Infertility /ugumba

Infertility /ugumba

Nicas saguda

Member
Joined
Jun 8, 2015
Posts
15
Reaction score
16
Kwa mwanamke ambaye anashindwa kupata ujauzito na amepimwa ultrasound akaonekana yuko salama apime vipimo vifuatavyo

1. prolactin hormone
2. thyroid stimulating hormone (T4)
3. sukari
4. HSG
5. Sperm analysis mumewe

Kwa mwanamke anayeshindwa kupata ujauzito moja ya sababu zinazopelekea mwanamke mwenye umri wakuzaa kutokuzaa nipamoja Na TB YA MFUKO NA MIRIJA YA UZAZI kapime haraka

Kama mwanaume anayeshindwa kupata mtoto Na Hana hamu ya tendo la ndoa

Akafanye vipimo vifuatavyo
1. Testosterone hormone
2.follicle stimulating hormone

Na atapata majibu na atakuwa salama kabisa

Mwanamke hata Kama ametoa kizazi lakin akabakiziwa mayai huyu anaweza akapata mtoto kwa njia yakupandiliza

Kupima saratani ya shingo ya kizazi nibure kwenye Vituo vyote vya kutolea huduma nchini main land and Zanzibar

Kansa inayoweza kutibiwa kwa urahisi kwa mwanamke inaitwa endometrial cancer
Na sababu zinazoweza kupelekea ukapata kansa hiyo ni pamoja na zifuatazo
1. Early menarche
2. Late menarche
3.obesity
4. PCOS
5. Exogenous unopposed estrogen
Mwanamke anapoanza kupata siku zake kabla ya miaka 12 na kumaliza siku zake katika miaka ya 50 huyu anaweza kupata hiyo aina ya saratani , lakin Ndio saratani pekee inayotibiwa kirahisi

Habari njema nikwamba kwa sasa hakuna mwanamke atakayeweza kushindwa kupata mtoto labda aamue mwenyewe njia nyingi Za kisayansi sasa zinaweza kumsaidia

Wanawake wanaotumia vidonge vya uzazi wa mpango kwa ajili yakupanga uzazi habari njema nikwamba wanapata kinga kwa kuugua saratani ya mfuko wa mayai Yaan ovarian cancer

Mwanamke mjamzito mimba inapotimiza kuanzia miezi sita anaweza kuanza kusikia maumivu asiogope nikawaida tu ila yanapozidi atafute kituo chochote cha afya ahudumiwe

Mwanamke anayenyonyesha anaingia kwenye siku Za hatari wiki mbili mpaka nne baada ya kujigungua kwahiyo mwanamke anayenyonyesha anaweza kupata mimba hata kama haoni siku zake

Mda mzuri wakutaka kujua Kama mtoto wako hana tatizo lolote , fanya ultrasound mimba ikiwa na wiki 18-20
Tunaita ultrasound anatomy

Hakikisha unakutana Na mwenzi wako sio chini ya maratatu kwa wiki ikiwa unatafuta mtoto

Na Kama mwenzi wako yuko mbali mnakutana kwa mda maalumu
Waulize wataalamu wakupangie nisiku gani mhimu ambazo unaweza shika mimba

+255652580204
WHASAP only

HIV haiambukizwi kwa mate, kukohoa, Au kugusana mikono au kukaa pamoja

Jitahidi kabla hujashika mimba upime sukari , pressure na wingi wadamu ili kuepusha mtoto kuzongwa na ukuaji mbaya ambao kimsingi ungeepukika
 
IMG_0619.jpg

Cervical cancer screening is done to every woman attained 25yrs to 50yrs
 
Kwa mwanamke ambaye anashindwa kupata ujauzito na amepimwa ultrasound akaonekana yuko salama apime vipimo vifuatavyo
1.prolactin hormone
2.thyroid stimulating hormone (T4)
3.sukari
4.HSG
5. Sperm analysis mumewe
T4 na infertility zina uhusiano gani?? Clarifications please

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Mkuu kuna njia yoyote ya kujua kuwa wewe ni mgumba tofauti na kupima ( kwa wanaume)
Wewe unaonekana ni muoga wa kufanya vipimo kujua afya yako. Hebu nenda hapo clinic uonane na mtaalamu akupime akupe majibu. Achana na hizi chenga za mwili.
 
Kwa mwanamke ambaye anashindwa kupata ujauzito na amepimwa ultrasound akaonekana yuko salama apime vipimo vifuatavyo
1.prolactin hormone
2.thyroid stimulating hormone (T4)
3.sukari
4.HSG
5. Sperm analysis mumewe

Nilimaanisha hivi vipimo gharama yake
 
Mkuu kupima sperm kama ziko sawa inaweza kwenda gharama kiasi gani ?

Itategemea na hospitali ila nikati ya 30 mpaka 50 elf , na kuna utaratibu unapewa usikutane Na mwanamke siku tano kabla yakutoa hizo mbegu Na kuna mda tunakupatia sex toy
 
Habari njema nikwamba kwa sasa hakuna mwanamke atakayeweza kushindwa kupata mtoto labda aamue mwenyewe njia nyingi Za kisayansi sasa zinaweza kumsaidia
Mfano ana kuwa ana hitaji mtoto lakini gharama zenyewe ndio hizo kuanzia 14milioni na yeye ni masikini.Hapo tutasema kuwa huyu hajaamua?
 
Mfano ana kuwa ana hitaji mtoto lakini gharama zenyewe ndio hizo kuanzia 14milioni na yeye ni masikini.Hapo tutasema kuwa huyu hajaamua?

Gharama sio hizo Kama unazosikia anaweza pia akahudumiwa hata kwa bei rahis zaidi lakin Je unauhakika kwamba njia nyingine zote zimeshindikana?!!!
 
Gharama sio hizo Kama unazosikia anaweza pia akahudumiwa hata kwa bei rahis zaidi lakin Je unauhakika kwamba njia nyingine zote zimeshindikana?!!!
Njia zote nyingine ameshajaribu iliyobakia ni hiyo ya kupandikiza mimba!!alienda pale hospital ya kairuki kujaribu kutaka kujua ki undani!!!ndipo akakutana gharama hizo,kuwa japo kuna vipimo vingi atatakiwa kufanyiwa kwanza lakini navyo ni gharama pia.ila ni kuanzia 14M, na inaweza kuongezeka kutegemea na vipimo atakavyofanyiwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom