Iran waongeza ujuzi wabuni teknolojia ya makombora ya supersonic

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,000
17,909
Aug 10, 2023 07:44 UTC

Wataalamu wa kijeshi na wahandisi katika Wizara ya Ulinzi ya Iran wameripotiwa kubuni teknolojia ya kutengeneza ndani ya nchi kombora la kisasa la cruise kenye uwezo wa kusafiri kwa mwendo kasi wa supersonic.

Kombora hilo lililotengenezwa ndani ya nchi limearifishwa kama kizazi kipya cha makombora ya cruise ya Iran na kwa sasa liko katika hatua ya majaribio. Hayo yaliripotiwa jana na Shirika la Habari la Tasnim lenye makao makuu yake mjini Tehran.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa kombora hilo litafungua ukurasa mpya katika teknolojia ya ulinzi ya Iran, kwani ni vigumu sana kulinasa kombora la cruise linaloruka kwa kasi ya supersonic.

Hadi sasa, makombora ya cruise ya Iran yamekuwa yakitegemea sana mfumo wa injini wa RATO kwa ajili ya kurushwa hewani katika hatua ya kwanza na injini ya Turbojet iliyopewa jina la Tolou’ (macheo) katika hatua ya pili.

Kuanza kutumika injini za ramjet katika makombora ya cruise baharini na utengenezaji wa makombora ya supersonic nchini ni muhimu sana, kwani yataimarisha sana uwezo wa Iran kukabiliana na adui endapo patatokea makabiliano yoyote ya kijeshi na kuzuia vikosi vamizi kuchukua hatua za kulipiza kisasi kwa wakati unaofaa.

Wataalamu na wahandisi wa kijeshi wa Iran katika miaka ya hivi karibuni wamepata mafanikio makubwa katika utengenezaji wa aina mbalimbali wa zana za kivita ndani ya nchi, na hivyo kuvitosheleza vikosi vyake vya kijeshi na kuvifanya visitigemee msaada wa kigeni.

Viongozi wa nchi wanasisitiza mara kwa mara kwamba nchi haitasita kuimarisha uwezo wake wa kijeshi, ikiwa ni pamoja na uwezo wa makombora kwa ajili ya kujilinda dhidi ya adui, na kwamba Iran haitafungua mlango wa majadiliano na yeyote yule kuhusu suala hilo

Makombora ya supersonic ya Iran

4c3o1d7706a7f92cccu_800C450.jpg
 
Netanyahu akisikia hivi huww mzigo unagonga chupi ,alitaka yeye awe peke yake kwenye anga
 
Back
Top Bottom