jikuTech
JF-Expert Member
- Apr 9, 2023
- 228
- 290
UFAHAMU KUHUSIANA NA SOFTWARE NA HARDWARE (KOMPYUTA SYSTEMS).
Unapo zungumzia kompyuta kuachana na tafsiri yake halisi ina mifumo miwili mifumo ambayo ni software na hardware mifumo ambayo inawezesha utendaji wa kompyuta kwa ufanisiVifaa vyote vya kushikika kwenye Kompyuta (physical components) huitwa HardwareMkusanyiko wa programs tendaji mbalimbali zinazo toa amri jinsi gani hardware ifanye kazi kwa kufuata maelekezo maalum huitwa Software
Programu/Software.
Seti ya maagizo ambayo huambia vifaa vya kompyuta(Hardware) nini cha kufanya inajulikana kama programu za kompyuta (Kompyuta Software). Programu hii au mkusanyiko wa programu kama hizo hujulikana kama programu za kompyuta.
Kwa ufupi kompyuta software ni kama akili bandia softwares hutoa maelekezo kulingana na utaratibu au utendaji ulio kusudiwa na mtengenezaji wa hiyo software kwa ajili ya kutatua matatizo au tatizo flani katika ulimwengu halisi au jambo lake binafsi.
Aina za software.
Kwenye Kompyuta software zipo za aina mbili ambazo niSoftware Endeshi (System Software)
Software Tendaji (Application Software)
Software tendaji huwa na zana mbalimbali kwa ajili ya utendaji rafiki kwa mtumiaji kulingana na kazi anayo ifanya. Mfano wa Software tendaji ni kama
Microsoft Office
Google chrome
Virtual dj studio
Games
Software Endeshi hii ni mifumo endeshi ya Kompyuta ambapo ili Kompyuta ifanye kazi lazima iwe na mfumo endeshi mfano wa mfumo endeshi wa kompyuta ni kama
Microsoft Windows
Linux
Mac n.k
Mifumo hii imeundwa ili kuwezesha utendaji fanisi kwa mifumo tendaji {software application} software tendaji inafanya kazi kwenye kompyuta yoyote au kwenye kifaa chochote kutegemeana na uwepo wa software endedhi katika kifaa hicho.
Mfumo endeshi pia kazi yake kubwa huwa ni kufanya muunganiko wa vifaa vya hardware kwenye kompyuta na kuendesha au kuwezesha ufanyaji kazi wa software zingine kwenye kompyuta. View 08
Bonyeza HAPA Ingia kwenye mafunzo haya, Ujifunze moja kwa moja