Information Technology(IT-TEHAMA)-02

Information Technology(IT-TEHAMA)-02

jikuTech

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2023
Posts
228
Reaction score
290

JINSI YA KUPATA ELIMU YA MAMBO MBALIMBALI KUPITIA DIGITALI YA TEHAMA



Jiku Tech Tips itakufundisha njia za kutokana na wewe. Njia za kutokana na wewe hapa maana yake kama unavyofahamu kila mtu ana uwezo wake wa pekee ambao ikiwa itakuwepo taarifa moja na watu wawili basi matumizi ya taarifa hiyo kwa manufaa flani hayawezi kulingana kati ya hao watu wawili.

Kama ilivyo watu wawili wanaweza kusoma kitabu kimoja, darasa moja wakati mmoja, wakafanya mtihani mmoja matokeo yao hayawezi kufanana.

Vilevile ilikufanya au kutumia jambo ambalo haujaligundua wewe kwa umahili na usahihi basi inabidi ujifunze, Swali Je utajifunza wapi??? Mfano kuna wakulima wengi sana lakini wapo wanaopata manufaa makubwa, manufaa ya kati na wanao nufaika kidogo na kilimo chao. Hata katika mambo mengine wapo wanao nufaika sana, kati na kidogo.

Ili ufanye au utumie jambo kwa usahihi wa kunufaika sana ikiwa haujaligundua wewe inakulazimu ujifunze kwa anayefanya au anayetumia kwa usahihi ule wa kunufaika sana. Inakufaa ama umfuate mgunduzi au mtu mwenye namna za kufanya au kutumia akufundishe kwa ajili ya wewe kuwa mahili katika hilo jambo.

Mfano ikiwa haujui kusoma lazima umfuate anaejua kusoma akufundishe kwa ajili ya wewe kujua kusoma. Mara nyingi ni Kwenda shule, mara chache kutafuta Mwalimu mtaani.

Mtu utakuwa na amani kujifunza jambo ambalo linatoa kiu yako, na hapo ndio NIA ya kujifunza au angalau kuanza kufuatilia itakuja.

Tukumbushane uelewa mdogo kuhusu nia, nia naweza sema ni malengo anayokuwa nayo mtu baada ya kuelewa jambo flani, kulielewa jambo zaidi ya mambo mengine katika ufahamu wake kwa muda huo na ili mtu kulielewa jambo flani huwa inataka mtu kuwa na Subira angalau muda kidogo wakufuatilia jambo mtu anataka kuelewa.

Ninaposema jambo, kila mtu katika Maisha anakuwa na kitu anacho kipenda kwa mfano kama movie inakuwa na urefu wa kutosha na inabeba maudhui mengi lakini unajikuta unavutiwa na maudhui flani zaidi yam engine yote katika movie.

Mfano: Scene ya mambo ya comedy, Scene ya mambo ya technology na Scene ya kufundisha.

Sasa baada ya kupata ilo jambo Fulani kinachofuata ni kutafuta anayefahamu jambo hilo ili ujifunze kwakuwa utauwa na nia basi itakuwa unajiskia furaha wakati wa kujifunza jambo hilo na kuelewa itakuwa rahisi kwa sababu ya nia katika jambo hilo.

Ikiwa unania na masuala ya Tehama chukua muda kufuatilia hata kama usipo ielewa Jiku Tech Tips.


Kukua kwa sayansi na teknolojia kumefanya sasa hivi kuna vyanzo vya elimu vingi ambavyo ni rasmi na ambavyo sio rasmi ambapo unaweza kupata elimu ya kitu kupitia taasisi au watu ambao sio rasmi lakini wanaweza elimisha jambo. Kwa namna mbili.

  • Kukutana nao moja kwa moja.
  • Kwa kupitia mtandao wa intaneti.
Katika Jiku Tech Tips tutajifunza mambo mengi kwenye mtandao hasa namna unayoweza kupata elimu au taaluma unayo itaka.

Ulimwengu wa teknolojia ni ulimwengu wa taarifa hivyo kwenye mtandao wa intaneti kuna mahali maalum taarifa huwa zinahifadhiwa na watu pindi wanapopata taarifa kamili kuhusu jambo flani kwa ajili na wengine popote ulimwenguni wanapo tafuta kuhusiana na taarifa hiyo waweze kuona kwa kupitia mtandao wa intaneti.

Nitakueleza ni sehemu gani watu wanahifadhi taarifa kwenye mtandao wa intaneti. Mimi nadhani inaeleweka binadamu anapo zaliwa huwa hana kumbukumbu na kumbukumbu huendelea kuhifadhiwa kwenye kichwa chake kadiri anavyo endelea kuishi. Watu nao kadiri wanavyo vumbua taarifa kamili za mambo mbalimbali huendelea kuhifadhi mahali hapo kadiri wanavyo ishi kutoka sehemu mbalimbali za dunia. i.e America , Africa , Asia, Europe

Kutokana na mimi hapa ili uelewe nitasema kwenye mtandao wa intaneti kuna vitu vitatu.

  • Hifadhi: sehemu hii huitwa seva
  • Taarifa: Habari inayo hifadhiwa
  • Mtafutaji: huitwa client kwa lugha ya kitaalamu
Tulejee kidogo kwenye maana ya mtandao wa intaneti, ukiachana na hapa, ongeza ufahamu wako nenda u – google “what is internet” chukua majibu uyatranslate kuja Kiswahili ikiwa hauelewi lugha ya kiingereza kwa ajili ya wewe kuelewa vizuri.

Mtandao wa intaneti ni muunganiko wa kimataifa unaounganisha kompyuta kote ulimwenguni. Kwenye huu muunganiko wa kimataifa wa kompyuta ndio kuna seva,taarifa, na client kama tulivyo eleza hapo awali.

Seva: ni sehemu au ni kompyuta kubwa maalum kwenye mtandao wa intaneti kwa ajili ya kuhifadhi taarifa.

Taarifa: ni Habari au kumbukumbu zinazo hifadhiwa kwenye seva au maelezo.

Client(mteja): ni kompyuta inayo tumiwa na mtu anaye tafuta taarifa kwenye mtandao wa intaneti.

Tumetaja muunganiko wa kompyuta, lakini tukiachana na maana ya kawaida ya kompyuta inayo kuja kwa kutazama kifaa hicho cha kompyuta, kuna maana ya kitaalamu.

Kompyuta ni kifaa chochote kinacho tumia umeme kinacho weza kuchukua taarifa za mtumiaji na kuzichakata chini ya maelezo maalumu na kutoa majibu Pamoja na kuhifadhi majibu hayo kwa ajili ya matumizi ya baadaye.

Hivyo nikisema kompyuta na maanisha vifaa vyenye uwezo huo vyote kama vile Desktop Kompyuta , Laptops , Smartphones na vingine ambavyo sija vitaja hapa.

Tumeeleza kwenye mtandao wa intaneti kwamba ni muunganiko wa kimataifa hivyo kompyuta maalum zinazotunza taarifa huwa zipo maeneo tofauti tofauti duniani ama America, Europe, Asia , Africa.

Ipo miundombinu ya kufurahia mtandao wa intaneti na ili utumie intaneti vizuri kwenye mambo yako unatakiwa kufahamu miundombinu ya kufurahia ulimwengu wa mtandao wa intaneti.

Miundombinu hiyo ni zipo programu ambazo zimetengenezwa ili kukuwezesha wewe kupata taarifa kwenye mtandao wa intaneti.

Programu hizi huitwa vivinjali kikiwa kimoja kivinjali kwa kiingereza (Browsers).

Hauna haja ya kufahamu taarifa unayo itafuta imehifadhiwa mahali gani, teknolojia ya Browsers inatumia injini za utafutaji kupata taarifa yoyote kwenye mtandao wa intaneti inayo endana na kile unacho tafuta na kukuletea kwenye kifaa chako kupitia kivinjari unacho tumia.

Mfano wa kivinjari ni kama​

  • Google Chrome
  • Firefox
  • Edge
  • Safari
  • Opera Mini

Mfano wa injini za utafutaji​

Google search

Microsoft Bing

Yahoo

Yandex

DuckDuckGo (best darkweb browser)

Injini za utafutaji hupatikana na huwa zimewezeshwa automatic kwenye Browser unayotumia wewe na hivyo inakuwa ni kuchagua tu.

Unatakiwa kupata uzoefu wa namna ya kuchuja matokeo yanayo kuja kulingana na wewe na urasmi wa wavuti uliyo ichagua ili kuepuka kupotoka mwenyewe.

Aina mbili za utafutaji wa taarifa kwenye mtandao wa intaneti kupitia browser.​

Moja, utafutaji kwa kutumia kiungo kinacho kupeleka moja wa moja sehemu taarifa ilipo.

Pili, utafutaji kwa kutumia maelezo au maneno yanayo endana na kile unacho kusudia.

Mfano:
Kiungo cha moja kwa moja ni https://www.necta.go.tz hii ni kiungo (link) au (url) au anuani itakayo kupeleka Baraza la Mitihani Tanzania kwenye mtandao wa intaneti moja kwa moja.

Kwa kutumia maneno utaingia kwenye browser yako na kuandika maelezo “Baraza la mitihani Tanzania” au “Necta”.


Zingatia:

Kiungo kwenye browser huandikwa kwenye Address Bar; yaani kwenye box la kujaza anuani ya kile unacho tafuta, yaani ni kama vile umesha ambiwa JUMA flani anaishi mkoa wa Dar es Salaam, Temeke,Mtaa flani block namba 2 nyumba namba 12 maana yake utaenda moja kwa moja na kumpata juma unayemtaka wewe.

Maneno au maelezo kwenye browser huandikwa kwenye Search Box yaani kwenye box la kujaza kile unacho kitafuta kwenye intaneti yaani unakuwa unafahamu tu unachotafuta kwenye mtandao wa intaneti ila haufahamu kipo sehemu gani kwenye mtandao wa intaneti, hauna anuani yake kamili. Kama vile uambiwe mtafute juma flani ambaye unamfahamu ila haujui yuko wapi na utampataje kwa hiyo utakuwa na kazi ya kuwatafuta akina juma kisha kuangalia juma yule unaye mfahamu wewe.

Ndio maana njia ya kiungo (link) itakupeleka moja kwa moja na njia ya maelezo itakuletea matokeo mengi uchague wewe unalotafuta.

Utafutaji wa maelezo au maneno unategemea uzingatie urasmi wa mtoa taarifa utakayo ichagua.

Kama vile ukitafuta Necta utakuta wengi wana taarifa za kuhusu NECTA lakini wewe unatakiwa uchague chanzo ni NECTA.

Hivyo kama mtu anakupa kazi ya kutafuta kitu flani mtandaoni ni vizuri akupe link au kiungo cha moja kwa moja.

Jiku Tech Tips itafafanua mambo mengi ya teknolojia na kama unavyo elewa au kama hauelewi teknolojia ina vitu vingi sana na ni pana.

Turejee kwenye maana ya Teknolojia ili kuelewa kwa nini umekua mdau au kama utavutiwa uwe mdau wa teknolojia kuanzia sasa.

Teknolojia ni matumizi ya maarifa ya kisayansi kuunda zana, mbinu na michakato ambayo husaidia watu kutatua shida, kuboresha maisha yao na kufikia malengo, Inaweza kujumuisha anuwai ya vitu kutoka zana rahisi hadi mifumo migumu kama kompyuta na mtandao wa intaneti.

Hapa Jiku Tech Tips tutajadili zaidi kuhusu teknolojia ya kompyuta kwa ajili ya kujiandaa kuwa wabobevu wa Tehama ya Juu na Namna gani unaweza kunufaika na vipengele mbalimbali kwenye Tehama. View 03

Bonyeza HAPA Ingia kwenye mafunzo haya, Ujifunze moja kwa moja
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom