Inflammatory: CHADEMA hawako kwa maslahi ya taifa, they are just another tool

Mzee mwenzangu Weberoya,

Zamani ilikuwa ukitoa hoja jamvini watu wanajadili kwa hoja na mantiki. Siku hizi watu wanajibu kwa ushabiki pasina kuona tatizo liko wapi. Unabishana na watu ambao wamepofuliwa na ushabiki wao wa chama hawatakusikiliza kitu. Au kama wamekusikiliza hawatakuelewa au kukufahamu. Ni vizuri uwaache waendelee na ushabiki wao kwani nina hakika hata Chadema wakipewa nchi leo wanaweza kuwa kama CCM au kuwazidi CCM sasa only few of us tunaweza kuliona hilo na ndio maana narudia tena bora wengine hatuna vyama maana bado vyama vya siasa Tanzania havijakomaa kisiasa.

Endelea kusubiri vikomae
 
Mkuu,

Kwanza wazanzibar na wapemba wako kule Mzalendo.Net maana kule kama hujawa mzanzibari huwi member. Huku sisi ni watanganyika tena born and bread, huna vya kunivua utanganyika wangu. Maandishi yako yanaonyesha wazi umejaa ushabiki na upenzi pasina kupima uzito wa mada husika. Mkae mkijiuliza je Chadema ina majimbo mangapi? na CCM ina majimbo mangapi? Sasa jiulize Chadema itashinda vp mikoa ya Mtwara, Lindi, Morogoro, Tabora, Mafia, Kagera na Pwani na Kigoma (ukimtoa Zitto). Pia yapime vizuri maneno ya Karume kuwa Dar-es-Salaam CCM wamewaazima majimbo yao. Watu wengi mtaani wanaregret kwanini waliwapigia kura Chadema sasa jiulize kwanini? Ukishayapata majibu ndio utafahamu nini nazungumza.

mkuu ... unamaana hii mikoa ni joint stronghold ya sisiem na cuf au...... ? you have justified the cause
 
Umejaribu kuandika kama mwanazuoni. Siku nyingine unapofanya rejea (reference-citing), tumia credible sources (books, journals etc) and dont copy and paste. wikianswer na wikipedia are not deemed 'credible sources' in the academic world.

First this is not academic world! we are in politics
second you are shallow about wikipedia, if you post something there you must put citations, their citation are from books and journals name them...if you dont cite they alert you that this information has no reference!!! du tecknolojia ina kazi sana kupenya!
 
Waberoya said:
Kwa hiyo unakubali kuwa serikali ya mseto is ok! kwa reference ya kigoma na zenj?

wachache wwanajua hilo na ndipo niliposimamia,

Waberoya,

..naomba unisome kwa makini.

..nimesema vyama vililazimika kuunganisha nguvu Zanzibar na Kigoma kwasababu kila kimoja kilishindwa kupata clear majority.

..sasa hivi Chadema wametimiza vigezo vyote vya kuunda kambi ya upinzani bila kuvishirikisha vyama vingine. katika mazingira hayo, can you tell me why Hamad Rashidi anajaribu kuunda kambi nyingine ya upinzani? tena anajaribu mpaka kupata baraka za Spika!!!

NB:

..nina hakika hizo nchi ambazo zimeunda serikali za mseto ni kwasababu hiyo hiyo ya vyama kushindwa kupata a clear majority ktk kura za uchaguzi.
 
Nonda,

..CUF ni chama kilichoanzishwa kwa ajili ya kutetea maslahi ya Wapemba.

..muonekano wao huku Tanganyika ni kukamilisha tu utaratibu wa kisheria kuhusu usajili wa chama cha siasa.

..kama ni kuunda kambi ya upinzani, ieleweke kwamba walishaunda vipindi vilivyopita. suali la kujiuliza ni kuwa CUF walitumia vipi jukwaa hilo?

..sasa hivi wana wabunge wawili tu wa kuchaguliwa huku Tanganyika. does that make any sense to you, ukizingatia kwamba walikuwa chama kikuu cha upinzani bungeni, na kwa kipindi kirefu wamekuwa hawana migogoro ndani ya chama?

..je, mwenzetu unakumbukumbu ya hoja yoyote ile iliyoanzishwa na CUF bungeni kutetea maslahi ya wa-Tanganyika?

..je, ni kitu gani kimebadilika sasa hivi mpaka wa-Tanganyika wawe na imani nao na kuwapa jukumu la kuongoza kambi ya upinzani ktk bunge la muungano[tanganyika]?

..lini umesikia CUF wakijisumbua kuanzisha matawi ktk mikoa na maeneo mbalimbali ya Tanganyika? unafahamu wamekuwa wakipata ruzuku kiasi gani, na wametumia kiasi gani kuweka mtandao huku Tanganyika?

..nakuhakikishia kwamba CUF hawana interest na masuala ya Tanganyika. hata base yao Pemba inapinga muungano kwa nguvu zote. other than kura za wabunge wa CUF bungeni, kambi ya upinzani will not miss anything significant kwa kutokishirikisha chama hicho.
.
Mkuu,
Ni kwa nini umeshikilia msimamo wa kuwa CUF ni chama cha wapemba?cha kutetea wapemba?....Ninavyoelewa CUF imeshinda viti vya ubunge na uwakilishi Pemba, unguja na bara...ingawaje wewe unaona wabunge wawili ni kidogo lakini vyama vyengine vyote ukiondoa CCM hakuna kilichopata Mbunge au mwakilishi hata mmoja Zenj

CUF walipounda kambi ya upinzani waliingiza wabunge kupitia vyama vyengine na hawakung'ang'ania kwamba wao ndio wawe waanzilishi wa hoja inayotetea Tanganyika..kwa hiyo walifanya kosa kuipa CDM platform ya kujitambulisha?

Mkuu,CUF imeweza kushinda ubunge bara bila ya kuwa na matawi? au wanachama?

kama base ya CUF inapinga muungano haina maana CUF kama chama inapinga muungano..hata rasimu sifuri yao inataka muungano wa serikali tatu...sijui kama wewe ni CDM ..lakini unaitetea sana CDM na rai yako ni kuvunja Muungano..jee tuihukumu CDM kwa matakwa yako ya kuukataa muungano?

CUF haijawa na migogoro? Labda umehafilika...Ni kuwa CUF wamekabiliana na migogoro mingi, ni kuwa wamekabiliana nayo vizuri tu...unasahau kuwa chama chochote kinachoinukia lazima CCM inakishughulikia?ikiwa ni pamoja na kupandikiza migogoro?

Mkuu, myonge mnyongeni lakini haki yake apewe...mimi siitetei CUF hapa najua wana madudu yao pia,,ila naona unatoa points zinazopindisha ukweli...wala mimi si mwanachama wa chama chochote cha siasa mkuu..kwa hiyo siongozwi na ushabiki wa kichama.
 
Mdondoaji said:
Hebu tuulizane Chadema imeshinda majimbo gani na mikoa gani?

Mdondoaji,

..CDM wasingekosana na kina Kafulila wangechukua majority ya majimbo ya Kigoma.

..sote tunakubaliana kwamba wakazi wengi wa Kigoma ni Waislamu.

..personally, sidhani kama Udini ulichukua nafasi kubwa ktk uchaguzi huu.

..badala yake naamini FEDHA na INCUMBENCY ndizo zilizoipa CCM ushindi.

NB:

..kwetu bara wananchi hawaulizi dini, bali wanauliza kama umezaliwa ktk eneo lau.

..hakuna Uislamu au Ukristo mkali kama huu wa mjini na kwenye mitandao.

..mikoani kuna Waislamu kibao ambao ni wapika pombe mahiri, pia kuna Wakristo wameoa wake mpaka 9.
 
Nonda said:

..hivi huoni diversity iliyopo ktk wabunge wa CCM au CDM huku Tanganyika.

..kwa mfano CDM wana wabunge toka Arusha,Dar,Kilimanjaro,Kigoma,Rukwa,Mbeya,Iringa,Shinyanga etc.

..kuna mtu alipata kudai kwamba Pemba ni sawa na jimbo la Ubungo!!!!

..kwa msingi huo kuwa makini kidogo unapajaribu kulinganisha EFFORTS na RESOURCES zinazohitajika kufanya siasa huku Tanganyika na huko Pemba waliko CUF.

..hivi unafikiri CDM wakiamua kubanana hapa Dar na wasitoke nje, watashindwa kuzoa viti vyote vya ubunge na udiwani, kama wanavyofanya CUF huko Pemba?

..CUF hawakufanya hisani kuwashirikisha CDM na vyama vingine ktk kambi ya upinzani. kanuni za bunge kuhusu uundwaji wa kambi ya upinzani ndizo zilizolazimisha ushirikiano huo.

..kwa mtizamo wangu CUF wame-enjoy muda mrefu sana wa amani na stability. vilevile wamekuwa wakipata ruzuku kubwa kulinganisha na vyama vingine kama CDM,TLP,UDP,NCCR.

..kinachonishangaza CUF hawakuchukua hatua kujitanua na kuwafikia Watanganyika wengi zaidi. UZEMBE huo wa CUF ndiyo uliosababisha wakapokonywa na CDM nafasi ya kuwa chama kikuu cha upinzani ktk bunge la muungano.

..ndiyo maana naendelea kusisitiza kwamba CUF ni chama cha Pemba. huku Tanganyika wanageresha tu ili kutimiza masharti ya sheria ya usajili wa vyama vya siasa.

..otherwise, were u impressed when CUF led the opposition camp? I was not. kwa hiyo wacha tuwapime CDM.
 
CCM ni chama tawala kinaundwa na Genge la watu wenye nia ya kufilisi nchi na rasilimali yake
Hivi chama(CCM) kinachundwa na Wezi na kuendesha shughuli zake kwa fedha za wizi kina maslahi gani kitaifa?
Richmond
Dowans
Mermeta
Kagoda.
DeepGreen
Mgodi wa Kiwira.
Mikataba ya Kuchimba Madini
Vibali vya kuvua samaki
Kuuza mbuga za Loliondo.
kuuza Eneo la Wahadzabe kule Arusha kwa Sultan Wa Saudia.
Kupokonya mashamba ya wananchi na kuwapa Wageni.
Muungano fake
Katiba Fake
Umalaya na uzinzi sugu( Kikwete& Kikwete)
Matusi ya nguoni(Makamba)
Kuua wananchi kwa kutumia POLISI

Msululu ni mreeefu sana.
Chama kianacho simamia uchafu wote huu maslahi yake ni kitaifa nini?
 
Mdondoaji,

..CDM wasingekosana na kina Kafulila wangechukua majority ya majimbo ya Kigoma.

..sote tunakubaliana kwamba wakazi wengi wa Kigoma ni Waislamu.

..personally, sidhani kama Udini ulichukua nafasi kubwa ktk uchaguzi huu.

..badala yake naamini FEDHA na INCUMBENCY ndizo zilizoipa CCM ushindi.

NB:

..kwetu bara wananchi hawaulizi dini, bali wanauliza kama umezaliwa ktk eneo lau.

..hakuna Uislamu au Ukristo mkali kama huu wa mjini na kwenye mitandao.

..mikoani kuna Waislamu kibao ambao ni wapika pombe mahiri, pia kuna Wakristo wameoa wake mpaka 9.

JK hivyo unasema kuwa Chadema problem ya udini haiwatafuni? basi nimeshindwa mimi ila utafiti wangu mdogo tu nilioufanya unaonyesha udini unawatafuna Chadema kama hawajaligundua basi nawatakia kila la kheri.
 
Sijui kama mwandika hii hoja yuko serious of producing something relevant of solution or any kind of advice here. But he or she has right to his/her opinions.

All examples ametoa hapo juu inaonyesha jinsi gani hajui maana ya coalition government and why people in their countries build these coalition to archive something big. What coalition consists of CUF and Chadema will bring? Kuna tofauti kubwa kati ya CUF na Chadema jinsi ya kupata solutions za matatizo ya Taifa letu na kitu kingine ni jinsi CUF-Hamad kukubali matokeo haraka haraka huko Visiwani. Watanzania hatufahamu sababu zilizo wafanya CUF-Visiwani kujiunga na serikali ya CCM ambayo inaendelea kuiba raslimali za Taifa (Dowans/Richmond) letu kupitia mikataba hewa na wizi wa kura.

Kama huyu mwandikaji hoja hajui kuundwa kwa coalition just for the sake of coalition hakuna maana manufaa endapo CUF wanashirikiana na CCM na wanataka Chadema washirikiane na CUF. What hake is that? CUF-CCM and "CCM-CUF-Chadema" What is this for you? Wananchi tuna uhakika kama CUF wataleta hoja za maana za Watanzania Bungeni au Kitaifa, Chadema wataungana nao kupigania Rights of the People. Wanachama wa CUF don't take Chadema decision personal, these are results of your poor CUF national leadership just that.

One day we will have one coarse and aim but for now things will fall like that....
 
Thread ndefu lakini ungesema na ukweli kidogo basi. Umesahau kuwa CDM walimuunga mkono Prof Lipumba mwaka 2000? Utasemaje eti CDM hawawezi kuunga mkono CUF kwa lolote? Acha hizo. Upinzani sio lazima mtu awe waziri kivuli, jenga hoja tu za kutetea maslahi ya watanzania nasi tutakuhesabu. Kuandika mi-thread mirefu kwa minajili ya kupigia spidi pesa ya kambi ya upinzani bara wakati visiwani unavuta ya serikali ni bure kabisa!

Usisahau hawa wabunge walitumia hela nyingi kupata huu ubunge. Kuna madeni ya kulipa. HELA ZINATAFUTWA ZA KULIPA HAYA MADENI
 
To cut the story short; Waberoya sijakuelewa unaongelea nini... hivi coalition uliyoi-refer hapa ni model ipi hasa?

KWanini basi CUF bara nao wasiingie kwenye serikali kama Zanzibar tuamini kweli hii ni coalition inayomaanisha na si danganya toto?

How did CDM become a center of you patriotism na not CUF ambao tayari bara wana-operate tofauti na zanzibar wakati ni chama kimoja?

Just review your denominator
 
CUF si wapinzani,coz wapo serikalini na wanamakamu wa raisi..na Tanzania ni serikali ya muungano kati ya Tangany... Na Zanzibar.
 
Sijui niko upande gani lakini, sifahami vizuri kazi ya serikali kivuli, kidogo nichofahamu kwa muungano niofahamu sidhani CUF wanatakiwa KUWAZA KUOMBA kushiriki katika serikali hii.
- Maamuzi ya muungano yanayohusu Zanzibar watakaa wapi? manake wako serikalini Zbar na wako upinzani Muungano!!!!
- Muungano wao wa visiwani unawafanya watakiwe kuwepo kati ya mawaziri wa serikali ya muungano? hivyo kuna uwezekano wangekuwamo katika serikali ya Pinda????
 
Acha propaganda, chadema imewaambia cuf kuwa watangaze nini kilichomo katika huo muafaka
 
Waberoya,
Nadhani umeamua kupotosha watu ama hujui ulitendalo.

Sawa, unazungumzia coallition governmemnts, umetoa mifano kwa kutaja nchi mbali mbali zenye kuunda hizo coallition government.Hata tukichukulia mfano wa serikali ya zanzibar na meya wa kigoma 2005-2010 then utaona kwamba hayo mashirikiano yako kwenye upande wa kuunda serikali tu na sio kambi ya upinzani bungeni.

Hizi lawama zako au shutuma dhidi ya cdm kukataa kuungana na cuf kuunda kambi ya upinzani bungeni, naona umepotea njia kiongozi.Nadhani unashindwa kutofautisha kati ya coallition government(CG)/governments of national unit(GNU) na Parliamentary opposition camp.Sikuelewi unapotaka cdm washirikiane na cuf kuunda CG sijui ya wapi hiyo. Kama ungelikuwa na mawazo huru na nia njema kabisa ungewashauri ccm waunde CG au GNU kwa kushirikiana na cdm, cuf,tlp,nccr mageuzi na udp. Maana huko ndiko ideologies zinapotekelezwa kutokana na manifesto za vyama husika. Sasa sijui unataka kutuambia kwamba opposition camp bungeni kuna ideologies gani zinatekelezwa.

Kama kumbukumbu zako ziko vizuri utakumbuka ni juzi tu mwezi novemba wabunge wa cuf waliwapigia kura Spika na Naibu spika wa ccm halafu leo wanataka cdm iwashirikishe kwenye kambi rasmi ya upinzani. Wangejua kwamba watahitaji kushirikishwa na cdm basi wangeanza kuonyesha msimamo huo tangu mwanzo.Wao walitarajia kwamba maadam wamewaunga mkono ccm na kwa kuwa wanaunda serikali na ccm kule zanzibar basi wangepata mteremko kwa spika kuwaruhusu kujiundia kambi ndogo bungeni, sasa walivyoona wamekwama ndo wameanza kulialia na waberoya unawasaidia kupaza sauti.

Narudia kukueleza kwamba CUF IS PART OF THE GOVERNMENT, hawana nafasi katika kambi ya upinzani!! kama wanaona kuna umuhimu wa ushirikiano, waelekeze nguvu kujadiliana na ccm ili wajumuishwe serikalini.
 
Mwita huwa sipendi sana kujibu post zako zimekaa kishabiki zaidi kuliko hali halisi!

Narudia silazimishi CDM kuungana na CUF!!! there is no where I have suggested that, rather I am saying reasons that CDM used to expel CUF was not proper!! naona unarudia kosa hilo hilo.

Kuhusu NGU, CG, Grands governments n.k nimeweka definition please dispute that definition, soma post no.36 uone naelezea nini maana naona bado uuko kwenye dunia ya 'upinzani' na sio ideology. usiseme hatuungani na CUF kwa sababu ni sehemu ya serikali..ukisema hivi unachukulia upinzani as to be against na sio upinzani kama ideology na different alternative!!! je wananchi watafaidika na haya maneno yenu yasiyo na tija kwa taifa, leo hii CDM wakishika nchi basi TLP ni wapinzani..hata kama wanafanya mazuri, hii ndio dunia yako ubadilike sasa mkuu
 
you have said so many things without saying anything,...the question is...maalim seif ataweza kwenda against na serikali anayoiongoza,kwa sasa hivi anatekeleza sera za ccm,hawezi kuzicriticize
 
Back
Top Bottom