Ipeni Dar es salaam Young Africa (Yanga) heshima yake

Lyrics Master

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2016
Posts
482
Reaction score
681
Katika pita pita zangu mitandaoni, nimeshuhudia kauli zinazoshangaza ,eti Yanga inamuogopa Simba! Jamani, kweli hii ni Yanga mnayozungumzia? au kuna Yanga nyingine? Hakuna timu hapa Tanzania inayoweza kumtisha Yanga! Ni ipi hiyo? Haipo! Yanga ni mfalme wa soka la Tanzania, na historia inashuhudia hilo kwa dhahiri.

Wanaosema Yanga anaikimbia Simba wamefumbia macho ukweli. Hii ni Yanga ile ile iliyompiga Simba mara nne mfululizo. Hii ni Yanga iliyomcharaza Simba mabao 1-5, kipigo kilichoandikwa kwa wino usiofutika kwenye vitabu vya historia ya soka la Tanzania. Hii ni Yanga, ambayo timu iliyoifunga mara nyingi kuliko zote ni Simba! Hii ni Yanga ambayo inawinda ubingwa wake wa 31 wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Kwa lipi hasa Yanga imuogope Simba?

Tunapozungumzia hadhi ya Yanga, hatuzungumzii timu ya kawaida. Timu hii ni alama ya heshima, ni urithi wa mpira wa miguu wa Tanzania. Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Baba wa Taifa, alikuwa mwanachama wa kwanza wa Yanga. Hivyo basi, kumdharau Yanga ni sawa na kudharau historia ya taifa hili.

Hivi majuzi, kiongozi mkuu wa TFF aliposema kuwa malalamiko na madai ya Yanga ni utoto, aliteleza vibaya! Hii sio tu dharau kwa viongozi wa Yanga, bali pia ni dharau kwa mashabiki wake, wanachama wake, na urithi wake mkubwa. Heshima kwa Yanga ni heshima kwa mpira wa miguu wa Tanzania!

Mafanikio hayana mjadala!

Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, hakuna timu nyingine katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati yenye mafanikio makubwa kama Yanga. Kufika fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF si jambo la kubeza. Kushindwa kuchukua ubingwa kwa tofauti ya mabao tu si jambo dogo. Kutolewa na Mamelodi Sundowns kwa magumashi si udhaifu wa Yanga, bali ni nguvu ya mfumo ulioshindwa kusimamia haki. Yanga imekuwa ngome isiyopenyeka, na rekodi yake ya kutopoteza mechi kwa muda mrefu ni ushahidi tosha kuwa hii ni klabu inayopaswa kuheshimiwa.

Wanaosema Yanga inamuogopa Simba wanapuuza ukweli. Wanadhalilisha mpira wetu. Wanajenga simulizi za uongo. Mpira wa miguu ni heshima, ni historia, ni ushindani wa haki. Upeni heshima mpira wa miguu!

Na mwisho, mpeni heshima yake Eng. Hersi Said. Mtu huyu akiwa angali hai, amefanikisha maendeleo makubwa ndani ya Yanga. Heshima yake ni heshima ya klabu, ni heshima ya mpira wa Tanzania.

Na kwa Wallace Karia – kuwa na heshima na Yanga! Kama baba anavyoongea na wanawe kwa hekima, basi tambua kuwa Yanga ni msingi wa mpira wa Tanzania. Bila Yanga, hadithi ya soka la Tanzania itakuwa na mapengo yasiyoweza kuzibika!

IPENI YANGA HESHIMA YAKE!
 
Haya Sasa vyura jaribuni kuleta kiburi kutokuleta timu uwanjani tarehe ya marudio ya derby itakapopangwa. Mtajua hamjui.
 
Kama viongozi hawakuheshimu kwa nini tuipe heshima?
 
Haya Sasa vyura jaribuni kuleta kiburi kutokuleta timu uwanjani tarehe ya marudio ya derby itakapopangwa. Mtamjua hamjui.
sentence yako haifichi ukweli kwamba YANGA ndio team bora hapa Tanzania
 
Tuendelee kula mtori nyama ziko jikoni
GhldYfQXQAAonLc.jpeg
 
Huu ni mwandiko wa Haji Manara.

Yanga imekosa viongozi na imeamua kuongozwa na majeshi ya kukodi kama yale ya Interahamwe, M23 na Janjaweed na inaonyesha Manara na Jerry Muro ndiyo wasemaji wa hayo makundi.
 
Mambo mengine yanafurahisha sana! Yaani unakimbia mechi kwenye tarehe iliyopangwa kwa sababu za kitoto, halafu baadaye unakuja kujisifia bila hata chembe ya aibu eti ile timu uliyoikimbia; inakuogopa!
 
Haya Sasa vyura jaribuni kuleta kiburi kutokuleta timu uwanjani tarehe ya marudio ya derby itakapopangwa. Mtamjua hamjui.Aru

Haya Sasa vyura jaribuni kuleta kiburi kutokuleta timu uwanjani tarehe ya marudio ya derby itakapopangwa. Mtamjua hamjui.
Marudio ya nini? sisi tusha maliza mechi nyie kama mna marudio mtacheza nyie na Simba queens
 
Katika pita pita zangu mitandaoni, nimeshuhudia kauli zinazoshangaza ,eti Yanga inamuogopa Simba! Jamani, kweli hii ni Yanga mnayozungumzia? au kuna Yanga nyingine? Hakuna timu hapa Tanzania inayoweza kumtisha Yanga! Ni ipi hiyo? Haipo! Yanga ni mfalme wa soka la Tanzania, na historia inashuhudia hilo kwa dhahiri.

Wanaosema Yanga anaikimbia Simba wamefumbia macho ukweli. Hii ni Yanga ile ile iliyompiga Simba mara nne mfululizo. Hii ni Yanga iliyomcharaza Simba mabao 1-5, kipigo kilichoandikwa kwa wino usiofutika kwenye vitabu vya historia ya soka la Tanzania. Hii ni Yanga, ambayo timu iliyoifunga mara nyingi kuliko zote ni Simba! Hii ni Yanga ambayo inawinda ubingwa wake wa 31 wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Kwa lipi hasa Yanga imuogope Simba?

Tunapozungumzia hadhi ya Yanga, hatuzungumzii timu ya kawaida. Timu hii ni alama ya heshima, ni urithi wa mpira wa miguu wa Tanzania. Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Baba wa Taifa, alikuwa mwanachama wa kwanza wa Yanga. Hivyo basi, kumdharau Yanga ni sawa na kudharau historia ya taifa hili.

Hivi majuzi, kiongozi mkuu wa TFF aliposema kuwa malalamiko na madai ya Yanga ni utoto, aliteleza vibaya! Hii sio tu dharau kwa viongozi wa Yanga, bali pia ni dharau kwa mashabiki wake, wanachama wake, na urithi wake mkubwa. Heshima kwa Yanga ni heshima kwa mpira wa miguu wa Tanzania!

Mafanikio hayana mjadala!

Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, hakuna timu nyingine katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati yenye mafanikio makubwa kama Yanga. Kufika fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF si jambo la kubeza. Kushindwa kuchukua ubingwa kwa tofauti ya mabao tu si jambo dogo. Kutolewa na Mamelodi Sundowns kwa magumashi si udhaifu wa Yanga, bali ni nguvu ya mfumo ulioshindwa kusimamia haki. Yanga imekuwa ngome isiyopenyeka, na rekodi yake ya kutopoteza mechi kwa muda mrefu ni ushahidi tosha kuwa hii ni klabu inayopaswa kuheshimiwa.

Wanaosema Yanga inamuogopa Simba wanapuuza ukweli. Wanadhalilisha mpira wetu. Wanajenga simulizi za uongo. Mpira wa miguu ni heshima, ni historia, ni ushindani wa haki. Upeni heshima mpira wa miguu!

Na mwisho, mpeni heshima yake Eng. Hersi Said. Mtu huyu akiwa angali hai, amefanikisha maendeleo makubwa ndani ya Yanga. Heshima yake ni heshima ya klabu, ni heshima ya mpira wa Tanzania.

Na kwa Wallace Karia – kuwa na heshima na Yanga! Kama baba anavyoongea na wanawe kwa hekima, basi tambua kuwa Yanga ni msingi wa mpira wa Tanzania. Bila Yanga, hadithi ya soka la Tanzania itakuwa na mapengo yasiyoweza kuzibika!

IPENI YANGA HESHIMA YAKE!
Kabisa kabisa.
 
Back
Top Bottom