ipad 4 vs samsung galaxy note 10.1

Gudasta

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2011
Posts
627
Reaction score
1,153
Habari wana jf, Kama thread inavyojieleza ni kwamba nataka kununua ipad 4 au samsung galaxy note 10.1, naomba kwa ambae ameishatumia hizi gadgets au anayezifahamu vizuri anielezee ipi ni nzuri interms of quality of picture and video, speed, free apps from store, battery life, camera, etc, nitashukuru sana kwa msaada wenu kwani utaniwezesha kununua kitu sahihi, hasa napenda nijue ni ipi kati ya hizo ambayo ina apps nyingi za bure.
 
mkuu kiujumla ipad ni nzuri kuliko note lakini kwa criteria zako zinaweza change decision.



tuanze na quality of picture and video

japo hujaspecify uchukuaji wa picha na video au kuangalia picha na video (kwa kudownload au kutoa kwenye pc yako)

mkuu ipad 4 kioo chake ni full hd sababu ina resolution ya 2048 x 1536
pixels inayoresult kwa 264 pixel kwa kila nchi 1 hiki ni kioo advance sana kwa tablet.

Note 10.1 ina hd(sio full hd) maana ina resolution ya 1280 x 800
pixels na pixel 149 kwa kila nchi

hizo specification hapo juu zinadetermine quality ya picha utakayoiangalia kwenye kioo. Na ipad four imeshinda kwenye quality ya picha.

Kwa maelezo zaidi ya kukuelimisha kujua kama kitu ni hd au full hd unaangalia namba ya 2 ya resolution. Ikiwa imezidi 720 hio inaitwa hd na ikiwa imezidi 1080 hio inaitwa full hd, ina maana note namba ya pili ya resolution 1280x800 ni 800 hii imepita 720 lakini haijafika 1080 so inakua hd na sio full hd. Ipad 4 imefika 1080 ndo mana nikasema ni full hd.

Tuendelee hapa hapa kwenye picha na video lakini sasa tuongelee quality ya picha utakayochukua.

Zote mbili zina camera ya 5mp lakini camera ya ipad 4 ina uwezo wa kuchukua full hd (1080) wakati ya note inachukua hd kawaida (720p)

kwenye front camera zote zinazo sema note ina camera ya kawaida ya video calling wakati ipad 4 ina front camera ya hd (720p)

hapa napo kwenye uchukuaji wa video ipad ni bora.

speed
mkuu kwenye speed specs wise note ina specification kubwa ikiwa na 1.4 quadcore processor na ram 2gb wakati ipad 4 ina 1.4ghz dual core processor na ram 1gb.

Ila hapa kuna kitu unote android inatumika kwenye note sio smooth kama ios inayotumika kwenye ipad, unaweza ukawa na note yenye specification kubwa lakini isiwe smooth kama ipad yenye specification ndogo.

apps
mkuu apps ipad inazo nyingi kuna kadiriwa apps 300,000 za ipad ambazo zipo optimized kwa ajili ya tablet tatizo nyingi si bure.

Android nayo ina apps za bure nyingi ila tatizo lake nayo hazipo optimised na tablet. Mfano unakuta apps ni ya simu basi ikirun inaonekana kwa udogo ile apps haichukui screen nzima

kwa hio hapa angalia mwenyewe.

Pia mkuu apss za ipad si bei sana nyingi ni cent 99 za kimarekani around 1500 za bongo.

battery
kwenye battery mkuu zote zipo vizuri zinaweza kaa siku nzima kwa matumizi heavy ukachaji usiku. Japo sina data za kutosha kwa note ila review nyingi za ipad 4 zinaonyesha inakaa siku 3 hadi 5 kwa matumizi ya kawaida
 

Mkuu aksante sana kwa maelezo yako yatanisaidia sana kufanya maamuzi
 

Mkuu asante sana kwa uchambuzi huu hii kitu ilikuwa inanisumbua kichwa hasa Samsung Galaxy Note zinavyo kuwa advertised!!

Labda kuna kitu hapa nakumbuka nilikiona kwenye net kuwa Samsung Galaxy Note ina pre installed photoshop ambayo itawafaa sana ma artist. Labda na hiki ni kitu cha ku consider wakati una compare na ipad.
 

sjajua mkuu kuhusu hilo ila apps nyingi za android ni port za ios ina maana developer wengi wanatengeneza kwanza kwenye ios then ndo wanaziport kwenda android.

Na hio photoshop ya note ni bure? Au ndo wameeka trial version ukinunua unalipa
 
1. kitu kikubwa kinachoboa kwenye iPad ni kwamba huwezi kupiga wala kupokea simu au sms kama kwenye simu za kawaida. Hii inaleta shida sana wakati wa kuongeza vocha inabidi utoe line kwenye simu alafu urecharge kupitia simu ingine ndo urudishe kwenye iPad. Applications zingine kama whatsapp na viber zinazohitaji uwezo wa simu zinakuwa hazisupport kwenye iPad. Otherwise itakulazimu uJailbreak!
2. Kingine ni kwamba iPad haziingizi memory card hivyo inakuwa shida kufanya expansion ya storage.
3. iPad haina USB Host support ambayo ni muhimu kuwezesha kuchomeka (flash disk, mouse, keyboard, powered external hard disk etc) kwenye device yako.
4. Applications nyingi za Note 10.1 ni bure na unapata a full version 'photoshop touch' kwenye tablet yako.
5. bei ya iPad 4 ni kubwa sana almost twice bei ya note 10.1 ( 1.1mil for Note 10.1 'samsung store' wakati iPad 4 inafika mpaka 1.8mil)
6. Uwezekano wa kushare data na device zingine kupitia Bluetooth ya Note 10.1 (iPad ni kwa Apple devices otherwise through Jailbreak), na pia Note 10.1 inakuja na ir port inayokuwezesha kutumia remote ktk devices kama Tv, Radio, etc..
7. Android 4.2.2 Jelly Bean ni nzuri sana ina features nyingi ukilinganisha na IOS, na inaruhusu customization kibao kwakuwa ni open source.
8. Camera zote ni 5MP although zinatofautiana features.
9. Battery ya Note 10.1 ina nguvu sana (1500hrs of standby time ukilinganisha na 720hrs of iPad's) pia ina talk time kubwa of about 33hrs compared to 9hrs za iPad.
10. Note 10.1 ni nyembamba na nyepesi zaidi ukilinganisha na iPad 4.
11. Kioo cha iPad kina resolution kubwa kulinganisha na Note 10.1.
12. Browser ya Note 10.1 inaSupport Adobe Flash hivyo inasaidia kuplay flash contents papo kwa hapo unavyoBrowse internet.
13. Note 10.1 inakuja na S Pen stylus stick (nzuri kuchorea, signature, navigation na kwa mambo ya Artistic).
14. Note 10.1 ni rahisi kutransfer data from computer to tablet na kuzipangilia kama unavyofanya kwenye computer ofisini au nyumbani kupitia file manager (iPad ni lazima uJailbreak ili kupata iFile). iPad syncronisation ni ngumu na maranyingine unaweza ukadelete data zako accidentally kwasababu syncronisation inahitaji utumie computer moja tu otherwise ufanye transfer backup kwanza ndo usync!
15. Note 10.1 inaruhusu kuExplore root directory inayosaidia kuUpload chochote kutoka kwenye simu na kuDownload chochote kwenda kwenye simu (eg. Torrent files, files with various extensions wakati iPad inadownload compatible extensions tu (.ipa,.pdf,,),

All in all zote ni nzuri lakini nadhani Samsung Galaxy Note 10.1 ina Specification za kisasa zaidi na hutoboreka kuitumia. Its loaded!
 
sjajua mkuu kuhusu hilo ila apps nyingi za android ni port za ios ina maana developer wengi wanatengeneza kwanza kwenye ios then ndo wanaziport kwenda android.

Na hio photoshop ya note ni bure? Au ndo wameeka trial version ukinunua unalipa
iPad pia ina photoshop Touch, imetulia sana tu, lakini app moja isiwe ndio sababu ya kuchagua Tablet.
 
In simple words: If you like to pay more and live in a jail then ipad 4 it is. If you want freedom to do whatever you want to do with your device then galaxy note 10.1 it is.

It is more of a battle of iOS vs Android than physical hardware.
 
Nadhani chief-mkwawa ameeleza vizuri mambo mengi. Kikubwa zaidi kuhusu ipi bora kati ya mbili hizi kila mmoja atakupa hoja kwa utashi wake. Mpaka sasa pamoja na kuwepo utitiri wa tablet za Android iPad bado ina market share kubwa, hii ina maana watumiaji wengi hupendelea iPad, labda nigusie mambo machache tu kwa ufupi:-

Faida za iPad (baadhi)
- Ni rahisi kuitumia

- Ina Apps nyingi za quality ya juu kulinganisha na zile za Android.

- Skrini ni ya hali ya juu (high resolution)

- Una uhakika wa upgrade kwa angalau miaka mitatu ijayo (iOS mpya) [Samsung wana-acha ku-upgrade baada ya mwaka tu ukiwa na bahati basi miaka 2, tena hizo update zenyewe zinachelewa mno]

- Iko professional zaidi kwa vile implementation ya app za kikazi na mambo ya maana ni ya uhakika.

Faida za note 10.1 (baadhi)

- Ni kubwa zaidi kwa 0.4" kuliko iPad (sidhani kama hii ni faida yenye uzito anyway)

- Unaweza ku-customise, hii ndio sifa kubwa ya Android devices.

- Ina "peni" fulani ambayo inaongeza burudani kiasi katika matumizi (haina matumizi ya maana sana)

- Ni bei rahisi sana kulinganisha na iPad

- Unaweza kupata Apps zinazouzwa bila ya kununua kama uko tayari kui-root (ingawa hili pia linawezekana kwenye iPad kama utakuwa tayari kujailbreak)

- Implementation ya multi tasking ni nzuri na widgets ni ziada ambayo haipatikani kwenye iPad.

Kwa ushauri wangu: Kama unataka "toy" muda wote unachezea na kuibadili badili (customisation) na mambo kama hayo basi Note 10.1 inafaa sana. Kama unataka Tablet kwa shughuli za maana(kazi, mwanafunzi au biashara) nunua iPad.
 
Last edited by a moderator:
Mkubwa,

Huwezi ku "jailbreak" tablet ikageuka simu!

Ipad haina uwezo wa kupiga simu, period!

Na haina uwezo wa kutuma text message, kwa hiyo huwezi hata kuongeza salio bila kuchomoa ki sim card. Kero tupu!
 
Mkubwa,

Huwezi ku "jailbreak" tablet ikageuka simu!

Ipad haina uwezo wa kupiga simu, period!

Na haina uwezo wa kutuma text message, kwa hiyo huwezi hata kuongeza salio bila kuchomoa ki sim card. Kero tupu!
ni kweli kero tupu mkuu, lakini kuna jamaa flani wameweza kutengeneza tweak inayowezesha ipad kupiga simu na kutuma sms after a jailbreak. Kwenye Cydia kuna tweak inaitwa (phonelt ipad) kupitia repostitory (app.iphoneislam.com) inawezesha hizo features na inaongeza dial pad japo ina cost kidogo na ipo limited to some ipad models na atmost ios 5!

!
 

Hapo kwenye RED naona kama biased comment kwa sababu it's not true kwamba ni toy. Ila nakubaliana na ulichosema kwa IPAD inatumika na inatumiwa ki professional zaidi.

Kwangu mimi it's very hard decision and you have to think thrice before making any decision!!
 
Last edited by a moderator:
<br />
<br />
mkuu acha masikhra note 10.1 toy?......note ndio habari ya mjini ndani ya note user unafanya unavyotaka....wakati kwenye ipad 4 user hawezi kutamba kama kwenye note....mkuu note ndio mpango mzima.
 
&lt;br /&gt;<br />
&lt;br /&gt;<br />
mkuu acha masikhra note 10.1 toy?......note ndio habari ya mjini ndani ya note user unafanya unavyotaka....wakati kwenye ipad 4 user hawezi kutamba kama kwenye note....mkuu note ndio mpango mzima.


mtu anaposema toy kwenye tech anamaanisha sio productive apps zake nyingi ni za kitoto zaidi sio za kiproffesional.

Apps nyingi za android either zimekua ported toka ios au kama ni native ichunguze chunguze utakuta ina background fulani za umalware.


Ndo mana unakuta watu wengi makazini wanachagua ipad maana ana uhakika atapata software za kumanage wafanyakazi pamoja na security vya uhakika.
 
Kwa kawida humu ndani kunapokuwa na debate ya ulinganifu kati ya apple products na samsung naona kila mdau anatake side fulani. Hii inanipa picha kila mtu anaipigia debe aina ya gadget anayoitumia, sio mbaya ni hulka ya kawaida kwa binadamu kuthamini kile anachotumia au kumiliki. So mtoa mada chukua michango yote hasa ile uliyoitegeme kuipata then ikusidie kufanya maamuzi. Dhaifu kwako haina maana ni dhaifu kwa mwenzako pia, inategemea na vigezo vyake.
 

Advantage kubwa ya Android ni customisation. Isn't customisation just "toying" with your device? It looks blue, it has a different skin, it has more pages, change the look of the digital watch, port another firmware altogether, put live background, change menu positioning, lets be honest there is nothing productive here, take it as no offence as I personally do "toy" with my android devices a lot, its just having fun.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…