“Injili na msahafu” wa siasa kadiri ya Dk John Magufuli

Hii ndiyo "injili na msahafu" wa siasa tunayoisikia ikienezwa na John Pombe Magufuli na serikali yake, kwamba wafanyakazi wa umma wanaifilisi nchi huku wanasiasa wakiwa ni malaika wa kuwaletea maendeleo wananchi. Injili hiyo inasisitiza kuwa ili Tanzania iendelee lazima wanasiasa wawashikishe adabu wafanyakazi wa umma kwa sababu wanasiasa wanaeneza injili na msahafu usio na doa. Injili na msahafu huu unapigiwa upatu kuwa ndio wa kweli na hakuna ukweli zaidi ya injili na msahafu huo.

Wafanyakazi wengi wa umma wanafukuzwa kazi na wanasiasa ambao wamejigeuza kuwa ndio rejea ya ukweli kuhusu utaratibu wa kazi. Sheria za kazi hazifanyi kazi badala yake maamuzi ya wanasiasa ndiyo yamegeuka kuwa sheria za kazi. Wanawaweka wafanyakazi wa umma rumande kwa sababu ndivyo injili inayotakiwa kuaminiwa na kufuatwa na wananchi wa nchi hii. Wengi tu, na cha kushangaza hata wabeba maboksi wazee ambao ni “wazalendo” wa nchi yetu nao wameshabatizwa na kusilimu na wameshaokoka, kuiamni na sasa wanaitangaza injili na msahafu huu wa serikali ya Magufuli.

Kwa wengine, na wala si wachache injili na msahafu wa Magufuli hauna ukweli wowote. Nchi yetu imefikishwa hapa ilipo na wanasiasa. Injili na msahafu wa kweli ni kuwa wanasiasa ndiyo walioifilisi nchi hii. Nyumba za serikali ziliuzwa na wafanyakazi wa umma kwa maelekezo ya wanasiasa huku John Pombe Magufuli akisimamia zoezi hilo baya. Wanyama waliohai wakiwemo twiga wamepakiwa kwenye ndege kwenda nje ya nchi na wafanyakazi wa umma kwa maelekezo ya wanasiasa. Ufisadi wa aina mbalimbali katika mikataba ikiwemo Escrow, Richmond, EPA n.k yote imefanyika kwa maelekezo ya wanasiasa. Mikata 19 imesainiwa kwa siku moja gizani (bila Bunge kujua) imefanyika kwa matakwa ya wanasiasa. Uharamia na wizi mkubwa katika nchi hii unafanyika kwa maelekezo na kusimamiwa na wanasiasa. Watendaji wa umma wakijaribu kuzuia mambo ya aina hii wanaishia kufukuzwa kazi.

Hivi, mawaziri mfano yule wa awamu iliyopita wa maliasili anausafi gani wa kupata uhalali wa kuwafukuza wale waliokuwa watendaji wa serikali? Kwa ujumla ni kuwa Tanzania ni maskini kwa sababu ya wanasiasa, siyo watendaji wa umma. Hii ndiyo injili na msahafu sahihi unaotakiwa kuaminiwa na kutangazwa ndani na nje ta Tanzania. Kule Zanzibar yule mwenyekiti mzee kabisa wa tume amepindua matokeo halali ya uchaguzi wa Zanzibar kwa maelekezo ya wanasiasa. Yule mwenyekiti ni mtendaji na hawezi kupata nguvu ya kupindua matokeo ya uchaguzi halali bila maelekezo ya wanasiasa. Sasa injili na msahafu wa kweli ni kwamba tukiwachia wanasiasa kueneza injili na msahafu wao wa uwongo tutaendelea kuumia kama nchi.

Kinachotakiwa ni wanasiasa waanze kutumbuana majibu wenyewe kwa wenyewe. Na kama wakishindwa kutumbuana wenyewe kwa wenyewe ni jukumu la sisi wananchi kuwatumbua majibu hawa wanasiasa. Sasa hivi hawataki kukosolewa na wanaendeleza vitisho. Wameanza kufungia magazeti na kupeleka mahakamani wananchi. Tusiwaendelekeze hawa wanasiasa, tuikatae injili na msahafu wao na mambo yake yote. Wanasiasa ndiyo majipu makubwa na wananchi tuyatumbue kwa kusimamia ukweli huu.
nakubaliana na wewe kwa mfano hili suala la Elimu bure alikuandaliwa vizuri kila kunapofanyika kikao cha shule waalimu na wazazi wanaona mapungufu mengi kwa elimu ya watoto wao lakini kila mmoja anaogopa kutoa mawazo ya kuboresha kwa kuhofu kwamba akitoa mawazo tofauti na Makufuli atafukuzwa kazi au kuandamwa. kwa kifupi serikali hii inataka kusifiwa tu,haitaki kukosolewa sasa tunaanza kumkumbuka Kikwete
 
Hao watumishi unao watetea nao ni wabadhirifu wa kutisha,hebu jaribu kufanya utafiti kwenye halmashauri uone rushwa ilivyo tawala angalia utajiri walionao wakuu wa idara mbali mbali.Mwizi ni mwizi haijalishi ametumwa ametumiwa,ameiba kidogo au ameiba kikubwa.Naona wabadhilifu taratibu wanaanza kupata watetezi.Magufuli fukuza hayo majambazi huku kwenye halmashauri pameanza kupumua,.
 
Donald Trump yule mgombea uraisi kule marekani ndio suluhisho la yote haya.
Mtu kama nape na mwigulu eti wao ndio wakufukuza watu kazi..!
Kweli only in Tanzania. Alafu wanahubiri eti nchi inayoheshimu na kifuata sheria pamoja na haki za binadamu.magu mwenyewe jipu sijui anakua vipi leo eti ni msafi anaeona machafu ya wengine.
Mkuu naona umeisha tumbuliwa unakuja humu jf kulia kulia,ulivyokuwa unaiba haukutushirikisha iweje leo hii yanakukuta haya unaanza kulilia unatafuta huruma ya wananchi.Naona mwigulu na Nape wanakunyima usingizi,Magufuli njoo utumbue jipu linguine huku limeisha iva.
 
Wafanyakazi wa serikali wanaotetewa na mleta mada, wakati wa JK na awamu zilizotangulia wamewatesa sana watu. Wizara ya ardhi ni mfano hai wa uonevu unaosababishwa na watumishi wa serikali, ambao walisomeshwa kwa kutumia kodi ya wananchi.

Watumishi hawa wanaotetewa ndio ambao baadhi yao wamekuwa wakituhumiwa kutengeneza urafiki na matapeli ya ardhi, kiasi cha kusababisha kero kubwa sana.

Mzalendo ambaye ameitumikia nchi hii tangu 1962 anasumbuliwa na watu wa ardhi kwa miaka zaidi ya 24, ananyimwa hati ya kiwanja chake cha mbezi beach. Vipi kuhusiana na haki za wananchi ambao hawakuweza kupata elimu kubwa ya darasani. Vipi kuhusiana na haki za watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali?, mzee mstaafu aliyefanya kazi kwa uaminifu kwa muda wote anakuja kunyanyaswa na vijana ambao kiumri ni watoto na wajukuu zake.

Muafrika akipata makalio yake hulia mbwata, nadhani mleta mada anaufahamu msemo huo wa miaka mingi.
 
Ninahakika kuna baadhi ya viuongozi wa siasa na serikali ya TZ tena ngazi za juu tu, wakienda nchi nyingine hata kazi ya kufagia hawawezi pata.
 
Back
Top Bottom