Inflammatory: CHADEMA hawako kwa maslahi ya taifa, they are just another tool


It is ok, sibaliki wala silazimishi muungano wa cuf na cdm, japo unaweza kuwa na impact in near future.ninachopinga ni sababu inayotolewa na cdm kuwa cuf ni sehemu ya serikali, hii sababu inaidhalilisha chadema yote kuwa still hawajui upinzani ni ideology sio kuwa against!!!!!!!!!!!!!!!
 
you have said so many things without saying anything,...the question is...maalim seif ataweza kwenda against na serikali anayoiongoza,kwa sasa hivi anatekeleza sera za ccm,hawezi kuzicriticize

rudia tena kusoma, soma pot yangu no.36 , upinzani defintion unayoichukua wewe sio , haujui siasa bado...cuf ni cuf, cdm ni cdm, ccm ni ccm, haiwezekani kama una mlengo wa kulia ukageuka kuwa wa kushoto simply kwa sababu unaunda serikali...stick in knowing upinzani i different ideology!!!! mko dunia gani??
 
Very smart Waberoya, huu ndo ukweli ambao watu humu hawapendi kuusikia. Mara kibao nimejaribu kuongea haya, lakini kwa vile watu wa humu wanaongozwa na upepo, wafata mkumbo, tafakari kwao ni mwiko. Mwenye akili na asikie

Are these words comming from you??? unajiaibisha sana, ni bora ukaiondoa hiyo picha ya Michelle, kwani naye asingependa picha yake itumike na watu wenye upeo mdogo ( wa shule za kata) kama huu.
 

Tukumbuke kuwa CUF kwa sasa ni undefined organ; upinzani wanataka,lakini wakati huohuo wao wanaongoza serikali kwa kushirikiana na CCM, linapokuja swala la maamuzi ya kiutawala watakaa na CCM, Kwa upande mwingine linapokuja swala la kuipinga serikali ya CCM wao pia wanataka washirikishwe na CDM.Hili ni janga la kitaifa kuwa na chama cha aina hii.

Hatuwezi kuwaona CUF kama chama cha siasa, kwani hakina tija kwa watanzania.
 

Naona uchu wa uwaziri kivuli umewadanda. Hakuna ulazima wa cuf kuwa kwenye kambi rasmi, kuwepo tu bungeni kwa tiketi ya chama cha upinzani tayari ni upinzani, bado wanataka nini tena? Mtaumia sana mwaka huu.
 
Copy + Cut + Paste + Confusing language/info/x = Inflammatoryx

Pole kwa kazi kubwa uliyofanya - my suggestion for you next time, usitumie sana taarifa za kwenye websites, na hata ukizitumia jaribu kutoa maana unayotaka kutoka katika hizo taarifa ili uweze kujenga hoja kuendana na hali ya vyama na nchi yetu inavyokwenda. Tujaribu ku "contextualise" whatever information we access / receive from other sources. Look at the font type and size...mmm :coffee:.
 
Mimi ningedhani kaka, ungeraribu kujibu kwa ufupi kidogo, maswali yanayotokana na faida za CUF kuwa kwenye kambi rasmi ya upinzani,
CUF kilivyo sasa, au kwa kutoa mfano na chama kingine duniani kilicho na muundo kama wa CUF duniani, yani kimo kwenye serikali iliyo madarakani upande mmoja wa upinzani na kiko kwenye upinzani upande wa muungano, je utaratibu wa kazi wa chama hisho serikalini au kwenye upinzani unakuwaje?
Wengine sie tunajifunzia humu JF, kwa hio tunawategemea sana nyie wataalamu mtueleweshe bila kumung'unya maneno, pia naomba usichoke kutuelewesha kwani kama unavyoona hii ni mada iliopendwa na wengi.
Pia jipe moyo , huwa kuna wanafunzi ambao wanapenda kubishana(kuchallenge) na waalimu wao
 


Waberoya, hakuna anayemlazimisha mwenzake kujibu post yake.
Huu ni mjadala ambao umeuleta na sisi tunawjibika kutoa mawazo yetu, kama hayakupendezi ama hayakubaliani na muono wako inabidi ukubaliane na hali hiyo. Kwani mara ngapi umeleta mijadala hapa na nikai-support? sifanyi hivyo kukufurahisha mazee ninatoa mawazo yangu kama ambavyo na wewe unatoa mawazo yako.Kama ni ushabiki hata wewe ni mshabiki, inawezekana tu kwamba mimi nashabikia yanga na wewe unashabikia simba, kwahiyo hata uhalisia ninaouona basi wewe unauona kwa jicho la ushabiki.

Sasa kiongozi wangu nataka twende hatua kwa hatua; unasema nitofautishe ideology na upinzani, kitu ambacho naamini kwamba ninajua kuvitofautisha, labda unisaidie kukuelewa unatofautishaje upinzani na ideology ili twende pamoja, tena kwa kuzingatia siasa za kitanzania ama kiafrika. Manake hapa unataka tufanye siasa za kimarekanoi wakati sisi ni walewale waafrika watanzania. Wamarekani hawakufika huko waliko kiurahisi, wamepitia hatua kwa hatua, miaka na miaka. Na kama unataka tufanye siasa za kimarekani, je ni kwa cdm kushirikiana na cuf ama kuna issues kubwa za kitaifa zinapaswa kufanywa ili kufikia hilo lengo?

Kwa suala la kama cdm ikishinda tlp inakuwa upinzani liko bayana kabisa. lazima kunakuwepo na chama kinachounda serikali na kunakuwepo na chama/vyama vya upinzani. Sasa kama neno upinzani ndilo linakupa shida basi unaweza kuita chama/vyama mbadala.
 

Ahsante kiongozi,
Nadhani hilo ni swali la muhimu sana waberoya akitusaidia tena kwa mifano kama alivyotutajia nchi zinazounda serikali za mseto na serikali za umoja wa kitaifa huko duniani. Atufahamishe na vyama vinavyoshiriki upande mmoja kuunda serikali za umoja wa kitaifa na kwa upande wa pili vikashirikishwa kuunda kambi rasmi ya upinzani bungeni.
 
Guys in short and let me done in this point, we have a very wrong definition of upinzani!! upinzani kwetu ni to be against na sio kuwa na different ideology ya kuleta maendeleo kwa wananchi nasikitika sana hata Slaa ana mawazo haya!!!! huu nu ujinga wa kupindukia na chadema wameeneza uongo huu kwa wananchi kwa malengo yao wanayoyajua wao wenyewe!!! kama issue ya kuaminiana ni option chama chochote kinaweza kutoaminiwa, regardless kiko kwenye power au la, issue ya serikali ya mseto ni desirable hapa nchini, TUKIWEKA UPINZANI NI TO BE AGAINST THEN WE DONT HAVE IDEOLOGGIES GOVERNNING THIS INSITUTION, namalizia ni haki kabisa cdm kutoungana na cuf, ila sababu isiwe eti cuf ni sehemu ya serikali, hii inaifanya chadema kuwa joke of the century, hii sio sababu hata kidogo.

Pili kwa chadema inayoyapitia sasa na tuhuma zote walizonazo wakae chini na kuangalia metholdogy ya wao kujikoa, propaganda zinaua vyama jamani, hamtaki kunielewa shauri zenu, will recall these posts in near future.
 


Mwanazuoni kama wewe hukutakiwa kuhitimisha mjadala kwa staili hii.

Kwa kiswahili rahisi kabisa inaonekana hilo ni dua la kuku, halimpati mwewe kamanda.

anyway, hayo ni mawazo yako na una haki ya kusema hivyo.
 
Mimi nataka niulize swali moja kwa viongozi wa CUF kama wako huku wanijibu.

CUF na CCM wana sera na mweleko tofauti katika kutimiza mahitji ya wananchi mfani ni kama ifuatavyo:


1. CUF wana sera ya kushughulikia mafisadi ambao wengi wao ni wanachama na viongozi wa CCM, Je katika serikali ya umoja wa kitaifa CUF ina nafasi gani ya kuyatimiza haya?


2. CUF wana sera ya kufutilia mbali mikataba mibovu ya madini, Nishati n.k wakati mikataba hii ndio inayoinufaisha CCM na viongozi wake Je katika serikali ya umoja wa kitaifa CUF wanasimamia wapi?


3. CUF miaka ya nyuma ilikuwepo katika kudai katiba mpya ambayo ndiyo kichaka kikubwa cha maovu ya CCM na Viongozi wao je serikali ya umoja wa kitaifa inasimamia sera gani, ya kuwa na katiba mpya au kuendelea na katiba ya sasa?


NOTE: Kwa muda sasa sijasikia Maalim Seif akizungumzia katiba mpya na ufisadi unaoendelea nchini je ndio kusema amepata alichokuwa anakitafuta au kajiwekea kitanzi? na ninapozungumzia CUF ina maana ni Visiwni na Bara.


Baada majibu haya yatafuata maswali mengine.
 

what is upinzani may be we should start from here!!! siamini kama hauelewi kwa ninavyokufahamu, ideology inahama?? acha kuniaibisha au hukuwahi kufikiria kabla?? anza sasa!
 
Duu wakuu mnajadili mavitu magumu kweli...tatizo hatuwezi kuyasoma sas simnajua tena umeme hakuna
 

Wewe unatoa maana ya upinzani kwa upeo wako, hatujawahi kusikia CCM wanasema watatoa elimu bure CDM au CUF wakasema elimu isiwe bure, hatujawahi kusikia CCM wanaonyesha kwa vitendo kushughulikia mafisadi CUF au CDM wakasema NO.
Vile vile hatuoni kama katika maendeleo tunapiga hatua mbele sasa unataka tusiwe wapinzani wa CCM unataka tufanye nini.

Unasema kuwa Chama kingine ni kuwa na "different ideology ya kuleta maendeleo", kama upinzani wanataka watu wapewe elimu yenye tija kwa maendeleo yao, Chama tawala hakitaki rusults ni nini si ndio kupingana.

Sema unachokitaka usizunguke sana, kama ni unakiunga CCM mkono no hiari yako si kwa kuzunguka zunguka ilimradi tu uwachanganye watu.


Mimi nawaunga mkono wapinzani mpaka mwisho
 
Out of curiousity, hivi haya mainflamatory ndo pia yanasababisha mainflation?
 
Duu! Mkuu, we kiboko, yaani mda huu wote umeshindwa kujibu/kukubali ukweli kuwa hakuna duniani nchi yoyote ambapo chama kwa wakati mmoja kimekuwa/shiriki kuunda serikali na wakati huohuo kikawa nje ya serikali??(sijatumia neno upinzani). Na please tusaidie, umepinga kwenye post zako nyingi Cuf isiitwe ni SEHEMU ya serikali!! hivi huko zanzibar nani ni sehemu ya serikali? Je, ni Ccm pekee???
 
Waberoya,
CUF ni sehemu ya Serikali ya Mapinduzi( Sorry, ya Nchi ya Zanzibar!) ya Zanzibar. Sasa hivi Maalim Seifu ni Makamu wa Kwanza( sio wa pili) wa SERIKALI ile ingawa cheo hiki hakimo kwenye KATIBA yetu ya JMT. Maalim Seif pia ni Katibu Mkuu wa CUF. Mpangilio huu unaidhalilisha CUF sio CHADEMA.
 
good choice of words!
Tatizo moja hapa tunapoongelea mambo ya chama fulani ni rahisi mtu kuwaza zaidi zile personalities, na powers zinazoandamana nazo.
Sijui wenzangu ila ninaposema CDM, CCM, CUF na maana fikra wanazosimamia (walizotuambia na wanazotekeleza) nina maana afya, elimu, uchumi nk, nikisema upinzani nina maana ya sera/mtazamo mbadala wa walio madarakani kwa sasa.
 
what is upinzani may be we should start from here!!! siamini kama hauelewi kwa ninavyokufahamu, ideology inahama?? acha kuniaibisha au hukuwahi kufikiria kabla?? anza sasa!

Mkuu,
Kuna watu hapo juu mmoja wapo stein amekuuliza baadhi ya mambo yanayovitofautisha vyama vya ccm,cuf na cdm labda ujibu ili tupate kukufahamu zaidi.
Lakini pia naona unachanganya kati ya upinzani na uadui, manake hapa tunazungumzia upinzani katika context ya utofauti wa itikadi(ideology) lakini wewe unauzungumzia upinzani katika context ya uadui, hapo hatuwezi kukubaliana kamanda kama tafsiri ya upinzani inakupiga chenga kiasi hicho.
Ni vizuri ukaacha kurukaruka kama layman, wewe ni mwanazuoni majibu na hoja zako ni vizuri yakasimama kwenye hoja. Jaribu kuwa tofauti na kiongozi wangu Mtatiro Julius(samahani wa nyumbani kwa kukutolea mfano).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…