IPTL/PAP wamvaa David Kafulila

shadow recruit

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2011
Posts
1,844
Reaction score
384

Chanzo: GAZETI LA MAJIRA 8th October 2014
 
Kafulila atakoma kuingilia mambo ya kampuni binafsi, hivi kwani hawezi kupigania viwanda vya mawese vinavyoendela kufilisika kila siku huko kigoma badala ya kuingilia kampuni ambayo iko pale kisheria

''Tunapenda kuwasisitizia watanzania waendelee kumpuuza mtu huyu kwani kwa sasa amevurugwa ndio maana anahamishahamisha mijadala na kiasi cha kumhusisha Waziri Mkuu, Baraza la Mawaziri huku akijua ESCROW ni jambo la kisheria na si la kisiasa na yalikuwa malipo halali kwa IPTL/PAP na huo ndio ukweli na utaendelea kuwa hivyo, na ningemshauri Kafulila ajifunze nini maana ya ESCROW hata kwa njia ya mtandao

ili siku nyingine asiendelee kulishwa ujinga wa namna hii bila kujua ukweli wa ndani kufanya hivyo ni kufedhehesha watanzania kwamba wanawachagua wabunge wenye uelewa mdogo kama Kafulila''. ilisema taarifa hiyo.

Ilisema uelewa finyu huu wa Kafulila unamsababisha ashindwe kutofautisha kati ya mali ya umma na mali binafsi, fedha za umma zilizopo BoT na uwakala wa ESCROW wa BoT, kazi za serikali na kazi za mbunge kazi za IPTL/PAP na kazi za TANESCO tunasisitiza IPTL/PAP sio shirika la Umma wala mali ya serikali,

Kafulila na wenzake waelekeze nguvu katika mashirika ya umma yanayofilisika kila kukicha huku na yeye akiwa sehemu ya ufilisi huo, Watanzania tuwapuuze wabunge vibiriti fitini kama Kafulila na wenzake waliokubali kuweka pembeni uelewa wao na kutumika na makampuni shindani dhidi yetu pamoja Standard Chartered, vinginevyo ajiseme hadharani yeye ni mbia wa Standard Chartered.

Hivyo, tunawahakikishia watanzania tutaendelea kuzalisha na kuwauzia umeme wa uhakika na kwa bei nafuu na mchakato wetu wa kushusha bei ya umeme kutoka 450 ya sasa kwa uniti mpaka sh. 80 uko mbioni kukamilika ili watanzania wafurahie huduma ya umeme na wachagize maendeleo yao japo kina Kafulila na wapinzani wetu wa kibiashara hawapendi watanzania wafaidi matunda yao
 
nini tena jaman mbona mnanitisha

''Tunapenda kuwasisitizia watanzania waendelee kumpuuza mtu huyu kwani kwa sasa amevurugwa ndio maana anahamishahamisha mijadala na kiasi cha kumhusisha Waziri Mkuu, Baraza la Mawaziri huku akijua ESCROW ni jambo la kisheria na si la kisiasa na yalikuwa malipo halali kwa IPTL/PAP na huo ndio ukweli na utaendelea kuwa hivyo, na ningemshauri Kafulila ajifunze nini maana ya ESCROW hata kwa njia ya mtandao

ili siku nyingine asiendelee kulishwa ujinga wa namna hii bila kujua ukweli wa ndani kufanya hivyo ni kufedhehesha watanzania kwamba wanawachagua wabunge wenye uelewa mdogo kama Kafulila''. ilisema taarifa hiyo.

Ilisema uelewa finyu huu wa Kafulila unamsababisha ashindwe kutofautisha kati ya mali ya umma na mali binafsi, fedha za umma zilizopo BoT na uwakala wa ESCROW wa BoT, kazi za serikali na kazi za mbunge kazi za IPTL/PAP na kazi za TANESCO tunasisitiza IPTL/PAP sio shirika la Umma wala mali ya serikali,

Kafulila na wenzake waelekeze nguvu katika mashirika ya umma yanayofilisika kila kukicha huku na yeye akiwa sehemu ya ufilisi huo, Watanzania tuwapuuze wabunge vibiriti fitini kama Kafulila na wenzake waliokubali kuweka pembeni uelewa wao na kutumika na makampuni shindani dhidi yetu pamoja Standard Chartered, vinginevyo ajiseme hadharani yeye ni mbia wa Standard Chartered.

Hivyo, tunawahakikishia watanzania tutaendelea kuzalisha na kuwauzia umeme wa uhakika na kwa bei nafuu na mchakato wetu wa kushusha bei ya umeme kutoka 450 ya sasa kwa uniti mpaka sh. 80 uko mbioni kukamilika ili watanzania wafurahie huduma ya umeme na wachagize maendeleo yao japo kina Kafulila na wapinzani wetu wa kibiashara hawapendi watanzania wafaidi matunda yao.
 
wala hamna haya kupoteza muda kumpuuza kafulila,wabunge wenzake wameshamdharau kwa kupokea hongo,hana support ya mmbunge wowote wa upinzani, wote wanajua jamaa ana tamaa sana
 
Sasa hii habari mbona magazeti yote imeandaliwa na mwandishi wetu ? Ndio matumizi ya mabilioni yetu yanafanya kazi ....

Mkuu ushaanza kutafuta sababu tena du kweli nimeamini kigoma line ni wabishi maana apo kungeuwa amna source ungeuliza iko wapi ila now umeona source ipo unaanza habari mbona za mwandishi wetu acha umbulula wewe mkuu jadili hoja kwa fact
 
unajua si kila hoja mtu anatakiwa kujadili nyingine unapotezea tu, so anaweza kupotezea tu mada.
 
Kafulila atakoma kuingilia mambo ya kampuni binafsi, hivi kwani hawezi kupigania viwanda vya mawese vinavyoendela kufilisika kila siku huko kigoma badala ya kuingilia kampuni ambayo iko pale kisheria

Watu wote wanaodhani mh david kafulila anaota wasome the citizen ya leo tar 8 October 2014 front page.
tuhuma za Kafulila Na ZZk zina mashiko ndio maana Development partners kupitia mwenyekiti wa Balozi wa finland hapa nchini Ms Sinikka Antila; wamefunguka rasmi kwamba wamezuia shilingi trilioni moja pending report ya CAG kuhusu fedha za Escrow account/IPTL; kama Kafulila anagekuwa anaota mchana wale DP's wana vyanzo vingi credible vya kujua ukweli na uongo wa taarifa nyeti kama hizo wasingetoa tamko kama hili la leo!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…