Dada yangu amemaliza masomo yake ya udaktari wa binadamu mwezi huu,nchi moja ya Ulaya.Kuna nchi nyingine amepata nafasi ya kufanya internship lakini mwenyewe amesema,anapenda zaidi kuja kufanya internship yake Tanzania ili apate uzoefu zaidi kwa vitendo kwavile kuna wagonjwa wengi na madaktari ni wachache.
Ana maswali yafuatayo:
1.Kama atakuja mwezi ujao wa November,itamchukua muda gani mpaka atakapoanza kufanya hiyo internship?Yaani mchakato mzima wa kutuma maombi,kukubaliwa nk huwa unachukua muda gani?
2.Ni wapi pazuri kufanya internship na kujifunza zaidi kati ya Muhimbili na hospitali za Wilaya za Dar kama Mwananyamala au Temeke au Hospitali za Mikoani na Wilayani?
3.Kwa siku intern doctor anatakiwa afanye kazi kwa masaa mangapi?Ni jumatatu mpaka Ijumaa au hata weekends?
4.Je kuna posho/mshahara?Ni shilingi ngapi kwa mwezi?
5.Atapata likizo?Kwa mwaka ni wiki ngapi?
Madaktari na wakuu wengine mnaofahamu,naomba majibu tafadhali
asante mk
uu Mahmetkid kwa majibu mazuri.Nitamtumia kama ulivyoandika.Unaweza pia kunitajia basic salary ya Daktari ambayo ndiyo mshahara wa Intern doctor?
posho ya intern doctor ni 80% ya basic salary ya daktari...na kama anataka uzoefu zaidi aende hospital za mikoani,,,,hamna likizo
nimekuPM MKUU CHECK INBOXangalia ur inbox
angalia ur inbox
Nadhani itabidi arudie ila nimembiwa kuna nchi ukifanya intern ukija bongo ni moja kwa moja ila majority naona wanarudia kufanya wakifika bongo.....ila usitie shaka kurudia maana ni muhimu kujifunza health system ya bongo kabla hujaingia kazini jumla jumla ukizingatia pia atapokea 80% ya mshahara wa daktari si haba...shukran mkuu kwa majibu yako mazuri..swali la mwisho..kama atafanyia nje internship,let's say Ulaya,halafu akataka kuja kufanya kazi Tanzania kama daktari,atapokelewa na kuanza kazi moja kwa moja au itabidi afanye tena internship Tanzania?
Nadhani itabidi arudie ila nimembiwa kuna nchi ukifanya intern ukija bongo ni moja kwa moja ila majority naona wanarudia kufanya wakifika bongo.....ila usitie shaka kurudia maana ni muhimu kujifunza health system ya bongo kabla hujaingia kazini jumla jumla ukizingatia pia atapokea 80% ya mshahara wa daktari si haba...
Mkuu La Cosa Mia,nashukuru.Huyu binti pia amepata nafasi ya kufanya internship Ulaya.Lakini baadaye lengo lake ni kurudi Tanzania.
Hizo nchi ambazo akifanya intern hawezi kurudia tena Tanzania,ni za Afrika au hata nje ya Afrika?Unaweza kuzitaja?Lakini kama ulivyosema,hata akirudia tena intern pia si mbaya.Nitamjulisha