IPSO FACTO: CHADEMA AND CUF MUST 'RESIGN'! So as you...if..! TUACHE UNAFIKI

Waberoya

Platinum Member
Aug 3, 2008
15,169
10,785
Ndugu watanzania;

Ujinga huu sio wa kawaida, lazima kuna jambo kubwa nyuma linalopelekea haya yote kutokea... HAIWEZEKANI Tanzania hii, yenye watu hawa , wanaoimba upole, amani na ukarimu wakiishi kwa namna hii wanayoishi leo!

HAIWEZEKANI kuona wakati watu wanakufa na kupotezana, wakihangaika na kupata adha zisizosimulika, kuna watu waliamka asubuhi kama hakuna kilichotokea! makazini kama kawaida, foleni kama kawaida! simulizi za udaku wa g/mboto kila kona, zilizo za ukweli na uongo, msiba kama hauko kwako basi si wako..-huu ni ubinafsi wa kipekee sana

Ubinafsi huu ndio uliopelekea watu kuwa mafisadi, kwa sababu hawana uzalendo, kujiangalia wao na familia zao, kwa kifupi taifa la Tanzania halipo wala haliishi kwa vitendo bali kwa furaha za muda na unafiki uliokithiri!

Wakati wanamuziki wakiimba na kuomboleza kwa sababu ni waimbaji wanasiasa wengi wamekuwa wakifanya yaliyo ada! kuzika watu baada ya uzembe!

Sijaona wala sifikirii kuwa kuna chama cha upinzani nchi hii chenye kubadili welekeo wa sasa wa maisha, kwenye mpira ukikosea kidogo tu basi adui anatosha kabisa kufunga goli, vyama vya siasa vikiwamo vile vinavyojiita mbadala au vikubwa havina tofauti na CCM kwa matendo, wakati JK anaenda kuona wagonjwa, viongozi wa vyama hivi nao wanaenda kuona wagonjwa! wakati JK anasema anaunda tume, vyama hivi vya siasa vinasema tume iundwe! wakati wananchi wanasema viongozi wajiuzulu, vyama vya siasa vinasema viongozi wajiuzulu!!!

kwa haraka haraka hauoni tofauti ya CCM na opposition, hauoni tofauti ya wananchi na opposition, to cut it short so-called opposition parties they dont have any unique solutions than CCM and Citizen's!

Samahani chama gani cha siasa kilifuatilia kuwa waathirika wa Mbagala hawajalipwa mpaka leo? nani alifuatilia ile tume ilileta au ilitoa jibu gani?

Kwa nini majanga yanavyotokea serikali,chama tawala, wapinzani woote wanaonekana kitu kimoja tu? sijaona tofauti bado yakuwa chadema ni mbadala , sijaona tofauti ya kuwa CDM CUF au NCCR...name it ni wapinzani, woote hawa ni wezi na mafisadi tu!

Ni kitu gani kinazuia hivi vyama kuandamana kwa amani kuiondoa CCM madarakani? ni vitu gani vinazuia hivi vyama kukusanyika mnazi mmoja na vitambaa vyeupe vikiashiria hatuna ugomvi kuishinikiza CCM iondoke madarakani? ujinga huu umefikia wakati ili shibe ziendelee kwa makusudi zimeingizwa hoja za kutoaminiana! ili CCM iendelee! na wao waendelee! na kuwapa wananchi wajinga matumaini yasiyikuwepo yaendelee!

Tumaini la mtanzania leo ni nakala za mwanahalisi,raia mwema, kulikoni, blogs,FB, JF n.k? mpaka watu wanaandaa online petition eti Mwinyi ajiuzulu..what a joke!, HAYA amesema hatoki madarakani so what next??!!Tumaini la mtanzania liko wapi? is this not a seduction? hivi vyama vimeaminisha watanzania kuwa vinaweza, vikasema vinaweza, vikapigiwa kura na hawa watu wa Gongo la Mboto! je malipo yao ni kuona wananyanyaswa namna hii, nani wa kuwasaidia at least justice must be done?

Chama gani cha siasa na lini kilishauri kuwa hizi ghala za silaha zisikae karibu na watu? Vilifika mbali kiasi gani kuhakikisha hili halitokei? zili-force haya mAswala kiasi gani? au upinzani ni kutoyaangalia haya?? nauliza tena tumaini la watanzania kuunda wizara vivuli na kamati za bunge ni nini? wakati tunasema wakina Mwinyi wajiuzulu hawa mawaziri vivuli wa upinzani wao hawatakiwi kujiuzulu?

Ukiacha upinzani ambao umeoza na hamna tumaini, hata kama mtatoa machozi ya damu kumsifia Slaa au Hamad au sijui nani, hakuna tumaini huku! hakuna maisha huku! JE hizi asasi za serikali zinazokula fedha za misaada zinafanya nini? wanaharakati wa haki za binadamu walifuatilia kiasi gani issue ya mbagala? ilifikia wapi na walifanya nini??

Kwa kifupi uzembe wa serikali ni superficial tu, kuna uzembe mkubwa karibu kila institution we are now reaping! mabomu yameonekana je ni mangapi yanayotokea nchi hii YAFANANAYO NA HAYA? ambayo hayaonekani sasa na athari zake zitaonekana vizazi vijavyo?

Narudia tena for the sake of next generations please forget about these opposition parties we better wipe them away, because we dont have one! kuvikataa hivi vyama ni mwanzo wa kuvikaribisha vyama vilivyo 'CRAZY' and 'ADDICTED' to redeem Tanzanian from CCM oppression!

Najua wengi mnaweza kuwa washabiki sijakurupuka! pengine sijui kazi ya wapinzani naona we are lacking something !

Ujinga ndio unatusumbua, ubinafsi unatutawala, roho mbaya inatuwinda, kutowaza vizazi vijavyo we are foolishly blind! NO ONE IS SAFE IN TANZANIA! NO ONE! haki ile ya G/Mboto haikuchagua maskini wala tajiri!

Narudi kwa chadema na wenzio, jiuzuruni kuwa chama cha siasa, mkianza nyie akina Mwinyi watafuata! maana hamjui siasa, hamjui wajibu wenu, kazi kukalia ruzuku! mkisema kwa sababu haiko madarakani basi hawakutakiwa kwenda kuona wagonjwa, hawakutakiwa kusema akina Mwinyi wajiuzulu! kama inaweza kusema haya kwa nguvu waliyonayo then they have every right to followup everything in this country!

Nasema kwa uchungu sana na hasa juu ya CDM ambayo imekuwa ikiwadanganya raia kuwa ni wasafi... tunaujua ukweli kuanzia mtei, tunajua urafiki wa wa karibu sana wa Kikwete na rafiki yake Lowassa kwa akina Mbowe na Kibanda!

Nyie wanachadema na wengine mpaka mtakapofikia hatua ya kuwakaanga viongozi wenu ILI WAFANYE KILE MNACHOKITAKA basi hakuna ukombozi nchi hii, CDM ya sasa imeishachakachuliwa!

Ujinga uleule wa kukubali kila kitu , ndicho kilichopelekea Slaa akubali kushindwa, huu ni ujinga tu wala hakuna maelezo mengine fasaha, ujinga huo huo ndio unapelekea wananchi na vyama vyao kutojali lililotokea Gongo la Mboto na kuendelea na shughuli zao!

Upinzani umeshindwa kuhoji mpaka makampuni ya simu kwa nini walizima mitambo zile nyakati ambapo msaada wao ulihitajika sana!

Ni lini tunaowalipa bungeni, wanakula ruzuku zetu kutokana na kodi zetu watakuwa tayari kufanya au kuisukuma serikali katika kila kitu? hata kama hawapo madarakani, mbona ruzuku hazisemwi kuwa zisubiri wachukue madaraka? idadi yenyewe ya wapinzani ni ndogo still we are thinking opposition will RESCUE us? huu nao sio ujinga??

I repeat CDM CUF.. and all other opposition must resign! should I continue to describe this? hata wewe mwananchi kama hukufanya lolote kwenye hili swala basi jiuzulu uraia wa Tanzania! acheni unafiki aidha tuingie barabarani au tukae kimya kabisa! we have only two options! Wakati Slaa anasema ‘tunaonyesha mshikamano' Hamad anasema anaridhishwa na jitihada za JWTZ na eti anasubiri majibu ya tume.. ili hali ya mbagala haijajulikana mpaka leo! mlifikia mbali kiasi gani kufuatilia issue ya mbagala? hamuoni na nyie ni magoal-keeper tu wa kusubiri catastrophes? mnaishauri serikali? tuelezeni issue ya mbagala mlifuatilia kwa umbali kiasi gani??

CDM and CUF must resign kwa sababu haikuzuia hili swala wala kufuatilia toka maafa ya kwanza ya mbagala nao wamekuwa wasubiriaji tu na imeshindwa kuwapeleka watu barabarani ili CCM ijiuzulu! You have willfully loosed opportunity to lead us into our Tahrir square! you are nothing you are weakers! Au nyie kusaidia wananchi ni mkiwa viongozi tu? Tauache unafiki kuwachekeachekea hawa wapinzani ili wali ndio wanatakiwa kuongoza jahazi nyakati hizi ni siyo ujinga ni zaidi ya ujinga! Mnawapa misifa sijui nani kawaroga, ukiamka CDM hivi Slaa vile sifa tu! Nothing has been done at a all at all at all! Kama tuna value output then we have to evaluate output of this vyama! Otherwise aibu tupu na ushabiki usio na msingi!

Sorry vyama vingine sijaviongelea maana vinawakilishwa na hivi vinavyojiita vikubwa!

Nendeni kwa msajili wa vyama vya siasa mkaombe vyama vyenu vifutwe ili muanze upya, hakuna opposition Tanzania, kuna false hope na ujanja mwingi wa kutaka ruzuku zetu na kujifanya mna uchuuuungu kumbe kutaka maisha yenu yaendelee, you better find another JOB!

Kwa mnaodhani ninavionea vyama ebu tafuteni kwenye literature functions of opposition! You will be surprised their role and strength is big!

Wenu katika harakati za kulikomboa taifa hili from CCM.

Waberoya
 
Maneno yako ni mazuri sana aisee na yana kila chembe ya hamasa ya uzalendo. Hata hivyo naamini yako misplaced. Wanaotakiwa kuwajibika kwanza ni chama tawala in this case CCM. Wapinzani wanaweza kupiga kelele, wanaweza kusema na kusema wanaweza tatizo ni kuwa wanaotakiwa kuwajibika ni CCM. Mimi nafikiria ungetoa wito kwa wabunge wa CCM ambao kwa wingi wao ndio wana uwezo wa kubadilisha mwelekeo wa serikali ya wajiuzulu. Yaani wapinzani wajiuzulu halafu ndio chama tawala kijiuzulu? au wapinzani wajiuzulu halafu chama tawala kitawale pasipo upinzani?

Wrong number, Kikwete na serikali yake wanawajibika na wanapaswa kuwajibika kwa madudu yote yanayotokea chini yao. Vyama vya upinzani vitawajibika kwa kiwango kile tu ambacho kimo ndani ya uwezo wao kusababisha matokeo.

Licha ya kusema hayo nakubaliana na wewe kwa asilimia mia moja kuwa vyama vya upinzania na hasa Chadema vingeweza kuonesha kuwa kweli viko katika kuipa pressure serikali. Tatizo ni kama ulivyosema "hawajui siasa" na hiyo ni conclusion ambayo nakubaliana nayo kwani wangekuwa wanajua siasa kweli hakuna chama kilichopendelewa kwa matukio ya kisiasa kama Chadema. Na wameshinwa kuyatumia matukio hayo vizuri.
 
Waberoya

Kuna madai yako mengine ni sahihi na mengine hayako sahihi.

Why condemn CHADEMA on Mbagala/GMboto sagas? Try to be specific.Hapa wa KULAUMIWA to be fair ni CCM and CUF.
CCM na CUF kwasababu wao ndiyo WANAOENDESHA SERIKALI KWA SASA BARA NA VISIWANI. Halafu siyo sawa kusema vyama vya siasa ndiyo vijiuzulu,wanaopaswa kujiuzulu ni viongozi wa vyama husika WALIOKO KWENYE MADARAKA KWA SASA NA HASA WALE AMBAO MAENEO YAO NDIYO YAMESABABISHA MADHILA HAYA YA MABOMU KWA WATANZANAI.

Watu wanaotakiwa kujiuzulu ni Waziri wa Ulinzi- Dr. Hussein Mwinyi,Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi-Davis Mwamnyage na Waziri wa Mambo ya Ndani-Vuai Nahodha. Siyo sawa kusema serikali yote au Chama chote kijiuzulu.

Kama unataka Serikali yote na Chama chake INATAKIWA ITUMIKE PEOPLES POWER kama huko kwa wenzetu Uarabuni wanavyofanya kwa sasa. Sijui ni kitu gani kinatufanya Watanzania TUNAKUWA NA KIGUGUMIZI!
 
Maneno yako ni mazuri sana aisee na yana kila chembe ya hamasa ya uzalendo. Hata hivyo naamini yako misplaced. Wanaotakiwa kuwajibika kwanza ni chama tawala in this case CCM. Wapinzani wanaweza kupiga kelele, wanaweza kusema na kusema wanaweza tatizo ni kuwa wanaotakiwa kuwajibika ni CCM. Mimi nafikiria ungetoa wito kwa wabunge wa CCM ambao kwa wingi wao ndio wana uwezo wa kubadilisha mwelekeo wa serikali ya wajiuzulu. Yaani wapinzani wajiuzulu halafu ndio chama tawala kijiuzulu? au wapinzani wajiuzulu halafu chama tawala kitawale pasipo upinzani?

Wrong number, Kikwete na serikali yake wanawajibika na wanapaswa kuwajibika kwa madudu yote yanayotokea chini yao. Vyama vya upinzani vitawajibika kwa kiwango kile tu ambacho kimo ndani ya uwezo wao kusababisha matokeo.

Licha ya kusema hayo nakubaliana na wewe kwa asilimia mia moja kuwa vyama vya upinzania na hasa Chadema vingeweza kuonesha kuwa kweli viko katika kuipa pressure serikali. Tatizo ni kama ulivyosema "hawajui siasa" na hiyo ni conclusion ambayo nakubaliana nayo kwani wangekuwa wanajua siasa kweli hakuna chama kilichopendelewa kwa matukio ya kisiasa kama Chadema. Na wameshinwa kuyatumia matukio hayo vizuri.
hapo red;you have spoken my mind, mleta hii sredi alitaka iwe vipi wakati maswala ya jeshi hayazungumzwi kwa uwazi.Kama Shimbo alishesema halitatokwa tena la mbagala how could oppositon demand a much clear statment kwa wakati ule while mabomu ni ishu za kijeshi ambazo ONLY JESHI WANARUHUSIWA KUZISEMEA?If jeshi leo likisema mabomu yamelipuka kwa sababu A,B and C nani mwenye ruhusa ya kucross check hizo sababu wakati haturuhusiwi kujadili maswala yao?
 
Hoja ni nzuri na ina point zake.

Ni kweli inabidi kuwe na hoja tofauti,kati ya wananchi wazalendo na vyama vya upinzani! Mfano baada ya mabomu ya goms wananchi wakasema mwinyi ajiuzulu. Basi ingeishia kwa wanachi kusema, ila ilipochukuliwa hoja hii na cdm kuwa mwinyi ajiuzulu basi ikageuzwa hoja ya kisiasa ambapo serikali yetu ya ccm haikubaligi kushindwa! Wakapindisha kabisa uwajibikaji wa serikali.

Kweli,chama gani cha upinzani kilifuatilia tume kuhusu mabomu ya mbagala? Na walifikia wapi au walikwamia wapi? Ina maana hivi vyama havina mgawanyo wa majukumu?

Hii imekuja kunikumbusha jinsi cdm wanavomlinda mtu kama zitto wakijua wazi anatumia na kina ra. Je kwa uwajibikaji wao huu kama wa ccm , wa kutembea na mavi mfukoni,tutegemee mabadiliko kweli?

Jamani,wananchi wazalendo tukae kujipanga kwani upepo wa kisiasa pekee hautufikishi pahala! Tuchukue nafasi yetu kupaza sauti zetu wenyewe zisikike
 
Nimekumbuka a level aise,hv ni kitabu cha ngugi au cha chinua? "Beautiful ones are not yet born" da same in tz kikwete,slaa,ra, lipumba etc wote wachumia tumbo tu wanatofautiana level of greediness,sijaona wa kuniondolea umasikini wangu ktk wanasiasa wote wa tz wote WEZI tu
 
Chama gani cha siasa na lini kilishauri kuwa hizi ghala za silaha zisikae karibu na watu? Vilifika mbali kiasi gani kuhakikisha hili halitokei?
Mkuu, umesahau kuwa hata CCM ni chama cha siasa? Au unapozungumzia chama cha siasa unamaanisha CHADEMA na CUF?
 
Upinzani umeshindwa kuhoji mpaka makampuni ya simu kwa nini walizima mitambo zile nyakati ambapo msaada wao ulihitajika sana...ila hii si kweli mkuu,ilikuwa n congestion mkuu! Kwani utilization ya hii mitambo stimes ikivuka 75% huwa inacease ama kuhang ,ni traffic ambayo haikutegemewa so networks hazikuwa dimensioned kuibeba!
 
Mkuu una hoja nzuri na nzito,kama Tanzania ingekuwa nchi isiyo na madkteta,ikasikiliza hoja,mkuu maneno yako yangeumba! Tatzo hapa ni kutosikiliza kilio chetu. Mkuu,ikumbukwe pia upinzani unasaidia ila hapa tulaumu udkteta wa Taifa. Hivi,matamko ya cdm unayapata?ni mazito zaidi ya waraka wako,lakni nani anasikiliza?maandamano mpaka mauaji ya waandamanaji unayaonaje? CUF mara ngapi wanaandamana lakni madkteta wanaona kama CUF wanafanya ngonjera? Ngeleja alitaja mafisadi wamiliki dowans,rostam akasema hausiki,leo mwanajeshi wa Oman,AL ALDAWI anakuja na kusema Rostam anahusika,alikabidhiwa Dowans tangu 2006. Mkuu hapa unapata taswira gani? Mi naishiwa hamu na taifa ili.
 
Ndugu watanzania;

Ujinga huu sio wa kawaida, lazima kuna jambo kubwa nyuma linalopelekea haya yote kutokea... HAIWEZEKANI Tanzania hii, yenye watu hawa , wanaoimba upole, amani na ukarimu wakiishi kwa namna hii wanayoishi leo!

HAIWEZEKANI kuona wakati watu wanakufa na kupotezana, wakihangaika na kupata adha zisizosimulika, kuna watu waliamka asubuhi kama hakuna kilichotokea! makazini kama kawaida, foleni kama kawaida! simulizi za udaku wa g/mboto kila kona, zilizo za ukweli na uongo, msiba kama hauko kwako basi si wako..-huu ni ubinafsi wa kipekee sana

Ubinafsi huu ndio uliopelekea watu kuwa mafisadi, kwa sababu hawana uzalendo, kujiangalia wao na familia zao, kwa kifupi taifa la Tanzania halipo wala haliishi kwa vitendo bali kwa furaha za muda na unafiki uliokithiri!

Wakati wanamuziki wakiimba na kuomboleza kwa sababu ni waimbaji wanasiasa wengi wamekuwa wakifanya yaliyo ada! kuzika watu baada ya uzembe!

Sijaona wala sifikirii kuwa kuna chama cha upinzani nchi hii chenye kubadili welekeo wa sasa wa maisha, kwenye mpira ukikosea kidogo tu basi adui anatosha kabisa kufunga goli, vyama vya siasa vikiwamo vile vinavyojiita mbadala au vikubwa havina tofauti na CCM kwa matendo, wakati JK anaenda kuona wagonjwa, viongozi wa vyama hivi nao wanaenda kuona wagonjwa! wakati JK anasema anaunda tume, vyama hivi vya siasa vinasema tume iundwe! wakati wananchi wanasema viongozi wajiuzulu, vyama vya siasa vinasema viongozi wajiuzulu!!!

kwa haraka haraka hauoni tofauti ya CCM na opposition, hauoni tofauti ya wananchi na opposition, to cut it short so-called opposition parties they dont have any unique solutions than CCM and Citizen's!

Samahani chama gani cha siasa kilifuatilia kuwa waathirika wa Mbagala hawajalipwa mpaka leo? nani alifuatilia ile tume ilileta au ilitoa jibu gani?

Kwa nini majanga yanavyotokea serikali,chama tawala, wapinzani woote wanaonekana kitu kimoja tu? sijaona tofauti bado yakuwa chadema ni mbadala , sijaona tofauti ya kuwa CDM CUF au NCCR...name it ni wapinzani, woote hawa ni wezi na mafisadi tu!

Ni kitu gani kinazuia hivi vyama kuandamana kwa amani kuiondoa CCM madarakani? ni vitu gani vinazuia hivi vyama kukusanyika mnazi mmoja na vitambaa vyeupe vikiashiria hatuna ugomvi kuishinikiza CCM iondoke madarakani? ujinga huu umefikia wakati ili shibe ziendelee kwa makusudi zimeingizwa hoja za kutoaminiana! ili CCM iendelee! na wao waendelee! na kuwapa wananchi wajinga matumaini yasiyikuwepo yaendelee!

Tumaini la mtanzania leo ni nakala za mwanahalisi,raia mwema, kulikoni, blogs,FB, JF n.k? mpaka watu wanaandaa online petition eti Mwinyi ajiuzulu..what a joke!, HAYA amesema hatoki madarakani so what next??!!Tumaini la mtanzania liko wapi? is this not a seduction? hivi vyama vimeaminisha watanzania kuwa vinaweza, vikasema vinaweza, vikapigiwa kura na hawa watu wa Gongo la Mboto! je malipo yao ni kuona wananyanyaswa namna hii, nani wa kuwasaidia at least justice must be done?

Chama gani cha siasa na lini kilishauri kuwa hizi ghala za silaha zisikae karibu na watu? Vilifika mbali kiasi gani kuhakikisha hili halitokei? zili-force haya mAswala kiasi gani? au upinzani ni kutoyaangalia haya?? nauliza tena tumaini la watanzania kuunda wizara vivuli na kamati za bunge ni nini? wakati tunasema wakina Mwinyi wajiuzulu hawa mawaziri vivuli wa upinzani wao hawatakiwi kujiuzulu?

Ukiacha upinzani ambao umeoza na hamna tumaini, hata kama mtatoa machozi ya damu kumsifia Slaa au Hamad au sijui nani, hakuna tumaini huku! hakuna maisha huku! JE hizi asasi za serikali zinazokula fedha za misaada zinafanya nini? wanaharakati wa haki za binadamu walifuatilia kiasi gani issue ya mbagala? ilifikia wapi na walifanya nini??

Kwa kifupi uzembe wa serikali ni superficial tu, kuna uzembe mkubwa karibu kila institution we are now reaping! mabomu yameonekana je ni mangapi yanayotokea nchi hii YAFANANAYO NA HAYA? ambayo hayaonekani sasa na athari zake zitaonekana vizazi vijavyo?

Narudia tena for the sake of next generations please forget about these opposition parties we better wipe them away, because we dont have one! kuvikataa hivi vyama ni mwanzo wa kuvikaribisha vyama vilivyo 'CRAZY' and 'ADDICTED' to redeem Tanzanian from CCM oppression!

Najua wengi mnaweza kuwa washabiki sijakurupuka! pengine sijui kazi ya wapinzani naona we are lacking something !

Ujinga ndio unatusumbua, ubinafsi unatutawala, roho mbaya inatuwinda, kutowaza vizazi vijavyo we are foolishly blind! NO ONE IS SAFE IN TANZANIA! NO ONE! haki ile ya G/Mboto haikuchagua maskini wala tajiri!

Narudi kwa chadema na wenzio, jiuzuruni kuwa chama cha siasa, mkianza nyie akina Mwinyi watafuata! maana hamjui siasa, hamjui wajibu wenu, kazi kukalia ruzuku! mkisema kwa sababu haiko madarakani basi hawakutakiwa kwenda kuona wagonjwa, hawakutakiwa kusema akina Mwinyi wajiuzulu! kama inaweza kusema haya kwa nguvu waliyonayo then they have every right to followup everything in this country!

Nasema kwa uchungu sana na hasa juu ya CDM ambayo imekuwa ikiwadanganya raia kuwa ni wasafi... tunaujua ukweli kuanzia mtei, tunajua urafiki wa wa karibu sana wa Kikwete na rafiki yake Lowassa kwa akina Mbowe na Kibanda!

Nyie wanachadema na wengine mpaka mtakapofikia hatua ya kuwakaanga viongozi wenu ILI WAFANYE KILE MNACHOKITAKA basi hakuna ukombozi nchi hii, CDM ya sasa imeishachakachuliwa!

Ujinga uleule wa kukubali kila kitu , ndicho kilichopelekea Slaa akubali kushindwa, huu ni ujinga tu wala hakuna maelezo mengine fasaha, ujinga huo huo ndio unapelekea wananchi na vyama vyao kutojali lililotokea Gongo la Mboto na kuendelea na shughuli zao!

Upinzani umeshindwa kuhoji mpaka makampuni ya simu kwa nini walizima mitambo zile nyakati ambapo msaada wao ulihitajika sana!

Ni lini tunaowalipa bungeni, wanakula ruzuku zetu kutokana na kodi zetu watakuwa tayari kufanya au kuisukuma serikali katika kila kitu? hata kama hawapo madarakani, mbona ruzuku hazisemwi kuwa zisubiri wachukue madaraka? idadi yenyewe ya wapinzani ni ndogo still we are thinking opposition will RESCUE us? huu nao sio ujinga??

I repeat CDM CUF.. and all other opposition must resign! should I continue to describe this? hata wewe mwananchi kama hukufanya lolote kwenye hili swala basi jiuzulu uraia wa Tanzania! acheni unafiki aidha tuingie barabarani au tukae kimya kabisa! we have only two options! Wakati Slaa anasema ‘tunaonyesha mshikamano' Hamad anasema anaridhishwa na jitihada za JWTZ na eti anasubiri majibu ya tume.. ili hali ya mbagala haijajulikana mpaka leo! mlifikia mbali kiasi gani kufuatilia issue ya mbagala? hamuoni na nyie ni magoal-keeper tu wa kusubiri catastrophes? mnaishauri serikali? tuelezeni issue ya mbagala mlifuatilia kwa umbali kiasi gani??

CDM and CUF must resign kwa sababu haikuzuia hili swala wala kufuatilia toka maafa ya kwanza ya mbagala nao wamekuwa wasubiriaji tu na imeshindwa kuwapeleka watu barabarani ili CCM ijiuzulu! You have willfully loosed opportunity to lead us into our Tahrir square! you are nothing you are weakers! Au nyie kusaidia wananchi ni mkiwa viongozi tu? Tauache unafiki kuwachekeachekea hawa wapinzani ili wali ndio wanatakiwa kuongoza jahazi nyakati hizi ni siyo ujinga ni zaidi ya ujinga! Mnawapa misifa sijui nani kawaroga, ukiamka CDM hivi Slaa vile sifa tu! Nothing has been done at a all at all at all! Kama tuna value output then we have to evaluate output of this vyama! Otherwise aibu tupu na ushabiki usio na msingi!

Sorry vyama vingine sijaviongelea maana vinawakilishwa na hivi vinavyojiita vikubwa!

Nendeni kwa msajili wa vyama vya siasa mkaombe vyama vyenu vifutwe ili muanze upya, hakuna opposition Tanzania, kuna false hope na ujanja mwingi wa kutaka ruzuku zetu na kujifanya mna uchuuuungu kumbe kutaka maisha yenu yaendelee, you better find another JOB!

Kwa mnaodhani ninavionea vyama ebu tafuteni kwenye literature functions of opposition! You will be surprised their role and strength is big!

Wenu katika harakati za kulikomboa taifa hili from CCM.

Waberoya

Mkuu Pole sana na yaliyokukuta leo asubuhi.
Hapo juu (RED YA KWANZA) umeonyesha ulikurupuka kutoka usingizin. Tuliza akili mkuu, tafakari ndipo ujue ulete nini kwa wadau
 
Nimekumbuka a level aise,hv ni kitabu cha ngugi au cha chinua? "Beautiful ones are not yet born" da same in tz kikwete,slaa,ra, lipumba etc wote wachumia tumbo tu wanatofautiana level of greediness,sijaona wa kuniondolea umasikini wangu ktk wanasiasa wote wa tz wote WEZI tu

Hujakumbuka kitu hapo Mkuu bado umesahau, The Beautyful Ones Are Not Yet Born hakikuandikwa na Ngugi wala Chinua Achebe,endelea kukumbuka nani mwandishi
 
Waberoya hapa hujafikia vizuri kabisa, badala ya CCM na Serikali wawajibike, unatakata CDM na CUF wawajibike ili iweje? na kwa sababu ipi?
 
Waberoya.
Thank You for your concern. Hakika unaipenda nchi yetu na uko kwenye majonzi makubwa kwa hali ilivyo sasa.Kimsingi nakubalina na hoja zako lakini kuna mambo kadhaa ambayo kwa mtazamo wangu naona hayajakaa sawa.

1.Unasema vyama vya upinzani havijafanya tofauti na CCM hasa kwa mambo waliyoyafanya kwa mfano na wao kwenda kuona wagonjwa.Hili lisingeweza kuepukika kwani utamaduni wa kawaida kabisa wa Mtanzania,kupewa pole pindi anapopatwa na matatizo.Hatuwezi kubadili tamaduni zetu kwa sababu zozote zile ziwe za kisiasa ama la.Imependeza vionglozi wa vyama kwenda kuwaona wagonjwa.
2.Umependekeza kwamba ingekuwa ni vyema vyama hivi vikafanya maandamano ya amani,hivi unafanyaje maandamano wakati wahanga wako mahospitalini,msiba inaendelea,ni utamaduni wa wapi?ni lazima tulie pamoja halafu mengine yatafuatwa.
3.Siku zote vyama vya upinzani huwa na sauti moja na wananchi hivyo kuomba tume ya uchunguzi ni sahihi kabisa,wananchi wana forum ya kupeleka vilio vyao?si kupitia taasisi mbalimbali?wao wakilia,vyama vya siasa vikilia,asasi za kiraia zikilia huoni sauti zitasikilizwa kwa haraka?
4.Kuhusu Mawaziri Vivuli kujiuzulu Mwanakijiji amekujibu vizuri sana.
5.Si kweli kwamba the beautifull one are not yet born,wako wengi tu ila hawaoni kwa kuwa hawafanyi kama wewe unavyotaka.Kama siasa ingekuwa ni kuzungumza tu,mengi yangewezekana lakini kwa kuwa ni vitendo zaidi na kwa kuwa vitendo hivi huwa ni ngumu kuvifikia kwa wakati muafaka kwa kuwa kuna vikwazo mbalimbali bsi ni ngumu sana kuapreciate kazi inayofanywa.Ningekushauri uingie ndani uone utamu.
 
Maneno yako ni mazuri sana aisee na yana kila chembe ya hamasa ya uzalendo. Hata hivyo naamini yako misplaced. Wanaotakiwa kuwajibika kwanza ni chama tawala in this case CCM. Wapinzani wanaweza kupiga kelele, wanaweza kusema na kusema wanaweza tatizo ni kuwa wanaotakiwa kuwajibika ni CCM. Mimi nafikiria ungetoa wito kwa wabunge wa CCM ambao kwa wingi wao ndio wana uwezo wa kubadilisha mwelekeo wa serikali ya wajiuzulu. Yaani wapinzani wajiuzulu halafu ndio chama tawala kijiuzulu? au wapinzani wajiuzulu halafu chama tawala kitawale pasipo upinzani?

Wrong number, Kikwete na serikali yake wanawajibika na wanapaswa kuwajibika kwa madudu yote yanayotokea chini yao. Vyama vya upinzani vitawajibika kwa kiwango kile tu ambacho kimo ndani ya uwezo wao kusababisha matokeo.

Licha ya kusema hayo nakubaliana na wewe kwa asilimia mia moja kuwa vyama vya upinzania na hasa Chadema vingeweza kuonesha kuwa kweli viko katika kuipa pressure serikali. Tatizo ni kama ulivyosema "hawajui siasa" na hiyo ni conclusion ambayo nakubaliana nayo kwani wangekuwa wanajua siasa kweli hakuna chama kilichopendelewa kwa matukio ya kisiasa kama Chadema. Na wameshinwa kuyatumia matukio hayo vizuri.

ni kweli kabisa umegusa sehemu muhimu, cdm inatakiwa itumie nafasi kwa kuhoji na kufatilia maswala ya msingi mpaka kieleweke. Hata kama ccm watagoma kuwakubalia cdm basi effort zao zionekane kama ilivyokuwa arusha when you talk the talk you must walk the walk.
 
Ndugu watanzania;

Wenu katika harakati za kulikomboa taifa hili from CCM.[/B]

Waberoya

Hata kwa kutumia akili ya kawaida sana bila kushirikisha malitrecha yoyote ulitakiwa kujua kwamba haufanyi harakati yoyote ya kuikomboa nchi hii.
Kama wewe unajiona kwamba uko kwenye harakati za ukombozi wa nchi hii, kwa staili hii ya kutaka vyama vya upinzani ndivyo vijiuzulku ili ccm ibaki peke yake, basi wewe ni mwanaharakati wa kutaka ccm iendelee kututawala milele daima.

Huu muda ulioutumia kuvishutumu vyama vya upinzani ulitakiwa kuutumia kuwashutumu ccm kwakuwa wao ndio wanaounda serikali.
Serikali ya ccm ndiyo imewateua majenerali wa jeshi ambao wameshindwa kutumia makombora kuilinda nchi na wananchi wake badala yake "wameyaachia" makombora yawamalize wananchi wake.

Kama kweli unataka uaminike kwamba wewe ni mwanaharakati wa kuikomboa nchi toka mikononi mwa ccm basi tumia weledi wako kuhamasisha ama kushiriki kwa vitendo kuing'oa ccm n kwa jinsi hiyo unaweza pia kusiadia mbinu ulizonazo kuviimarisha vyama vya upinzani ili viweze kuing'oa ccm. Lakini ukiendeleza ngonjera zako za kila siku hasa hasa ukiishambulia chadema, na hata hapa najua umejaribu kujitahidi kukwepa kuwataja moja kwa moja ndio maana umewaongezea cuf, na ukisoma maandiko yako unaonekana hasira zako ni kwa chadema na si opposition yote kama unavyokuja kumalizia shutuma zako.
ccm ndo io madarakani kwahiyo ndo inapaswa kuwajibika, hussei mwinyi ni waziri wa ccm ndiye anapaswa kuwajibika, mwamunyange ni mteule wa ccm ndiye anapaswa kuwajibika. Kuvishutumu vyama vya upinzani katika hili ni dalili za kuishiwa hoja na sasa unaleta viroja.
 
"Sijaona wala sifikirii kuwa kuna chama cha upinzani nchi hii chenye kubadili welekeo wa sasa wa maisha, kwenye mpira ukikosea kidogo tu basi adui anatosha kabisa kufunga goli, vyama vya siasa vikiwamo vile vinavyojiita mbadala au vikubwa havina tofauti na CCM kwa matendo, wakati JK anaenda kuona wagonjwa, viongozi wa vyama hivi nao wanaenda kuona wagonjwa! wakati JK anasema anaunda tume, vyama hivi vya siasa vinasema tume iundwe! wakati wananchi wanasema viongozi wajiuzulu, vyama vya siasa vinasema viongozi wajiuzulu!!!"

Webs, sijui profession yako wala level yako ya elimu ila naweza kukusoma kwa baadhi ya post zako humu JF kwa sababu we' ni mchangiaji mzuri. Nahisi ume-obey archemedes principle kwa hiki ulichokieleza hapo na inawezekana kikawa kime-displace sehemu kubwa ya akili na uelewa wako. Nasema hivi kwa sababu zifuatazo:

1. Inaonekana wewe ni mwepesi wa kuchoka, kukata tamaa, kukurupuka na pengine kutaka mambo kwa pupa. Hapa namaanisha: Baada tu ya taarifa ya milipuko kutinga bungeni, Mh. Mbunge mmoja wa CDM aliomba suala hilo lipewe nafasi na kujadiliwa bungeni kama hoja ya dharula. Spika akakataa hilo ombi, na pale kulikuwa na uwanja mpana wa kuhoji usiri wa hizi tume zinazoundwa na pengine ingetakiwa taarifa hizi ziletwe bungeni ili kila mwananchi ajue kama kulikuwa na uzembe na nani awajibike. Hiyo ndo ilikuwa nafasi ya mbunge wa CDM, ungekuwa wewe ungemtukana Mh. Spika..?

2. Wakati mwingine unakuwa sio mkweli. Nimewahi kusoma post yako humu JF ulipokuwa ukijadili kuhusu ushirikiano wa vyama vya upinzani. Ulisema CDM wamewahi kushirikiana na CCM kuiongoza manispaa ya Kigoma, kitu ambacho hakikuwa kweli, kwa sababu waliongoza kwa kupokezana na si kushirikiana. Hivyo, napata wasiwasi na hiki ulichokiweka hapa leo.

Mi si mwanasiasa wala si mwanaCDM ila ni mfuatiliaji wa siasa za 'haki na wajibu' kwa sababu ndizo zinazofanya amani, umoja, mshikamano na dira ya uchumi wa nchi.

Mwisho neno 'RESIGN' litapoteza uzito wake linatumika ovyo hata kwa ambaye si mhusika, kuna wakati utafika mke wako akipika ugali mbichi utamwambia a-resign.
 
Mkubwa mie mbavu sina!!!!.....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom