Wamiliki wa Mtandao wa kijamii wa Instagram wameanza rasmi kutekeleza sheria ya kufuta picha za uchi/nusu uchi. Tayari baadhi ya masuper star wamefuta account zao akiwemo Rihana ambaye amejiondoa baada ya picha zake kufutwa. Mkurugenzi Mtendaji wa Instagram Kevin Systrom akiongea na BBC amesema wanataka Instagram wanataka iwe sehemu salama kwa watu wote wakiwemo watoto na watu wenye heshima zao, na hawatajali hata kama baadhi ya watu watajiondoa kwenye mtandao huo.