisasa iliyoundwa hapa nchini ambayo ina uwezo wa kusheheni makombora ya cruise.
Nyambizi hiyo iliyopewa jina la Fateh imezinduliwa katika sherehe iliyofanyika Jumapili katika mji wa bandarini wa Bandar Abbas.
Nyambizi ya Fateh ambayo kwa asilimia 100 imeundwa kwa kutegemea teknolojia iliyobuniwa na wataalamu Wairani inaweza kuenda mita 200 katika kina cha bahari kwa muda wa wiki tano mfululizo.
Nyambizi hii ambayo ni ya kwanza ya aina yake inayomilikiwa na Iran ina uwezo wa kubeba na kufyatua makombora ya cruise ikiwa chini ya maji.
Aidha nyambizi hiyo yenye uzito wa tani 527 ina silaha nyingine za kisasa kama vile torpedo na mabomu ya chini ya maji.
Hali kadhalika nyambizi ya Fateh ina mfumo erevu wa kuongoza makombora na rada ya kisasa aina ya Sonic ambayo inaweza kutambua haraka manowari za kivita za adui.
Mwezi Novemba mwaka 2018 pia Iran ilizindua nyambizi mbili za daraja la Ghadir ambazo zina uwezo wa kurusha makombora kutoka chini ya bahari.
Katika miaka ya hivi karibuni Iran imeweza kuzindua nyambizi kadhaa za kisasa zilizoundwa humo nchini kama vile Qaem, Nahang, Tareq na Sina.
hawa watu si wa kuwaamini sana,wakati mwingine wanataka kuwatisha israel na marekani.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom