INTERVIEW: kutana na interview ya Incredible terminator hapa.

INTERVIEW: kutana na interview ya Incredible terminator hapa.

incredible terminator

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2016
Posts
2,530
Reaction score
4,274
Habari wakuu, Mara nyingi watu ambao sio maarufu huwa tuna nondo na mambo kibao ya kushare katika jamii lakini huwa hatuhojiwi mwisho wa siku tunakufa na nondo zetu, cha ajabu wanaohijiwa ili kushare experience ni hawa watoto wajinga wasiojielewa kazi kutuonesha makalio. sasa ngoja nianze hapa
nitatumia mfumo wa dialogue yaani mahojiano kama thamthilia ila mwanzo nitaanza na utambulisho,

Naam mpendwa msomaji wa Jf leo tumekuatana na mchangiaji maarufu Incredible terminator karibu sana.

MTANGZAJI: Karbu sana ndugu terminator kwanini uliamua kujiita terminator na sio jina jingine

TERMINATOR: ahsante jina la terminator ni jina nilikuwa nalo tangu mda mrefu hata kabla ya kupata wazo la kujiunga jf na linatokana na maisha yangu binafsi ambayo sidhani kama kuna umhimu wa kushare kwa watumiaji wa JF.

MTANGAZAJI: Terminator unaonekana ni mtu flani mwenye nidhamu na mtu flani mwenye hadhi flani ya kiukubwa ila unazungumziaje post zako za nyuma ambazo always zilionekana zimekaa kiuongo uongo na zinazungumzia masuala ya mapenzi n.k

TERMINATORr: Kwanza kabisa naomba kuweka sawa kwamba JF kuna majukwaa mengi na kila jukwaa lina content zake so linapokuja suala la kuchanganya content au kushare link ya post yenye content flani katika post nyingine na katika jukwaa jingine nadhani ni suala la kukosa nidhamu na kukoseana heshima sababu kila kitu kina maandhari yake, hapo ni sawa na mtu kukuletea chakula bafuni, kwa maana hiyo ni kwamba kila post inapostiwa kulingana na content ya jukwaa husika Pia licha ya hapo JF haijaanza leo kuna watu wamekulia jf kuna mtu yupo JF tangu 2007 hadi sasa 2021 bado wapo Jf kwa maana kwamba watu wanakuwa watu wanabadilika wanakua wakiwa ndani ya JF kwa hiyo mtu anapopekenyua post yako ya mwaka 2009 na kuja kuiunganisha na post ya mwaka 2021 nadhani ni kukoseana heshima na ni suala ambalo moods wangedeal nalo maana ni kukoseana nidhamu kabisa, kama mtu alitoa post miaka hiyo hana mke hana familia wala kazi na leo ukaja kuiunganisha na post ya mwaka huu ambao mtu huyohuyo keshapata kata kazi na tayari ana watoto na familia ni kiwango kikubwa sana cha human violation ambacho sio cha kufumbiwa macho na uongozi wa JF. Hapo ni sawa na kuendelea kuiamini katiba ya nchi ambayo ilitungwa miaka ya 1970s na chakufurahisha na chakutofautisha ni kwamba bora katika katiba maana kuna vifungu vinafanyiwa marekebisho ila katika fasihi andishi haibadiliki, ''''labda tu nikuulize swali wewe hujawahi kupitia post zako za zamani au jumbe zako za zamani za messenger hadi ukajikuta unajidharau mwenyewe? hapa inabidi watu wakubari kuna ukuaji na mabadiliko ya kifkra,

MTANGAZAJI: Terminator inaonekana umekuwa mstari wa mbele kuanzisha nyuzi ambazo zinatuonyesha mafanikio yako, pengine huoni kama hii inaleta picha mbaya kuwa unajiona na kujimwambafai?

TERMINATORr: Hahahaa wewe hapo ulipo hujioni?..... suala la watu kuamini kama unajimwambafai lilikuwepo tangu enzi na hakijaanza leo ila sababu kubwa sio kwamba kweli hawapendi kuona unashare maendeleo yako, tatzo wanakuwa na makasiriko juu yako kwa kuona umefanikiwa umewaacha wao, maana siku zote binadamu tunaombeana tufeli ili ionekane tuko sawa, na kama huamini siku moja share na ndugu zako tatzo linalo kukabiri utaona wako upande wako kukupa pole ila siku ukishare tatzo limeisha na inatakiwa kulipwa fidia ya milioni mia tano utaona kama kuna mtu atasimama upande wako kukupongeza tena, utawaona kila mtu anaitikia mwitikio baridi na kusepa zake, kwa hiyo mimi sijali kuhusu wao wanasema nini? na suala la watu kusema jamaa mbona anavimba kisa kanyumba ka vyumba viwili na kavitz kwa kuamini kuwa ulichokipata sio chochote, ila twende mbele turudi nyuma kila mtu anafurahia alichokipata kwa kuangalia alipotoka, ikitokea umetokea katika familia ambayo hata baiskel mlikuwa mnaazima kwa jirani na leo hii unaendesha Vitz why usifurahie ushindi? ni kweli kuna watu wanaendesha maV8 and still hawajisifii ila inategemea hiyo V8 ilipatikana kwa mazingira gani, hata mimi nitakuoana wa ajabu kama familia yako ilikuwa inaendesha Prado alafu wewe ukaendesha VItz utakuwa binadamu wa ajabu kuwahi kutokea maana kiuchumi hapo itaonekana graph ya maisha umeishusha ila alietoka katika baiskel to Vitz itaonekana umepandisha graph why usienjoy?, Pia nadhani kuna notion ambayo jamii imeijenga kuwa mtandaoni ni sehemu ya kushare maumivu tu kama vifo na magonjwa na fitina kitu ambacho sio sahihi, kila mtu anapaswa kushare anachoona kinamfaa kwa mda huo, na kuna wengine wanashare vitu mtandao kama kuhifadhi maudhui (memory)
cool men achen majungu hakuna asiyejinosha hata hizo picha mnazoshare mitandaoni ni kujiona maana kuna wenzenu hawana hata afya ya kuweza kushare picha wanapambania uhai wao ICU pia kuna wengine wanawazia chakula cha usiku na hawawezi hata kutumia simu wala kumiliki bando kwa hiyo cool men.

MTANGAZAJI: Ahsante sana ternminator umetisha sana una nini chakuwashauri vijana ambao wanatamani kufikia ulipo

TERMINATOR: Ninachowashauri wakaze but wajaribu kujitengeneza wao wasiige kila kitu kwangu maana pengine njia nilizopita wao hawawezi kuzipita kwa hiyo kijana asipende kuiga kila kitu kwa waliomtangulia kimafanikio maana nyuma ya mafanikio kuna behind scene nyingi ambazo watu hawazizungumzii kikubwa tu if you want to success try to be you always usiige kuwa mimi hauwezi kuwa mimi maana hata ukijaribu kupitia njia niliyopitia huwezi kujua wapi nilipokanyaga nikabaki salama na hata ukijaribu kukanyaga pengine mguu wako hatuweza kufitisha njia, maisha ni kama fingerprint huwezi kufungua njia yangu isipokuwa mimi tu kwa hiyo jaribu njia zako mwenyewe huku ukiamini mungu yupo, hivi hivi ukijarubu kuniiga kwa kila kitu na kujifanya unanijua sana tutakuita chawa which is not good.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom