Ipo siku waliomwacha Mbowe wataanza kumrudia na kumkuta shujaa zaidi

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Nimefuatilia wabunge wote wa vyama vya upinzani ikiwemo CHADEMA waliowasaliti wananchi na kujiunga CCM wakipoteza umaarufu wao kabisa na kukosa umaarufu hata kwenye majimbo yao ila wanaotoka ccm kwenda upinzani wakiongeza wafuasi maradufu.

Nimeangalia namna Mbunge wa Kaliua alivyofifia, naangalia selasini, komu, na baadhi waliorejea bungeni Leo wanavyoshambuliwa na wananchi, najifunza kwamba kiburi Cha Mhe. Mbowe siyo kwenye idadi ya wabunge bali anatafuta ushujaa. Ameamua kusimama bila kuyumba kwa sababu anajua akiteleza hata leo akaenda chama kingine amejiua kisiasa.

Nadhani pia anafarijika sana kila anapotengwa na wale aliowaamini na bado akakuta nyuma yake wapo mamilioni ya Watanzania wanaomuunga mkono.

Ninajifunza pia kuwa maisha ya siasa za Tanzania kwa Sasa hayategemei Tena una wabunge wangapi bali unaweza usiwe Mbunge na bado ukawanyima usingizi watawala. Mfano mzuri Ni Mdude na Nondo, umaarufu wao hautokani na ubunge Bali unatokana na misimamo dhidi ya dhuluma.

Tumtafuta Slaa tumwambie aingie mtaani tuone atafuatwa na Nani, yupo wapi kafulila, namtafuta mtatiro kwenye ramani hayupo Tena.

Lakini pia natafuta angalau kijana mmoja ndani ya uvccm ambaye akisimama Leo akasema anagombea nafasi flani kwenye jamii bila kutumia pesa wala dola simwoni. Polepole alipata uungwaji mkono mkubwa ila amekuja kuishia kupata fedha Kama mshahara na kuishi maisha ya watu si maisha yake.

Ninaamini kwa njaa iliyopo kwa Sasa na ugumu wa ajira uliopo naamini Mhe Mbowe kufikia 2025 atakuwa na watu wachache wenye majina makubwa ila atakuwa mwenye wafuasi wengi endapo tu atawaacha waende akiamini ipo siku watarudi wakikataliwa.

Naiona chedema imara baada ya waomba ajira kwenda kuajiriwa.
 
Naskia Lijualikali katinga bungeni ..wewe Lijua jua utapigwa kofi na Mungu...wana ifakara ww
amekupambania sana wewe ndezi..
 
Ayo ndio mazara ya DJ kukurupuka, uwezi kuwa na uwezo mdogo wa kufikiri na ukawa unashauriwa na Mdee, Jacob au Lema ao wote wanafanya kazi kwa mihemko.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Title tu ina shida waliomwacha Mbowe? Tusijikute tunamwabudu mtu bila kujua ni udhaifu mkubwa sana, na Kwa Title hiyo hiyo ina maanisha Chadema ni Mbawe bila Mbowe hamna Chadema au Mali ya Mbowe.na sio taasisi tena, kazi ipo
 
I don't think so.

Alitumia muda kupata walioondoka , atatumia muda kupata wengine, kwa sasa yuko kwenye kipindi cha mpito, kwa bahati mbaya anaowapata nao hawakai it is a cycle ambayo itakidumaza Chadema ka muda mrefu.
 
Nimefuatilia wabunge wote wa vyama vya upinzani ikiwemo CHADEMA waliowasaliti wananchi na kujiunga CCM wakipoteza umaarufu wao kabisa na kukosa umaarufu hata kwenye majimbo yao ila wanaotoka ccm kwenda upinzani wakiongeza wafuasi maradufu.

Nimeangalia namna Mbunge wa Kaliua alivyofifia, naangalia selasini, komu, na baadhi waliorejea bungeni Leo wanavyoshambuliwa na wananchi, najifunza kwamba kiburi Cha Mhe. Mbowe siyo kwenye idadi ya wabunge bali anatafuta ushujaa. Ameamua kusimama bila kuyumba kwa sababu anajua akiteleza hata leo akaenda chama kingine amejiua kisiasa.

Nadhani pia anafarijika sana kila anapotengwa na wale aliowaamini na bado akakuta nyuma yake wapo mamilioni ya Watanzania wanaomuunga mkono.

Ninajifunza pia kuwa maisha ya siasa za Tanzania kwa Sasa hayategemei Tena una wabunge wangapi bali unaweza usiwe Mbunge na bado ukawanyima usingizi watawala. Mfano mzuri Ni Mdude na Nondo, umaarufu wao hautokani na ubunge Bali unatokana na misimamo dhidi ya dhuluma.

Tumtafuta Slaa tumwambie aingie mtaani tuone atafuatwa na Nani, yupo wapi kafulila, namtafuta mtatiro kwenye ramani hayupo Tena.

Lakini pia natafuta angalau kijana mmoja ndani ya uvccm ambaye akisimama Leo akasema anagombea nafasi flani kwenye jamii bila kutumia pesa wala dola simwoni. Polepole alipata uungwaji mkono mkubwa ila amekuja kuishia kupata fedha Kama mshahara na kuishi maisha ya watu si maisha yake.

Ninaamini kwa njaa iliyopo kwa Sasa na ugumu wa ajira uliopo naamini Mhe Mbowe kufikia 2025 atakuwa na watu wachache wenye majina makubwa ila atakuwa mwenye wafuasi wengi endapo tu atawaacha waende akiamini ipo siku watarudi wakikataliwa.

Naiona chedema imara baada ya waomba ajira kwenda kuajiriwa.
Mpuuzi mkubwa, huyu muhuni atakuja kupigwa mawe na watanzania wenye hasira kutokana na utapeli wake
 
Back
Top Bottom