Kiongozi Muadhamu: Baadhi ya viongozi wa nchi za Kiislamu ni vibaraka wa Marekani na Wazayuni
Apr 15, 2019 14:43 UTC
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, baadhi ya viongozi wa nchi za Kiislamu hawafanyii kazi maamrisho ya Qur'ani na ni vibaraka wa Marekani na Wazayuni.
Ayatullah Ali Khamenei amesema hayo leo hapa mjini alipokutana na washiriki wa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani na kusisitiza kuwa, kuifanyia kazi Qur'ani Tukufu kunaandaa uwanja wa kupatikana izza (heshima), ustawi, maendeleo, nguvu, mshikamano, mtindo mzuri wa maisha katika dunia na kudhaminiwa saada na ufanisi wa Akhera.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amebainisha kwamba, baadhi ya viongozi wa nchi za Kiislamu wamekuwa chanzo na chimbuko la hitilafu, mifarakano na vita kama vya Syria, Yemen na kuuawa Waislamu.
Ayatullah Khamenei amesisitiza kuwa, matatizo na masaibu mengi ya Umma wa Kiislamu na jamii ya wanadanmu yanatokana na kutoyafanyia kazi maarifa ya Qur'ani Tukufu.
Aidha Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa, hii leo kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hali ya wananchi hasa vijana kuyapokea na kushikamana na mafundisho ya Qur'ani Tukufu imekuwa ikiongezeka siku baada ya siku; na kwamba, hii hali ya kushikamana na Qur'ani Tukufu ndio itakayokuwa chimbuko la saada, nguvu na heshima ya mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu.
Ayatullah Khamenei, ameashiria uadui dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusisitiza kwamba, licha ya kuwa uadui huo umeongezeka kuliko huko nyuma, lakini inaonekana kuwa, hatua na njama hizi zinavuta pumzi zake za mwisho.
Sent using
Jamii Forums mobile app