Intaneti, Siasa na Uchaguzi Tanzania: Fursa, Changamoto na Mustakabali wa Demokrasia ya Kidijitali

Intaneti, Siasa na Uchaguzi Tanzania: Fursa, Changamoto na Mustakabali wa Demokrasia ya Kidijitali

Nchachali

New Member
Joined
Nov 29, 2025
Posts
3
Reaction score
2
Nafasi ya Intaneti katika Siasa za Kisasa
Katika karne ya 21, intaneti imekuwa mhimili muhimuwa siasa za kisasa. Nchini Tanzania, hasa wakati waUchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, intaneti ilijitokezakama nyenzo kuu ya upatikanaji wa taarifa, kampeni za kisiasa, ushiriki wa wananchi na uwajibikaji waviongozi.

Hata hivyo, pamoja na fursa hizo, ilibeba pia changamoto nzito ikiwemo kuenea kwa taarifa potofu, propaganda za kisiasa na hatimaye kuzimwa kwamtandao Agosti 29, 2025, tukio lililoibua mjadalampana kuhusu mustakabali wa demokrasia ya kidijitalinchini.

Intaneti kama Jukwaa la Kampeni na Ushiriki wa Wananchi
Kwa mara ya kwanza kwa kiwango kikubwa, mitandaoya kijamii kama Facebook, X (zamani Twitter), Instagram na WhatsApp ilitumika kama majukwaa yamoja kwa moja ya kampeni na mawasiliano kati yawanasiasa na wapiga kura.

Mwanachama mwandamizi wa CHADEMA, Patrick Sosopi, anasema intaneti imeondoa mipaka yamawasiliano ya kisiasa.

“Kwa dunia ya leo, intaneti si starehe tena bali nihuduma muhimu sana ya mawasiliano, Wakati wakampeni, si kila mtu anaweza kufika kwenye mikutanoya hadhara au kuangalia televisheni mubashara, lakinikupitia intaneti anaweza kufuatilia hata baadaye,” amesema Sosopi.

Ameongeza kuwa uzoefu wake wa kugombea ubungemwaka 2015 na 2020 ulimthibitishia kuwa mitandao yakijamii ni nyenzo muhimu ya kujitangaza, kujengauelewa wa kisiasa na kuwafikia wapiga kura kwaurahisi.

Taarifa Potofu na Juhudi za Kuzidhibiti
Pamoja na faida hizo, intaneti imekuwa pia chanzokikubwa cha taarifa potofu, Kwa mujibu wa Mkuu waIdara ya JamiiCheck kutoka Taasisi ya JamiiAfrica, Innocent Mangu, taarifa potofu zinazohusiana nauchaguzi ndizo zilizoongoza kwa mwaka 2025.

“Tulibaini jumla ya madai 289 ya taarifa potofuzinazohusiana na uchaguzi, zikiwemo kauli za uongokuhusu taratibu za uchaguzi, matokeo ya kubuniwa napicha au video zilizohaririwa,” amesema Mangu.

Ameeleza kuwa vyama vya upinzani vilikuwawalengwa wakuu kwa asilimia 43, huku madaimengine yakilenga viongozi wa dini, chama tawala, Rais na masuala ya kijamii na kiutawala.

Majukwaa ya Mtandaoni: Chanzo cha Tatizo naSuluhisho
Takwimu za JamiiCheck zinaonesha kuwa Facebook, X, WhatsApp na Instagram yalikuwa majukwaayaliyobainika zaidi kusambaza taarifa potofu,

Hata hivyo, Mangu anasisitiza kuwa majukwaa hayohayo yalitumika pia kama nyenzo ya kusahihishataarifa za uongo.

“Mitandao ya kijamii haikuwa tu chanzo cha taarifapotofu, bali pia ilikuwa silaha muhimu ya fact-checking, utoaji wa ufafanuzi na kusambaza taarifasahihi kwa wananchi,” amesema.

Kuzimwa kwa Mtandao Agosti 29, 2025: Athari naMjadala wa Kitaifa
Hatua ya kuzimwa kwa intaneti wakati wa uchaguziimeelezwa na wadau wengi kuwa pigo kwademokrasia, Mdau wa haki za kidijitali na uhuru wakujieleza, Imani Luvanga, anasema kuzimwa kwamtandao kulikiuka haki za msingi za raia.

“Kuzimwa kwa intaneti kuliathiri uhuru wa kujieleza, haki ya kupata na kutoa taarifa, na kuminya uhuru wavyombo vya habari, Uchaguzi ulifanyika gizani,” amesema Luvanga.

Ameeleza kuwa raia walinyimwa fursa ya kupatataarifa kupitia njia mbalimbali, waandishi wa habariwalikosa uhuru wa kufanya kazi zao, na Tanzania ilionekana kutengwa na dunia ya nje.

“Tuliona maandamano, lakini dunia haikuyaona, Hata wananchi wenyewe walikuwa kama wametengwa nadunia,” ameongeza.

Athari za Kiuchumi na Kijamii
Mbali na demokrasia, kuzimwa kwa mtandao kuliathiripia uchumi na maisha ya kila siku ya wananchi.

“Watu walishindwa kufanya biashara, kuwasiliana nandugu zao, na kutumia huduma za kidijitali kama TRA na BRELA. Uchumi uliathirika kwa kiasi kikubwa,” amesema Luvanga.

VPN na Mbinu za Wananchi Kupenya Vizuizi
Baada ya kuzimwa kwa mtandao, baadhi ya wananchi waligeukia matumizi ya VPN kama njia mbadala yakuendelea kuwasiliana, Hatua hii ilionesha kuwa katikaulimwengu wa kidijitali, taarifa haziwezi kuzuiwakabisa.

“Katika dunia ya kidijitali huwezi kuzuia taarifa, unaweza tu kuichelewesha, Mara nyingi kuzimamtandao huongeza wimbi la uvumi na taarifa potofu,” anasema Luvanga.

Uwajibikaji wa Viongozi na Sauti za Wananchi Mtandaoni

Kwa mujibu wa Sosopi, mitandao ya kijamiiimeongeza uwajibikaji kwa viongozi wa umma.

“Leo picha au video ikisambaa ikionesha kiongoziamekiuka maadili au kuna ukatili, hatua huchukuliwaharaka, Mitandao imesaidia viongozi kubainichangamoto ambazo wasingeweza kuziona kwa ziaraza kawaida,” amesema.

Vijana nao wamekuwa mstari wa mbele kutumiamitandao kutoa maoni yao ya kisiasa. Kijana mmoja amesema: “Mitandao imenipa nafasi ya kutoa maoni kuhusuuchaguzi na changamoto za jamii yangu, lakinikuzimwa kwa mtandao kuliniathiri kiuchumi na hatakisaikolojia.”

Intaneti na Mabadiliko ya Uandishi wa Habari za Siasa
Mwandishi wa habari za siasa kutoka chombo cha habari cha kitaifa anasema intaneti imebadilisha kwakiasi kikubwa kazi ya uandishi wa habari.

“Leo mwandishi anapata taarifa kwa haraka kupitiatovuti na mitandao ya kijamii, lakini pia anakabiliwana wimbi la taarifa potofu, hivyo analazimika kufanyauhakiki wa kina zaidi,” amesema.

Ameongeza kuwa intaneti imeongeza kasi ya habari, mwingiliano na wananchi, matumizi ya data journalism, lakini pia shinikizo linalohitaji maadili naweledi wa juu zaidi.

Hitimisho: Mustakabali wa Demokrasia yaKidijitali Tanzania

Uchaguzi Mkuu wa 2025 umeonesha wazi kuwaintaneti ni mhimili muhimu wa demokrasia ya kisasanchini Tanzania, Imetoa fursa za ushiriki wa wananchi, uwajibikaji wa viongozi na upatikanaji wa taarifa, lakini pia imeibua changamoto nzito zinazohitajimjadala mpana wa kitaifa.

Kama anavyosisitiza Imani Luvanga:
“Hakuna demokrasia bila haki na uhuru, Kama tumeamua kutumia demokrasia, basi misingi yakelazima iheshimiwe.”

Mustakabali wa demokrasia ya kidijitali Tanzania utategemea uwezo wa Taifa kulinda uhuru wamtandao, kupambana na taarifa potofu kwa njia za wazi na shirikishi, na kuhakikisha intaneti inabakikuwa daraja la kuunganisha wananchi na demokrasia, si kizuizi chake.
 
Back
Top Bottom