IPSO FACTO: CHADEMA AND CUF MUST 'RESIGN'! So as you...if..! TUACHE UNAFIKI

mmh kazi kweli hapo....ila kwa taarifa tu mi nshaingia gym...road to 2015,ngumi lazima zilike tu!!!!
 
Binafsi namuunga mkono mambo mengi waberoya,pamoja na mazingira magumu ya kisiasa ya tanzania lakini inafikia hatua inakatisha tamaa,kuna matukio mengi ambayo cdm(wanaokubalika zaidi kwa sasa) kama wangeyatumia vizuri wangechukua nchi au kuleta mabadiliko makubwa,lakini naona wanapita njia zile zile zilizofanya vyama vingi kufeli.kama alivyosema mwanakijiji,cdm imepata publicity kubwa kuweza kuleta mabadiliko makubwa lakini naona cdm wanaanza kuimba nyimbo ambazo ccm wanataka cdm waimbe.mzaha mzaha miaka mingine 5 itapita,matokeo ya uchguzi tuliyohaidiwa na cdm hakuna,wabunge wa cdm wamezomewa na kurushiwa vijembe hadi waliofuatilia bunge wabunge wa cdm morali ikashuka kabisa.nakubali cdm wanaelekea kushindwa kuleta mabadiliko maana hata wingi wa viti vyao bungeni ninawasiwasi kama utaleta mabadiliko sababu kuna misimamo mingi binafsi ya wabunge wa cdm ambayo for sure HUWEZI kuitoa ccm madarakani kwa mpango huo,Hata wananchi wachache walioyatoa hata maisha yao kusimamia hoja za cdm wamechanganyikiwa hakuna muendelezo wa mambo mengi na sasa wananchi wameanza kuamini maneno ya kina Makamba kuwa unaona yaliyowatokea wa Arusha! maana hawaoni matokeo yake.Spika Makinda anakuwa bias waziwazi lakini cdm hawajajipanga kumdhibiti ili awe walau na woga.Kwakweli safari ndefu sana,wananchi walihamasika sana cdm wakashindwa kuitumia hiyo pressure vizuri tena bila kuleta machafuko makubwa.Viongozi wa cdm nawaheshimu sana ila huku mtaani wananchi wameshachanganyikiwa hawajui nini ajenda iliyo mbele na mliyo tayari kuifia.
Uchaguzi utafika hakuna kipya,je cdm watasema pengine wananchi hawawaugi mkono? au watasingizia nini? Tunakosoa ili kujenga upinzani imara na lazima cdm wawe na mipango ya muda mrefu na muda mfupi ili kila kinachotokea wawe na majibu na jinsi ya kufanya,lakini kwa sasa CCM kama wanawazidi ujanja kwenye hoja nyingi na wanabaki wachache wanaofahamu ukweli kuwa hapa cdm wameonewa.Swala la utovu wa nidhamu kwa wabunge ndio kabisaaa inashangaza yanavyoshughulikiwa.niliwahi kusema bora muwe na wabunge wawili kama ilivyokuwa Dr slaa bunge lilopita lakini wapo mle kwa lengo moja tu na sio timu ya watu wenye makundi yao! kuna tofauti gani na CCM yenye wanamtandao na CCM asilia! Solution ya matatizo yetu ni kufumua mifumo yote mibovu na kuweka mifumo mipya dhabiti,lakini kwa mwendo huu CDM itabaki kwenye historia ya waliowahi kutikisa nchi kama NCCR,Mrema n.k lakini matunda ya kutikisa nchi hakuna! NI MTAZAMO TU WAKUU.
 
Kwa hili nadhani mwanzilishi wa thread alikuwa na jazba na bahati mbaya sana lawama ameelekeza kusipotakiwa. Kwa wakati huu ni wakati wa kupeana pole na wakati wa kuzika wafu. Halafu wote tukishazika na wengine kupata na nafuu au kupona kabisa sasa tuulizane nani kafanya nini nani awajibike na kuwajibika kuwe kivipi!!! Kwa muda huu si wakati wa kuanza kuleta chokochoko za siasa maana uhalisia na uzito wa janga lenyewe utapotea kabisa!!! Hata hivyo hasira yako inaonekana wazi lakini zaidi inaonekana wewe ni shabiki wa CCM na si wa uzalendo!!!!
 
Mkubwa mie mbavu sina!!!!.....
Mzee kuna vitu vingine huwa tunavisema kwa ushabiki tu sasa anaposema CDM na CUF wa resign ana maana gani, ni upuuzi wa kitoto ni sawa na kusema CCM i resign, you have to be specific who is to resign not a political party. Labda ana maana ya chama kuvunjwa may be CCM i resign kuwa chama tawala I'm not clear on that.
 
Ingawa kweli wapo wataosema muda wa hukumu bado,lakini hapa tunazungumzia harakati za muda mrefu za cdm na kupata wabunge wengi ilikuwa sehemu ya harakati tu.mfano tukio la Gongo la Mboto hakuna lolote mpaka watu wanaendelea na kazi zao na hakika ndio imekwisha hivyo! wanajeshi wametuma majibu ya kijeshi,watawala je? Au tumekubaliana na yale majibu mepesi? Watu wamekufa tena kwa tukio lililojirudia!
Sote tunaowajibu wa kupigania taifa letu,lakini haiwezekani bila kuwa na viongozi wenye udhubutu wa kujitoa.uongozi na kutetea haki za watu ni kazi ya kujitoa kweli kweli,je wanasiasa wetu wana sura hizo au kulalama tu bila hatua zozote kwenye media.kama mbinu za kisiasa hakuna basi tusubiri muujiza.siku mwanahalisi na magazeti machache yakizalendo "yakishughulikiwa" hivi tumeshaona kitachotokea? Ameshughulikiwa Sitta pamoja na ushawishi aliokuwa nao na sasa wamedhibiti mihimili yote muhimu na watakuwa makini ili cdm msiwe na matukio ya kuwapa sifa(not positively) na huku yaliyotokea nyuma wananchi wameyasahahu,kinatengenezwa kifo cha kawaida(natural death) kwa cdm.
 
Mkuu Quinine tuwasaidie wapendwa wetu wa cdm kwa kuanza kukosoa mapema ili wajirekebishe na kufikia malengo kwa wakati.Alicho chokoza mwenzetu hakiichafui cdm bali kukijenga zaidi hasa wakati huu ambao ni wazi kuna mengi ya kuweka sawa ili kutimiza malengo.Unga mkono pale alipo sahihi na kosoa alipo kosea ili viongozi wa cdm waelewe msimamo wako na mawazo yako.nakuheshimu mkuu maana wewe ni Senior hapa.
 
Kwa hili nadhani mwanzilishi wa thread alikuwa na jazba na bahati mbaya sana lawama ameelekeza kusipotakiwa.
I know this Waberoya is one of the Chadema Haters so I'm not surprised hebu angalia sababu zenyewe ni za kitoto kabisa huyu jamaa ana akili timamu kweli kuona wagonjwa kuna itikadi

Originally Posted by Waberoya

vyama havina tofauti na CCM kwa matendo, wakati JK anaenda kuona wagonjwa, viongozi wa vyama hivi nao wanaenda kuona wagonjwa!
 
Mtuma thread umesema mengi kwa hamasa kubwa, kiasi ambacho umeshindwa kudhibiti hasira zako na kuwaingiza waliomo na wasio kuwemo. Nilitarajia kuona unatoa rai ya kuvitaka vyama vya upinzani kuwacha tafauti zao, viangalie wapi vinatafautiana na wapi vinakubaliana, wachukue hili la pili na kuwa kitu kimoja katika kuushinikiza serikali ya CCM iwajibike. Si mara zote watu wote wanakuwa na mawazo mamoja, lakini wanakuwa na yale wanayokubaliana nayo na kutafautiana nayo. Kwa hiyo ushauri wangu kwa vyama vya upinzani vyote, ni kuungana kwa yale yanayowaunganisha - shida na mateso ya wananchi kutokana na uzembe na madudu ya CCM.
Hili la kuvitaka vyama vya upinzani vijiuzulu, naona umefika mbali mkuu
 
Mkuu huyu jamaa mimi namfahamu toka DARUSO lengo unalolidhania wewe si hilo ana lengo lake, ukitaka kujua lengo lake jaribu kufuatilia thread na posts zake ni mtu wa kuzushia watu, alimsingizia Zitto ana kiwanda cha kokoto, mara yeye ni Lecturer alipobanwa akasema anasoma masters US na mengine mengi ya kizushi, in short haaminiki is not reliable you cannot depend on.
 
Uko sawa kwa kuweka mawazo yako hapa, naogopa kuamini kuwa unataka mabadiliko hapa nchini kwa kuiacha ccm iendelee kutuongoza.Nina uhakika u mwanachama wa ccm, jambo ambalo si kosa lakini hofu yangu inakuja pale unapodhani matatizo haya ni kwa sababu ya cdm na cuf na solution ni kwa viongozi wao kujiuzulu
Tuwe wakweli mfumo tulionao chini ya ccm unatuletea matatizo mengi na mabadiliko ya kweli tutayafanya wananchi kwa kuongozwa na wazuri waliopo na tunawajua
 

Nimekupata mkuu ila kuna vitu ametaja naamini viongozi wetu wanapaswa kuvifanyia kazi,hiyo thread imeandikwa kwa hasira mno ila kama angetulia kuna kitu cha msingi alitaka kuwastua viongozi wa cdm lakini tuhuma alizoandika ndizo zilizonistua hasa kama ni mwanamageuzi wa kweli na bado anakiunga mkono cdm ambacho anafahamu kuna tuhuma alizohainisha.otherwise viongozi wetu watafakari namna ya kushughulikia maafa ya kitaifa isiishie kwenye matamko tu(kama tume zinazochosha za CCM).mfano wanamapinduzi wetu Arusha damu zao zisipotee bure,walichokuwa wanadai kipiganiwe kwa njia zote,hizi kesi zinaweza kuchukua miaka mitatu alafu ikatoka hukumu,rufaa ikaamuliwa after two years! Kweli hapo tunawatia moyo wananchi kutuunga mkono siku nyingine? Unafikiri kuzikwa kwa heshima pekee bila lengo kutimia lita wahamasisha wananchi au kuwatia woga tu.ndio maana juzi wanafunzi wa udsm yalirushwa mabomu machache sana lakini walikimbia mno hasa wakihofu ya Arusha.lakini kama tungesimama kidete baada ya yale mauaji ambayo hata mabalozi walianza kutuunga mkono pengine wananchi(hata wanafunzi juzi) wangejua kwa maandamano ya haki huwezi kupigwa risasi na hata askari wanajua matokeo yake.Lakini ya Arusha imebaki kesi ambayo ingekuwepo hata bila maandamano lakini umewatiaje moyo wananchi ili siku nyingine wakuunge mkono?
 
this post lacks national consciousness.... and at least i have learned that there is a hidden catastrophic movement behind the author .... !
 
Ni rahisi kusema tumeichoka CCM kuliko wapinzani kuachia ngazi, the question here is who has power and authority?
 
Waberoya
Thread yako umetoa ufafanuzi mzuri sana kuna mengi yana ukweli, ingawa utakutana na upinzani mkubwa kutokana na hii Thread yako lakini ukweli vyama vyetu vya upinzanì hivi vikubwa Policy zao kama za CCM tu, vinapita njia ile ile waliopita CCM yani ni vyama Stagger kabisa kama CCM yenyewe, vile vile vimekaa kimaslai zaidi juzi tu tumeona wabunge wote wa upinzani na CCM wamekubaliana kuchukuwa mkopo wa milioni 90 kila mmoja kiongozi gani wa upinzani kaongelea hili swala? bora tupate Katiba mpya tupate wagombea Indepentently wabunge na Rais labda tunaweza kuing'oa CCM, kweli hawa viongozi wanatakiwa wa Resign, submission hawapaswi kuendelea kuwadanganya wananchi watu wanafanya maandamano wanapoteza maisha then viongozi wetu wanakumbatiana na kusifiana na hao viongozi wa CCM ambao wameamlisha mauaji. huwo ndio upinzani imara
 
Hongera wameroya,nitafte tuanzishe chama cha ukweli kwa ajili yakumkomboa mamayetu Tanzania.
 

WABEROYA mimi naungana na WFM kusema ACHA unafiki ACHA udalali ACHA upopo, tunafahamu na tumefuatilia michango yako mingi ndani ya JF. Kama wewe ni mwanaharakati nilitegemea kutumia muda wako kutoa wito kwa wanaharakati wengine kupigania yafuatayo
1. Haki itendeke kwa viongozi wahusika wa wizara (Dr. Mwnyi, Katibu wa Wizara na Mkuu wa Majeshi). Kufanya hivyo ndio kuwajibika katika hili maana yake ni kwamba tatizo hili lisijirudie tena.

2. Bunge lifanyie kazi tamko ta kambi ya upinzani ambalo limetolewa siku ya pili ya tukio.

3. Watanzania kulaani hatua ya makinda spika kupoteza nafasi pekee ya kusikia kilio cha wananchi katika hili-kwa kukataa hoja mahsusi ya Tundu Lissu, watanzania sauti zetu zipo kwa wabunge wetu-Spika aombe radhi kwa kukataa nafasi ile muhimu

4. Utoe wito watanzania kukataa usanii wa CCM katka majanga manake nilijisikia kichefuchefu pale Rais wa Zanzibar -Shen aliposema tukio kama hili halitatokea tena-wamelewa madaraka sana hwa watu, how can shen dare to say that? anawafanya watanzania mbumbumbu?

5. Nilitegemea utoe wito kwa vyombo vya habari vinavyoshiriki kuficha ukweli kama muhimili unaojitegemea.

6. Lakini pia ningetegemea utoke na sauti nzito kwa viongozi wetu waliojitokeza na kuwapongeza wanajeshi badala ya kutatua tatizo huo ni unafiki mkubwa, hapa tunasikia ama ni hujuma ama ni uzembe -utawapongeza vipi wanajeshi kama sio unafiki? wanajeshi gani hao unaowapongeza wakati hujuma au uzembe wao ndio wahusika? hawa viongozi wetu wanapaswa kuwaomba radhi wafiwa.

7. Waberoya ACHA udali ACHA unafiki na ACHA siasa zilizopitwa na wakati. DR SLAA ansema siasa ni science kama zilivyo sayansi nyingine sio propaganda za kizushi, matusi na unafiki kama wako. Kuwa mkweli simamia kweli.
 
Vijiuzuru CDM na KUF?!!! Kwa sababu ipi nzuri au kwa kuwa unalalamika na kunungunika? We are supposed tothink critically.We are saying hueleweki katika maelezo yako.
Hata hivyo wa beroya chama ccm kimefanya nini kuhusu mabomu kulipuka mara tatu ktk utawala wa awamu hii ya nne? Majeshi-JWTZ limesema wao si wanasiasa halikusudii kufanya maamzi ya kisiasa hivyo linaweza kuwajibika tu kwa serikali ilyopo madarakani.Je ni lini ccm iliheshimu michango ya vyama vya upinzani?
Asitafutwe mchawi ,mchawi ccm na mafisadi wake!!!!
 
I dropped history on my form two sababu hakukuwa na facts na nilikuwa napata D ama F!
How can CHADEMA or CUF resign! I might be missing something.

Resign is a verb, with a literal meaning of

  • Voluntarily leave a job or other position.
  • Give up (an office, power, privilege, etc)
Wataalamu wa lugha mtanisaidia, resign hutumika zaidi kwa watu (individuals) na si kwa organisation kama vyama vya kisiasa - CUF, CCM ama CHADEMA these are political parties. Political party is a political organization that typically seeks to influence government policy, usually by nominating their own candidates and trying to seat them in political office. Chama chochote cha siasa agenda yake ya kwanza ni kutwaa dola na kutawala kwa kuweka sera zake.

Kuwa mwanachama wa chama fulani ni kukubaliana na sera na ideology ya chama husika. Huwezi tamka CCM ijiuzulu badala yake utatamka Mwenyekiti, ama katibu wa CCM wajiuzulu sababu 1. 2, 3. ......Ukisema CHADEMA ama CUF wajiuzulu nadhani unakuwa unaweka unafiki kwa makusudi. Labda kama ujumbe wako ungekuwa viongozi wa CHADEMA na CUF wamemeshindwa kutekeleza sera zao na kutetea haki na maslahi ya wanachama wake kwa mbali ningekuelewa.

Mara nyingi nionapo article ndefu sana huwa naisoma na akili nyingine, huenda muandishi anajitahidi kulazimisha mawazo yake bila fact.....

Webs nitolee mfano popote duniani chama cha siasa (CUF, CHADEMA) kilichoamua kujiuzulu.
 

Asante kaka, nimekupata nimekuelewa!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…