Interview yoyote inahitaji mtu mwenye general knowledge ya mambo ya nchi na dunia, kuwa na sifa ya unachokiomba, beba vyeti vyako vyooote original, kuwa nadhifu kwa muonekano, acha kujiremba na kujipodoa kupita kiasi, onyesha confidence kuwa unaifahamu vema kazi unayoiomba, jibu maswali kwa ufupi na ufasaha bila ya kuzunguusha maneno, na kama hujui kuwa wazi badala ya kusema uongo. Onyesha kujiamini kwa kutazamana usoni na wanaokuhoji. Salimia watu kabla na shukuru watu baada.