IPTL/PAP: Hatuna kesi na TANESCO

PINDA AWASHANGAA WAFADHIRI!!!!!!!!!

NA MWANDISHI WETU.
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda,ameshangazwa na baadhi ya wafadhili kusitisha misaada kwa Tanzania kutokana na kashfa ya kuchotwa kwa mabilion ya shilingi kwenye akaunti ya ESCROW ya kampuni ya IPTL.
Amesema wafadhili hao wamechukua uamuzi wa haraka kwa kuwa serikali imeanza kuchukua hatua ikiwa ni pamoja na kuagiza kufanyika kwa uchunguzi ili kubaini ukweli.
Hata hivyo amesema serikali imekuwa ikichukua hatua madhubuti katika kupambana na rushwa na matumizi mabaya ya fedha za umma.
Ukaguzi huo unasimamiwa na ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
Hatua ya serikali kuagiza kufanyika kwa uchunguzi kuhusiana na mikataba ya IPTL, inatokana na wabunge wakiongozwa na David Kafulila (Kigoma kusini-NCCR Mageuzi) kumtuhumu mmiliki mpya wa kampuni ya IPTL/PAP,kuchota fedha hizo kwa njia isiyo halali.
Akihojiwa na shirika la utangazaji la uingereza (BBC) juzi usiku,Pinda alisema uamuzi wa wafadhili kusitisha misaada ulipaswa kusubiri taarifa ya uchunguzi unaoendelea umalizike na kwamba kilichofanyika sasa ni sahihi.
"Ni kweli wamechukua uamuzi wa kusitisha misaada lakini wamefanya hivyo haraka sana.Si kweli kwamba Tanzania tunafanya vizuri kukabiliana na rushwa,"alisema.



 
IPTL hawana kesi na TANESCO kama wanasiasa wetu uchwara wanavyodai!

Mwaka 2006 serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupitia Wizara ya Nishati na Madini, shirika la IPTL na Benki Kuu ya Tanzania (wakala) kutokana na Mkataba wa kuzalisha na kuuza umeme kutoka IPTL kwenda TANESCO kulianzishwa akaunti ya ESCROW.
MAtakwa ya makubaliano ya kuanzishwa na kutekelezwa kwa mradi wa kujenga, kuendesha na kuzalisha umeme wa kuuza kati ya kampuni binafsi ya IPTL na TANESCO ni kwa serikali kufungua letters of credit au kufungua akaunti ya ESCROW.

Akaunti hiyo siyo fedha za serikali bali ni fedha ambazo ziliwekwa kutokana na matakwa ya mkataba wa kuuza umeme kwa TANESCO kutoka kampuni binafsi. Katika mkataba wa kufungua akaunti ya ESCROW kuna kifungu kinasomeka, "required amount means the amount in Tshs. That the government of Tanzania shall deposit from time to time in the ESCROW account which equals not less than two months estimated tariff payments under the PPA, provided that such amount shall be adjusted annually by IPTL and TANESCO pursuant in the PPA in the article 11 hereof, and government of Tanzania will be entitled will be entitled to review independently, the calculation of the required amount pursuant to this agreement".
Tafsiri yake kwa Kiswahili ni kwamba "kiasi kinachopaswa kuingizwa na serikali katika akaunti ya ESCROW ni kile ambacho kinalingana na madai ya malipo sawa na miezi miwili ya gharama ya kuuza umeme ambazo IPTL inadai TANESCO, IPTL na TANESCO watafanya marejeo kuhusiana na kiasi cha gharama za umeme kila mwaka. Hayo ni kwa mujibu wa makubaliano ya kuuza na kununua umeme kwa mujibu wa makubaliano ya mkataba wa mauzo ya umeme (Power Purchasing Agreement) au kwa kifupi PPA na kama ilivyobainishwa kwenye kifungu cha 11. Serikali itakuwa huru kufanya tathmimini yake kuhusu gharama halisi za uzalishaji na uuzaji wa umeme kwa mujibu wa mkataba wa PPA.
Wakati akaunti ya ESCROW inafunguliwa serikali na IPTL walikuwa katika mahakama ya usuluhishi ya ICSD ambapo suala la gharama za capacity charge lilikuwa linagombewa. Hivyo serikali ya Tanzania ilikataa madai ya kulipa dola za kimarekani milioni 3.6 kwa ajili ya capacity charge.
Katika Mahakama ya Usuluhishi fedha ambazo zilikubaliwa ni dola za Kimarekani millioni 120 na hivyo gharama za capacity charge kuteremshwa kufikia dola za Kimarekani milioni 2.6. Hivyo mgogoro kati ya serikali na IPTL ukawa umekwisha.
Kumalizika kwa mgogoro huo kunamaliza utata wote wa serikali kuwa na madai katika akaunti ya ESCROW, isipokuwa yale yanayohusu kodi ambazo TRA itakuwa inadai wakati akaunti ya ESCROW itakuwa imefunguliwa kwa wahusika kwa makubaliano ya kutoa fedha au pale fedha kutoka akaunti ya ESCROW zitakuwa zimetolewa na kuwekezwa katika vitega uchumi kama inavyoelezwa katika kifungu cha 3 kinachohusu uwekezaji wa fedha katika akaunti ya ESCROW.
Inaelezwa kwamba shria za Tanzania ndiyo zitatumika katika uthibiti wa fedha za akaunti ya ESCROW. Mtazamo huu wa sheria unazingatia matakwa ya usuluhishi ya Mahakama ya kimataifa ya usuluhishi ICSID ambayo inatamka wazi kwamba wahusika wanakubali kwamba IPTL inathibitiwa na Nationals na hivyo itachukuliwa kuwa shirika la Tanzania kwa madhumuni na matakwa ya makubaliano ya mkataba wa kimataifa. Na wakala wa akaunti ya ESCROW anathibitiwa na serikali ya Tanzania na hivyo anatambuliwa kama taasisi ya kitanzania kwa madhumuni ya mkataba wa ICSID.
Hivyo alipopatikana mnunuzi PAP ambaye alikubaliana kununua hisa za VIP Engineering and Marketing shirika hilo ambalo linamiliki aslimia 30% ya hisa zote, ilikuwa sahihi aondoe kesi ya kutaka IPTL ifunge hughuli zake na wabia wagawane mali. Mahakama Kuu haikukosea kukubaliana na VIP Engineering and Marketing kuondoa kesi na hivyo kufungua milango kwa mmiliki wa hisa zote 100% kuchukua fedha zilizokuwa Benki Kuu kwenye akaunti ya ESCROW.
 

Wamesha elewa. Ripoti inakuja kufunika kabisa, nakuwapoteza wanasiasa uchwara.
Nakaonea huruma katumbili nakumbuka siku zile alipokuwa analilia ubunge wake mpaka kamasi zinamtoka huku akitembea kwa magoti kumfata mbatia amsamehe. Dahhh!
 

Kafulila na wenzake waelekeze nguvu katika mashirika ya umma yanayofilisika kila kukicha huku na yeye akiwa sehemu ya ufilisi
huo, Watanzania tuwapuuze wabunge vibiriti fitini kama Kafulila na wenzake waliokubali kuweka pembeni uelewa wao na kutumika na makampuni shindani dhidi yetu pamoja Standard Chartered, vinginevyo ajiseme hadharani yeye ni mbia wa Standard Chartered.
 

Definition: An escrow account is a temporary pass through account held by a third party during the process of a transaction between two parties. This is a temporary account as it operates until the completion of a transaction process, which is implemented after all the conditions between the buyer and the seller are settled
 
Wamesha elewa. Ripoti inakuja kufunika kabisa, nakuwapoteza wanasiasa uchwara.
Nakaonea huruma katumbili nakumbuka siku zile alipokuwa analilia ubunge wake mpaka kamasi zinamtoka huku akitembea kwa magoti kumfata mbatia amsamehe. Dahhh!

Definition: An escrow account is a temporary pass through account held by a third party during the process of a transaction between two parties. This is a temporary account as it operates until the completion of a transaction process, which is implemented after all the conditions between the buyer and the seller are settled
 

Premier Pinda said there was no need to raise tensions as the escrow account was not for the public but rather was between IPTL and the Tanzania Electric Supply Company –Tanesco
 
Watu wengi waliongopewa kuhusu ili jambo la iptl!!
Bora sasa kidogo waru wameanza kupata ufahamu kuhusu hii issue
 
Mi nasubiri kifo rasmi cha kafulila na wenzake kisiasa..ujinga tu ndo umetawala kwenye hizo arguments zao..sioni huo wizi ukitangazwa..aibu yao,Ngoja tuone ngoma ya matumbili inaishia wapi!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…