Ingekuwa Wewe Ungefanyaje?

La Quica

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2017
Posts
1,335
Reaction score
3,140
House girl alitandika kitanda cha bosi wake Kama Sehemu ya jukumu lake la kila siku.

Alipomaliza akakitazama sana kile kitanda cha bosi wake akasema naweza kufa bure bila ya kulalia kitanda kama hiki akasema ngoja nijaribu kulala lau kidogo, akavua nguo zote akaziweka chini akabaki na gagulo tu akawasha AC akajifunika blanket gubigubi akalala.

Kwa bahati mbaya usingizi
ukampitia kweli akalala fofofo.
Ghafla Mume wa boss akarudi na haikuwa kawaida yake kurudi Muda huo. alipoingia chumbani akajua hakika huyu ni mke wangu na kwakuwa jana tulikwaruzana atakuwa amekasirika tu. Akaogopa
kumwamsha, mwanamme akasaula akabaki na msuli nae akajifunika hilohilo blanket kwa taratibu sana kwa hofu ya kumwamsha mke wake.


Kwa bahati mbaya naye usingizi ukampitia akalala fofofo. Boss (mke ) aliporudi akaingia chumbani akakuta watu wawili wamelala fofofo akafunua blanket kwa nguvu akawakuta wote wawili yaani yule mfanya kazi na mume wake wamelala pamoja walipoulizwa kila mtu akaeleza ukweli wake.


1.Je, kama wewe ungekuwa ndiyo yule Mke wa
bosi ungewaelewa?

2.Je Kama Wewe ungekuwa ndiyo yule mfanyakazi
ungejitetea vipi?

3. Je, Wewe ungekuwa ndiyo yule bosi ungejitetea
Vipi???

4.Je hapo Ugomvi itakuwa umesababishwa nani?
Mke,mume au mfanyakazi??
 
namalizia kusomba korosho , ntakujbu nikitoka mtwara.
 
Reactions: y-n
Mi napita tuuu mkuu..... Subir wenye majib wanakuja
 
Ngoja waje
 
hadithi haina mshiko, maana ukiishi na mtu kwa muda mrefu lazima tu utafahamu uwepo wake hata gizani. Huyo aliyeshindwa kutambua mke wake kisa kajifunika na blanket anazingua
 
Kwa hiyo hata story za kutunga nazo unataka zitolewe majibu? Huoni kuwa huko ni kusumbuana bila sababu?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…