Instagram yafuta picha za Uchi

Instagram yafuta picha za Uchi

Mtamile

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2011
Posts
2,838
Reaction score
1,274
140603111051_kevin_systrom_getty_304x171_getty_nocredit.jpg

Kevin Systrom afisaa mkuu mtendaji wa Instagram

Mmoja wa waasisi wa mtandao wa kijamii wa Instagram, ameambia BBC kuwa sheria zake kuhusu picha za uchi hazimbagui mtu yeyote.
Kampuni hiyo imekosolewa vikali kwa kwa kuondoa picha za wanawake walio nusu uchi kwenye mtandao huo.

Lakini Afisaa mkuu mtendaji wa mtandao huo wa kijamii, Kevin Systrom, amesema kuwa sheria hizo zinalenga kuhakikisha kuwa vijana na watu wazima wanaotumia mtandao huo wako salama.

Masharti ya matumizi ya mtandao wenyewe, yanasema: 'Mtu haruhusiwi kuweka picha za watu walio nusu uchi na picha zenye mada ya ngono. ''
Matamshi yake yanakuja baada ya mwanawe muigizaji maarufu, Bruce Willis, Scout Willis kuweka picha yake kwenye mtandao huo akiwa nusu uchi bila kitu kifuani.

Picha hiyo iliondolewa kwenye mtandao huo na wamiliki wa mtandao na hapo ndipo malalamiko yalianza kuibuka.

Muimbaji Rihanna, ambaye alikuwa na wafuasi milioni 1.3 aliunga mkono kampeini hiyo kabla ya kufunga akaunti yake.
Wamiliki wa mtandao huo wanasema sheria zinapaswa kufuatwa na kila mtu awe mtu mashuhuri au vinginevyo.

"lengo letu ni kuhakikisha kuwa Instagram, ni mahala salama kwa kila mtu , awe maarufu au la. ''
"tunapaswa kuwa na sheria na kuhakikisha kuwa kila mtu anafuata sheria hizo. Bila shaka tunapata changamoto nyingi lakini tutnaedneklea kusisitiza umuhimu wa sheria kufuatwa, '' alisema Systrom
140603095804_instagram_logo_304x171_afp_nocredit.jpg

Huku umaarufu wa mtandao huo ukiendelea kuimarika, mtandao huo umekosolewa kuhusiana na baadhi ya picha zinazochapishwa humo . Pia mtandao wenye umebana baadhi ya maneno yanayohusiana na madawa ya kulevya.
Instagram ilinunuliwa na Facebook mwaka 2012
.

Chanzo: BBC
 
Safi sana mwanzo mzuri...
 
Wamiliki wa Mtandao wa kijamii wa Instagram wameanza rasmi kutekeleza sheria ya kufuta picha za uchi/nusu uchi. Tayari baadhi ya masuper star wamefuta account zao akiwemo Rihana ambaye amejiondoa baada ya picha zake kufutwa. Mkurugenzi Mtendaji wa Instagram Kevin Systrom akiongea na BBC amesema wanataka Instagram wanataka iwe sehemu salama kwa watu wote wakiwemo watoto na watu wenye heshima zao, na hawatajali hata kama baadhi ya watu watajiondoa kwenye mtandao huo.
 
imetulia, naweza kushawishika kufungua Akaunt kwenu
 
Wale wa kuonyesha makalio imekula kwao
 
safi sana no shobo na mtu,walianza kumzingua Rihanna sahivi wamefatia wengine
 
picha za ngono zina athari gani kwani?
 
ni idea nzuri. Insta imegeuzwa kijiwe cha wahuni
 
Back
Top Bottom