#COVID19 India: Maambukizi ya Corona yapungua

Sam Gidori

Senior Member
Sep 7, 2020
165
414
India imeripoti kushuka kwa maambukizi ya virusi vya corona katika miji yake mikubwa miwili ya Delhi na Mumbai, inayokaliwa na zaidi ya theluthi mbili ya wakazi bilioni 1.4 wa taifa hilo.

Maambukizi mapya 326,098 yameripotiwa ndani ya saa 24 zilizopita, pamoja na vifo 3,890, ingawa wataalamu wa afya wanasema idadi inayoripotiwa huenda ikawa ndogo kuliko uhalisia.

Kwa mara ya kwanza ndani ya kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja uliopita, chini ya visa 10,000 vya maambukizi vimeripotiwa ndani ya siku moja. Mji wa Delhi umeshuhudia visa 8,506 vya maambukizi ndani ya saa 24 zilizopita. Katika mji wa kibiashara wa Mumbai, maambukizi yameshuka kufikia visa pungufu ya 2,000 kutoka 11,000 kwa siku.

Waziri Mkuu, Narendra Modi amewaonya wananchi kuchukua tahadhari zaidi hasa wakati huu ambapo maambukizi ya virusi vya corona yamehamia katika maeneo ya vijijini yenye uhaba mkubwa wa miundombinu ya afya.

Chanzo: ABC News
 
Hao wataalamu wao wanachojua ni kusema idadi iliyoripotiwa ni ndogo ila ikiwa kubwa isiyoendana na uhalisi hawasemi.
 
Walivyotakiwa kufanya ni kutufuata sisi! Kuimarisha matibabu ya asili. Haya pia yanaendelea vizuri pale ila kiserikali matibabu ya mwanzo ni yale yaliyotangazwa na WHO. Katika hizo, mtengenezaji wa kwanza yaani kubwa kuliko yote dunani ya vaccine ni India. Mumbai na Delhi kwa pamoja wana wakazi tusme millioni hamsini.

Yaani ni kama nchi nzima. Hesabu ya wakazi wa nchi moja India kwa jumla inafika kwenye wakazi 1.36 billion yaani kama nchi 87 za dunia. Asilimia ya watu walioripotiwa na ugonjwa huo ni chache sana tukilinganisha na nchi nyingine. Hata kama wakisema kwamba wengine hawa ripotiwi, asilimia itakuwa ndogo tu.

Na asilimia zaidi wanafuata matibabu ya asili - ayurveda - na wanapona ila mambo haya hayatangazwi. Kwa mfano, Patanjali wametoa matibabu ya Covid 19 kwa watu malaki na wamepona.
 
Tatizo wanatengeza vifaa vingi na kuuza nje badala wawasaidie wananchi kwanza
Nimeona madhehehu yao ya dini wananunua mitungi ya hewa na kuwasaidia wagonjwa ila ukienda hispitali huduma hizo hupati

Chanjo kwa app ni mtihani pia
 
Kwa sasahivi wanazo wave ya pili ambayo ni nzito sana kuliko ya kwanza. Waliuza na walitoa msaada kwa nchi nyingi baada yakupona kutoka wave ya kwanza kwa sababu hakukuwa vacinne mwingine na madawa mengine muhimu kwa nchi hizo. Lakini sasa nchi hiyo imeanza kupona kutoka wave ya pili na inatayarisha kwa ajili ya wave ya tatu ikitokea ambayo inakusudiwa kutoka.
 
Yapungue kwa kweli, nina biashara yangu ya pamba imekwama kutokana na hilo janga Mipango yangu mingi imeharibika
 
Back
Top Bottom