Interesting... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Interesting...

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mtoboasiri, Jan 8, 2011.

 1. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #1
  Jan 8, 2011
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Some interesting New Year resolutions, from Dr. Olomi

  Nimekuwa nafuatilia jinsi desturi ya kuchangia na kufanya sherehe kubwa inavyozidi kushika kasi, ikipelekea ule wigo wa kuomba michango kupanuka kiasi kwamba sasa hata mtu ambaye jina lako halijui vizuri anaweza kukuomba mchango.

  Aidha michango na sherehe hizi zimekuwa mzigo mkubwa sana kwa baadhi ya watu, ikiwa ni pamoja na wale wenye kipato kidogo wanaochangiwa na kulazimika kulipa michango hiyo kwa miaka mingi. Je, wajua kuwa kuna familia ambazo zimefikia kulazimisha ndugu wauze mashamba au mifugo mtaji ili kupata fedha za kuchangia sherehe?.

  Je, wajua kuwa kuna watu ambao zaidi ya nusu ya kipato chao wanatumia kuchangia sherehe na huku wakishindwa kulipia huduma muhimu kama shule, matibabu, lishe, nk. Na kuwa wakati mwingine wewe au mimi (au wengine kama mimi na wewe) ndio wenyeviti na makatibu wa sherehe hiyo?. Na ni sisi tunaoona fahari ya kutumia milioni 30 au zaidi kwenye sherehe usiku mmoja?

  Kuna kijana mmoja jamaa yetu juzi juzi alipata shule Australia akawa anatafuta mchango wa dola 5,000 aende. Alipata 2,000 na amwekwama kwenda. Mwaka kesho akisema anaoa tutamchangia milioni 15-20!!!. Hii si hadithi, ni ukweli, na ni kielelezo cha ulimbukeni tuliofikia.

  Siku za karibuni nimetambua kuwa kuna kundi kubwa tu linasikitishwa na huu mwenendo, na hata kutambua kuwa tunaweza kuwa tunaandikiwa dhambi kubwa (na hukumu yatusubiri) kwa jinsi wengi wetu tunashindwa kusaidia mambo ya msingi lakini tunakuwa wepesi kutoa kwenye sherehe. Wengi wanaamini kuwa tumeshatumbukia kwenye lindi la mazoea ambapo hatuwezi kujitoa mpaka upepo uje ubadilike wenyewe!.

  Mimi nafikiri wasomi tuna jukumu muhimu la kuwa chachu ya mabadiliko pale ambapo mazoea yenye madhara yanavuka mipaka na kuweza hata kuwa chanzo cha ufukara na kuviza maendeleo.

  Ili kubadilisha hili jambo, lazima tuanzie mahali. Mimi napendeleza na kuanza kutekeleza. Kuanzia Januari 2011, nitapunguza michango ninayotoa. Nitatoa tu kwa mtu wa karibu sana , na nitachanga kidogo. Usishangae nikakuchangia 20,000/= kama ulitegemea 50,000/= kwa mfano. Kuanzia July 2011, nitaacha kabisa kuchangia sherehe. Badala yake nitakuwa nachangia elimu pale ambapo mzazi hayupo au mhusika kweli hana uwezo na pia nitachangia miradi mingine ya jamii na maendeleo.

  Je waniunga mkono? Kama ndiyo sambaza huu ujumbe kwa mtandao wako.

  Dr. D.R.Olomi
  Box 35036 Dar es Salaam, Tanzania

   
 2. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #2
  Jan 8, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,318
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  Hulka ya waTZ hiyo...ngoma,harusi,kipaimara na msiba!
  Waaambie wachangie ada ama matibabu ya mgonjwa...utabaki peke yako!
   
 3. Kabembe

  Kabembe JF-Expert Member

  #3
  Jan 8, 2011
  Joined: Feb 11, 2009
  Messages: 2,236
  Likes Received: 928
  Trophy Points: 280
  Kwakweli mkuu naichukia sana tabia hii ya kishamba na iliyojaa ubinafsi,hatuwezi kusaidiana gharama za matibabu au School fees bali tumekazania mambo ya kipuuzi tu
   
 4. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #4
  Jan 8, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,318
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  kama unafanya kazi kwenye institution yenye employees wengi unaweza kupata hadi kadi 5 kwa mwezi..worse enough zina minimum contribution amount!!
   
 5. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #5
  Jan 8, 2011
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,519
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Mie nilishaacha kuchangia harusi ambazo wahusika wake wako too remote na mimi.
   
 6. Kiraka

  Kiraka JF-Expert Member

  #6
  Jan 8, 2011
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 2,551
  Likes Received: 613
  Trophy Points: 280
  Acha tu mimi ofisini kila mwezi hazipungui kadi mbili, acha mtaani yaani imekuwa kama ugonjwa na unakuta kwa kuwa watu wamechangishwa sana basi sasa imekuwa kama kukomoana maana mtu hata harusi ya mbali analeta kadi, acha za ujenzi wa makanisa etc. Yaani imekuwa kama mashindano ya kuchangisha michango.
  Hamna hata mmoja anataka mchango wa ada!
  Mi namuunga mkono Dr Olomi.
   
 7. m

  mbongopopo JF-Expert Member

  #7
  Jan 9, 2011
  Joined: Jan 24, 2008
  Messages: 1,112
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  hii story niliisoma Global publisher


  ok hili jambo wengine wanakaa na umasikini wao baada ya harusi kubwa kufanyiwa
   
 8. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #8
  Jan 9, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Tumezoea utegemezi ndio maana kila kitu tunataka tusaidiwe.
  Halafu kutokujiamini pia kunachangia.
  Kama unaamua kutochanga unatakiwa kuwa na msimamo.
  Sio bibi humchangii babu unamchangia.
   
 9. 22nd

  22nd JF-Expert Member

  #9
  Jan 9, 2011
  Joined: Aug 1, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  uncle wangu anaoa mwezi wanne, mke wa pili,mke wa kwanza amemuacha miezi mitatu iliyopita,ana watoto wanne,hana kazi ya maana,watoto wanaenda na kandambili shule na sometimes wanandugu tukiwa na majukumu mengine ya kifamilia basi watoto watakaa nyumbani kwa kukosa ada.
  ameniomba mchango wa harusi nimegoma kutoa,yaani nimeumia mpaka basi,baba anaomba mchango wa kuoa wakati watoto wanaenda shule ****** wazi.hapa nimenuniwa.
   
 10. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #10
  Jan 9, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ujuha! ulimbukeni
   
 11. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #11
  Jan 9, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Utakuta mtu anaugua hela ya matibabu shida na hata dawa akiandikiwa hamna wa kumsaidia,akija kufa angalia michango ya mazishi itakavyo miminika hata mara kumi ya kiasi ambacho kingemsaidia matibabu na labda kupona kabisa inasikitisha TUBADILIKE!
   
 12. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #12
  Jan 9, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Mabadilio ya kweli yataletwa na mimi nawewe! tuamke tuseme michango ya harusi basi.
   
 13. m

  mzeelapa JF-Expert Member

  #13
  Jan 9, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 1,034
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Wabongo yunapenda ufahari sana wakati tupo katikati ya umaskini. Sehemu muhimu katika harusi ni kanisani lakini mijitu haihudhurii kanisani (kushuhudia ndoa na kusali kuombea wanandoa waishi kwa amani, upendo...), inakwenda kwenye tafrija kisa kunywaaaaaa, kuangalia nani kapendeza, MC nani, ukumbi umependezaje nk
  .
  Wengi ninaowafahamu ambao sherehe zao za harusi zilikuwa za kifahari sana,ndoa zao zimeparaganyika au hazina amani, hii ni laana!!!! fedha zao zingeelekezwa kwa wahitaja kama yatima, wagonjwa,masikini, nk.

  Mie hatua ya kwanza nimeshaacha kuchangia sherehe za wenye uwezo mkubwa, nisiowafahamu personally na walio mbali nami.

  Kama tunaiga mambo ya magharibi mbona sijasikia wao wakichangishana??? Wao Kila mtu anafanya sherehe kufuatana na uwezo wake. kikubwa ni kuhalalisha na kupata baraka za Mungu.
  Hebu fikiria hawa wanaotaka kuoana wanafanyiwa, Kitchen party, Sendoff, Buggy party, Reception, sherehe za kijadi nyumbali nk alimradi fedha inachezewa.....:banplease:
   
Loading...