INTIMIDATION NI NINI?

Mjema Vushanje

Senior Member
Joined
Sep 24, 2017
Posts
158
Reaction score
355
INTIMIDATION NI NINI?

INTIMIDATION ina maana na tafsiri mbalimbali hasa ukitegemea na muktadha Stahiki.

Intimidation ni kitendo cha kumfanya mtu aogope, yaani akuhofie kiasi kwamba utakachomwambia ama kumuamrisha atekeleze.

Intimidation imewahi kutumiwa na wakoloni wakati wanafanya harakati za kuanzisha utawala wao katika nchi za afrika. Walifanyaje?

Wakati flani walikuwa wanatafuta mtu mbishi, ama kiongozi wa kiafrika anaekataa kuwatii na kumpiga risasi hadharani.
Ama pia waliweza kumchukua [mtu wa mfano tu] na kumchinja hadharani. Hii iliwafanya watu wawaogope.
Mbinu nyingine ni kufanya mazoezi ya kijeshi jirani na eneo wanalotaka kulitawala. Hapa utakuta askari wale wa kikoloni wanapiga kwata la nguvu huku wamenyoosha mistari yao wananyanyua miguu usawa wa kifua kisha wakishusha vumbi linatibuka. Zoezi hili lilifanyika kule dodoma hatimaye kesho yake walivyokuja ili kuvamia kile kijiji walikuta hakina mtu hata mmoja.

Kingine ambacho kinatumika ni kauli za vitisho, kauli hizi huwa ni za kibabe sana, mtu yeyote ambaye sio jasiri akisikia kauli hizo huahirisha kile alichopanga kufanya na kujikuta ametii. Kuna stori moja ya mzee aliyewahi kuibiwa simu kwenye gari ila alipouliza ninani amechukua kila mtu alikaa kimya.
Yule mzee aliamua ku'intimidate' watu kwa kuwaambia "kama simu hairudi basi naenda kufanya kile nilichofanya miaka ya sitini" baada ya kusema hivyo simu ikarudi. Hiyo ni intimidation.

Turudi kwenye pointi yetu...

Watu wanaweza kukuintimidate kwa mbinu nyingi, mfano mko shuleni alafu kuna mtu amefanya kosa ila walimu hawamjui. Ili kuwafanya mumtaje wanatumia mbinu ya intimidation... Mkiwa mmepanga kutosema unaletwa mzigo wa fimbo alafu zinamwagwa mbele yenu 'hwaaa' alafu mwalimu mmoja mnoko anasema "leo tutawanyoosha wote mpaka mseme" hapo sasa wale waoga lazima wataje!

Wakati mwingine mtu ambaye una ugomvi nae kabla hamjapigana anavua shati na kuliweka pembeni ... Ile ni intimidation, lengo lake ni uone misuli yake ili uogope usipigane nae, ama upigane ukiwa na hofu na ukishakuwa na hofu ni rahisi kukushinda.

Utajisikiaje mtu uliyemkosea na mnakaa nyumba moja au majirani kisha unamuona kila wakati ananoa panga lake na kulihifadhi ndani? Hiyo ni intimidation!

Nataka nikwambie kitu wewe usiyejua....

Watu wote wanaofanya intimidation kiuhalisia ni waoga kuliko wewe wanaekutisha. Kama wangekuwa na uwezo kuna sababu gani mpaka wakutishe? Si wafanye vitendo?

Kingine ni kwamba ukiona mtu anatoa maneno au anafanya vitendo vya kuku'intimidate' ujue hawana uwezo wa kupambana na wewe, wanaintimidate ili usipambane nao kwani wanajua utawashinda.
UKIMTAMBUA MTU ANAYEKUINTIMIDATE PAMBANA NAE UTASHINDA!
 

Attachments

  • images.jpeg
    21 KB · Views: 39
Hata kile alichofanyiwa Dr. Ulimboka ilikuwa ni Intimidation.
 
Though comment yangu ni namba 6,bado niko front seat.
Wacha ni Subscribe kabisa
 
Watu wote wanaofanya intimidation kiuhalisia ni waoga kuliko wewe wanaekutisha. Kama wangekuwa na uwezo kuna sababu gani mpaka wakutishe? Si wafanye vitendo?
Sawa kabisa Mjema; ila awmu ya 5 inafanya kweli!!!!
 
Kwenye serikali ya kidikteta INTIMIDATION na TERMINATION vinaenda sambamba. [HASHTAG]#HUTU[/HASHTAG]
 
Unamaanisha tar 264 tuingie Barabarani kama kawa au?
 
hana lolote mwoga kuliko kunguru huyu. dawa yake 26.4
 
Hilo neno gumu "intimidate" lilikuwepo kichwani then likapoteaga.
Jaribu kukumbuka wapi! Nikaamua ku-search other names for terrible, ndio nikajikuta nafika mpaka hapa.
 
Hata msemo wa mbayuwayu wa Mzee wa msoga enzi za maandalizi ya mgomo wa Tucta 2010 ilikuwa ni ku intimidate.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…