MGANGA MCHAWI
Senior Member
- Oct 15, 2015
- 199
- 393
Nakumbuka tarehe 17/12/2010 majira ya jioni ndipo habari zilipoanza kuenea kwa kasi kuwa kuna kijana wa ki- Tunisia (Mungu amrehemu) amejichoma moto kwa kujimwagia Petrol kisha kujiwasha na kuanza kukimbilia kwenye moja ya kituo cha Polisi cha nchini humo.
Hakuwa Gaidi bali ni kijana aliyechoshwa na utawala wa kimabavu wa nchi yake.Ni kijana aliyehitimu chuo na kukosa ajira na kuamua kufungua kibanda cha kuuzia vitu vidogo vidogo ili aweze kujikimu kimaisha na kutimiza ndoto zake bila kujua eneo alilojenga kibanda chake serikali ilikuwa na mpango mwingine wa matumizi wa eneo hilo.
Serikali kupitia askari wake ikabomoa vibanda vingi vilivyopo eneo hilo kikiwemo kibanda cha kijana huyo kitendo kilichoamsha hasira kubwa kwa kijana huyo hadi kufikia hatua ya kujimwagia Petrol kisha kujiwasha na kuamua kukimbilia moja ya kituo cha polisi lengo ni kuungua pamoja nao japo hakufanikiwa kwa kuwa walimuwahi na kuzima moto uliokuwa unawaka mwilini mwake na kumpeleka hospitali ambapo tar 7/01/2011 alifariki Dunia.
Tukio hilo liliamsha hasira za vijana nchi nzima ya Tunisia na kukawa hakukaliki tena.Vijana walijitokeza barabani kwa wingi na kuanza kupinga utawala wa kimabavu wa nchi hiyo.Vijana hao hawakuhamasishwa na viongozi wa kisiasa bali chuki mioyoni mwao za muda mrefu dhidi ya serikali yao na utawala wa kiimla wa nchi hiyo.
Pamoja na Serikali kutumia njia nyingi kuwatawanya na kufanya wasikusanyike kwa kuzima mitandao yote ya kijamii na kutumia jeshi lenye silaha za kivita lakini hali ilikuwa mbaya zaidi kwani vijana walikuwa tayari kupigana kwa mawe na askari walioshika bunduki mpaka pale umma uliposhinda serikali yao.
Tukio hilo lilihamasisha vijana wa nchi zingine za kiarabu kwa kuamini kumbe wakiamua wanaweza na hapo ndipo Vijana wa Misri nao wakaingia barabarani na kudai haki yao.
Kilichotokea Tunisia niliamini kitakuwa funzo kwa Viongozi wengine wa Africa ila cha kusikitisha halijawa funzo kwao.Nashindwa kuelewa kwanini viongozi wetu wamekuwa na roho ngumu kiasi hiki?Kwanini wanataka kuturudisha kule tulipotoka?Kwanini wanatumia mabavu kujenga hofu kwenye mioyo ya watanzania?Kwanini wanataka kutuaminisha kuuana ni jambo la kawaida nchini mwetu?
Wakati kijana mawazo akiuliwa kinyama nliamini labda ni ugomvi wao nje ya siasa.Nliposikia Ben saanane amepotea sikuamini ila kwa sasa sina shaka kabisa kuwa amepotea na Mungu na waliohusika pekee ndio wanaojua kilichompata.Nilipata hofu kubwa sana pale nlposikia Tundu Lisu amepigwa risasi zaidi ya 30 mchana jua likiwaka.
Niliogopa zaidi pale Viongozi wa serikali walipozuia mikutano ya kisiasa kwa kigezo cha kuleta maendeleo ila hofu imeongezeka zaidi ninapoona nguvu zinazotumika kupoteza upinzani Tanzania kwa kuwa nina uhakika watawala wanataka watupeleke kule walipokuwa nchi za kiarabu za africa zilizokuwa na utawala wa kiimla.
Hivi watu wanaotembea barabarani bila kuleta vurugu una wapiga risasi za moto ili iwaje?Mnafikia hadi hatua ya kupiga mtu asiyekuwepo hata kwenye tukio furaha yenu ni nini??Hiki kiburi cha watawala wanakitoa wap?Mnaita hadi Press conference kuzungumzia tukio kwa kiburi cha dunia mnadiriki kabisa kusema eti kati ya risasi zilizopigwa hewani moja ilimpata binti mdogo aliekuwa kwenye daradara kweli?
Mnafikiri kugharamia mazishi ya binti kutaondoa hasira na chuki zinazojengeka mioyoni mwa wananchi?Mnafikiri hasira za watu kubomolewa nyumba zao zitaondoka kwa kujengewa barabara za juu?Hivi hiki kiburi cha kusema hamtabomolewa nyumba zenu mkiichagua CCM mna kitoa wap?Hiki kiburi cha kuagiza nyumba za mkoa furani zisibomolewe kisa walikuchagua mnakitoa wapi?
Hiki kiburi cha kutojari maisha ya wenzenu mnakitoa wap?Kwamba mnaamini nyie mtaishi milele?
Kiukweli nimesikitishwa sana na Kifo cha mwanafunzi wa NIT(Mungu amrehemu) ambaye hakuwepo kabisa na inawezekana hata alikuwa hajui nini kinaendelea ila nimesikitushwa zaidi na majibu ya viongozi juu ya tukio hili.
Ni kijana mdogo aliekuwa na ndoto zake za maisha ambaye aliamka asubuhi akiwa hajui kama kodi zake zinazotumika kuendesha serikali ikiwemo kununulia silaha ndizo itakayotumika kuondoa uhai wake.Nimewaza zaidi nlipoona mandhari ya nyumbani kwake ambako viongoz wa serikali waliotoa uhai wameenda kuhani msiba wakiwa kwenye magari ya kifahari wakati yeye na familia yake ikioonesha kuishi maisha ya kawaida na ya chini kabisa.
Hakika nawaambieni mkimaliza kufanya mlichopanga kufanya, na pale mtakapojua mmefanikiwa na kufanya mnachotaka ndipo hapo damu za wanyonge wote zilizopotea zitakapo inuka na kuamsha hasira za wananchi maskini mnaowadharau na kuwabeza na kuwaua kila siku.
Amini nawaambieni siku hiyo wananchi hawatamuhitaji Mbowe wala Kinana kuwaonesha njia na kuwapangia cha kufanya, bali ni wananchi pekee wakiongozwa na mioyo yao iliyojaa chuki na hasira za muda mrefu zilizosababishwa na kiburi chenu.
Mungu naomba tuoneshe nuru kwenye giza lililotanda mbele yetu.