Zurie
JF-Expert Member
- Jul 6, 2014
- 2,002
- 5,534
Kufuatia mlolongo wa mashambulio yatokanayo na ubaguzi wa rangi dhidi ya Wanafunzi wa Kiafrika nchini India, Jumuiya ya Wanafunzi wa Afrika(AASI) imetishia kuandika malalamiko rasmi kwenda Umoja wa Afrika(AU).
Wiki hii Waafrika kadhaa wameshambuliwa, hasa eneo la Greater Noida katika jimbo la Uttar Pradesh. Ambapo katika shambulio la karibuni mwanamke wa Kenya alishambuliwa na kupigwa na wanaume wasiojulikana katikati ya mtaa.
Tukio hili linafuatia lile la tarehe 27 la Wanafunzi wa Nigeria kuvamiwa na kundi la watu wakituhumiwa kuwa wauaji na 'wala watu' kufuatia kifo cha mtoto mtaani hapo.
Wanafunzi hao walionesha kuchoka ahadi za Serikali ya India kuwa watawalinda kwani hawaoni hatua zozote zikichukuliwa. Serikali hiyo kupitia Waziri wake wa Mambo ya nje, Sushma Swaraj ililaani vitendo hivyo na kuomba uchunguzi kufanywa kuhusu matukio hayo ya kibaguzi.
Jumuiya hiyo imesema kuwa itataka Umoja wa Afrika uamuru nchi zote za Afrika kuacha biashara yoyote na India endapo serikali itashindwa kuwalinda na kutoa ulinzi mkali maeneo wanayoishi.
Pia wanafunzi hao wamesema kuwa watashawishi wanafunzi kutoka nchi zao kutoenda kusoma India kwani nchi hiyo si salama na wamechoka kuitwa 'wala watu'.
ASSI imewashauri Wanafunzi wote wa Kiafrika waishio Greater Noida kubaki ndani ya nyumba zao hadi hatua za kuridhisha za kiusalama zikichukuliwa.