Asante! Kumbe, nilikosa! Nilisoma kwa haraka mno basi sikutambua uliandika 'dhehebu' badala ya 'madhehebu'!
Hata hivyo, nilitafuta neno hili kwenye kamusi mbalimbali, lakini katika TUKI Kamusi neno 'dhehebu' halipo. Kamusi zote zinaonyesha kwamba neno 'madhehebu' linatumiwa kama 'singular' na 'plural'. Kamusi mbili zilitaja tu kwamba 'dhehebu' ni 'derived word' (lakini kwa ujumla halitumiwi), lakini 'madhehebu' linatumiwa kwa 'moja' na kwa 'uwingi'. Pia, ninapokuwepo Tanzania watu wanalitumia 'madhehebu' kwa 'singular' na kwa 'plural'. Kwa hiyo, sentensi, ''Je, inawezekana kila madhehebu ni sahihi?' ni sawa. Tafuta kwenye kamusi. Je, unaweza kuona tofauti?