Iran:Hatuna mpango wa kumiliki silaha za nyuklia

Iran:Hatuna mpango wa kumiliki silaha za nyuklia

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
11,190
Reaction score
24,620
Waziri wa mambo ya nje wa Iran, Mohammad Javad Zarif ameijibu Serikali ya Marekani baada ya rais Donald Trump kudai kuwa nchi yake haina nia ya kushinikizo mabadiliko ya kiutawala nchini Iran, badala yake inataka utawala wa Tehran uachane na urutubishaji wa nyuklia.


Kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Twitter, Zarif amesema Iran haina mpango wa kuwa na silaha za nyuklia na kuituhumu Marekani kwa kuendelea kuongeza wanajeshi kwenye eneo la mashariki ya kati hali inayozidisha sintofahamu zaidi kwenye ukanda.

Kiongozi wa kidini wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei alishawahi kusma kuwa nchi yake haina mpango wowote wa kuwa na silaha za nyuklia, ambapo alitoa makataa ya kuhakikisha hakuna utengenezaji wa silaha hizo, alinukuliwa Zarif.

Matamshi yake yamekuja baada ya Jumatatu ya wiki hii rais Trump akiwa nchini Japan, kudai kuwa Marekani inataka kuhakikisha kunapatikana makubaliano mazuri ya mpango wa nyuklia wa Iran na sio vinginevyo.

Rais Donald Trump alivyoingia madarakani alitangaza kuitoa nchi yake katika mkataba wa nyuklia wa Iran uliotiwa saini na mataifa 6 yenye nguvu duniani, ambapo akatangaza vikwazo vya kiuchumi dhidi ya utawala wa Tehrani.

Lakini tangu juma lililopita Marekani ilianza kutuma meli zake za kivita pamoja na wanajeshi zaidi kwenye eneo la mashariki ya kati kwa kile utawala wa Washington unasema inataka kukomesha hatari ya nchi ya Iran kwa nchi washirika za ukanda.

Mwezi Octoba mwaka jana rais wa Iran, Hassan Rouhani alidai kuwa utawala wa Marekani unafanya njama kuhakikisha kunakuwa na mabadiliko ya utawala tuhuma ambazo sasa rais Trump anakanusha.

Viongozi wa Tehran hata hivyo licha ya vikwazo na vitisho vya Marekani na nchi washirika, wameendelea kusisitiza kutotetereka huku wakitoa wito kwa mataifa ya ulaya ambayo yamesalia kwenye mkataba uliopo kuilinda nchi yake.

Mwezi uliopita Iran ilitishia kujitoa kwenye mkataba huo na kuanza upya urutubishaji wa Urani ikiwa nchi za Ulaya hazitasimama kidete kuhakikisha mkataba uliopo unatekelezwa.


FB_IMG_15583783312903391.jpg
 
Bahram Qassemi: Silaha za nyuklia hazimo kabisa katika ajenda ya ulinzi ya Iran
Mei 28, 2019 08:04 UTC
Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Paris Ufaransa amesema kuwa, silaha za nyuklia kamwe hazijawahi kuwemo kenye ajenda ya kiulinzi ya Jamhuri ya Kiislamu.
Bahram Qassemi alisema hayo jana katika mkutano wa "Kupunguza Wasiwasi katika eneo la Ghuba ya Uajemi" na kusisitiza kuwa, kamwe silaha za nyuklia hazijawahi kuwemo katika ajenda za kiulinzi za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kwamba mbali na jambo hilo kuwa na nguvu za fatwa ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu linatiliwa nguvu pia na mapatano ya JCPOA na ripoti 14 za Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA zinazothibitisha kuwa miradi ya nyuklia ya Iran ni ya amani kikamilifu na haihusiani kabisa na silaha za atomiki.
Qssemi ambaye zamani alikuwa msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran vile vile amesema kuwa, kustafidi na teknolojia ya nyuklia katika masuala ya kiraia yasiyo ya kijeshi kumetiliwa mkazo pia na makubaliano ya nyuklia ya JCPOA ni hilo ni katika haki za kimsingi za taifa la Iran.
Balozi huyo wa Iran nchini Ufaransa vile vile amesema kuwa, kupatikana amani, usalama na utulivu katika eneo hili kutawezekena pale tu manufaa ya nchi zote za Ghuba ya Uajemi yatakapoheshimiwi.
Amesema, Tehran inaamini kwamba nchi yoyote katika eneo hili haiwezi kuleta amani, utulivu na usalama bila ya kushirikiana na nchi nyingine za Ghuba ya Uajemi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom