Inawezekana ukaishi na mtu usiyempenda?

Illuminata Rodgers

JF-Expert Member
Nov 25, 2015
2,845
2,020
Habarini,hiki kitu kimenishangaza sana nikaona nikilete hapa jukwaani..hivi inawezekana kwa mwanaume kuishi na mwanamke usiempenda kama wanandoa au mwanamke kuishi na mwanaume usiempenda kama wanandoa,yani mkaishi wote kwa kigezo kwamba kuna sababu tu iliwafanya mkaishi wote ila mmoja wenu hampendi mwenzie hata kidogo yani yupo tu kwa vile imembidi,hii kitu inawezekana kweli watu watu wangu wa nguvu!
 
Wengi tu wanaishi hivyo. Ila nadhani unamaanisha anayekusisimua kimapenzi ,maana upendo sio hisia ni mlolongo wa mambo mema unayoyafanya kwa mwenzi wako kwa utashi wako. Unaweza kuchagua kumpenda Au kutompenda mtu bali hisia ni kitu tofauti
 
The answer is yes. Wewe hujapata sikia vijana wanavyohadaa mabibi wakizungu wakaishi Europe au US? Hapa ni wote me/ke. Sababu zipo nyingi.......kupata nafuu ya maisha/chapaa. Kufurahisha ndugu/marafiki/jamaa. Pia unaweza sema ni attitude ya mtu binafsi.....nini unataka katika maisha? Kwahakika zaidi huwezi sema sana fulani anaishi na fulani lakini hawapendani.
 
Nadhani swala la kuishi sio tuu linategemea upendo ila kuna vifungo vingine ambavyo huwalazimu tuu kuishi Haata kama upendo Hamna.

Watoto, kiapo cha ndoa, kuna Aina za kazi au status Fulani hiv huwez kumuacha mke / mume.

Pia inategemea na sababu zilizopelekea upendo ukawa zero. Kuna sababu zinavumilika with hope kwamba huko mbelen zinaweza kutatulika.

Naweza kusema mnaweza kuishi lakini mtaishi kama ccm na ukawa vile....
 
Labda sijaelewa Nini unamaanisha ila kuna maaana mbili nazipata ipi sijui ndio uliyo maanisha.

Mnaweza kuishi na usiyempenda kwa maaana kwamba hampendani ila mmeamua kuanza kuishi

Au mshaishi alafu mmejikuta tuu hampendani? Teyari mshaishi je mtaendelea kuishi?

Nadhani swala la kuishi sio tuu linategemea upendo ila kuna vifungo vingine ambavyo huwalazimu tuu kuishi Haata kama upendo Hamna.

Watoto, kiapo cha ndoa, kuna Aina za kazi au status Fulani hiv huwez kumuacha mke / mume.

Naweza kusema mnaweza kuishi lakini mtaishi kama ccm na ukawa vile....
Nimemaanisha kwamba hampendani lakini mnaishi wote kutokana na sababu fulani lakini hapohapo hiyo sababu inaweza ikaepukika
 
Kuna wakati kweli unaona hii ndoa hainifai...
Ndani na nje ya ndoa kila mmoja analiona hilo...
Kila jitihada ya kuachana haifanikiniwi....
Ni kana kwamba hilo "Ni kosa la maisha" japo moyo unakataa kukubali...
Kifupi inatokea.
 
Habarini,hiki kitu kimenishangaza sana nikaona nikilete hapa jukwaani..hivi inawezekana kwa mwanaume kuishi na mwanamke usiempenda kama wanandoa au mwanamke kuishi na mwanaume usiempenda kama wanandoa,yani mkaishi wote kwa kigezo kwamba kuna sababu tu iliwafanya mkaishi wote ila mmoja wenu hampendi mwenzie hata kidogo yani yupo tu kwa vile imembidi,hii kitu inawezekana kweli watu watu wangu wa nguvu!
Kuna kuishi na kuishi vizuri,
 
Ndio inawezekana kabisa.! Hasa kwa wanawake, kwani wanawake wengi huwapenda wanaume sio kwa namna ya mionekano yao Bali hupenda "Thamani aliyonayo mwanaume"( The values attached to the man), mfano Less, kipaji, Kazi n.k.

Hivyo mwanamke anaweza kuishi NA mwaume hata kama hampendi kwa muonekano wake. Mfano binti anaweza kuambiwa kunamkaka anataka kukuchumbia, jibu la kwanza kwa Binti ni, Anafanya Kazi gani?.

Ila kwa upande wa wanaume no vigumu sana kuishi na mwanake hasiyempenda kwa muuonekano wake, ushaidi wa hili Kijana akiambiwa kunu binti anakufaa kwa maisha, swali la kwanza kutoka kwa kijana huyo
 
Sorry.! Swali La kwanza kutokana kwa Kijana huyo, je binti huyo ni mzuri ? Then ndo swala La tabia litauliziwa.
 
Mbona watu wanaishi na shetani tena mioyoni mwao, kwani wanampenda?

Ndio iwe binadamu? Inawezekana sana.
 
Habarini,hiki kitu kimenishangaza sana nikaona nikilete hapa jukwaani..hivi inawezekana kwa mwanaume kuishi na mwanamke usiempenda kama wanandoa au mwanamke kuishi na mwanaume usiempenda kama wanandoa,yani mkaishi wote kwa kigezo kwamba kuna sababu tu iliwafanya mkaishi wote ila mmoja wenu hampendi mwenzie hata kidogo yani yupo tu kwa vile imembidi,hii kitu inawezekana kweli watu watu wangu wa nguvu!
Kwa mfano mr machache hata kama humpendi huwezi kuishi nae?
 
Habarini,hiki kitu kimenishangaza sana nikaona nikilete hapa jukwaani..hivi inawezekana kwa mwanaume kuishi na mwanamke usiempenda kama wanandoa au mwanamke kuishi na mwanaume usiempenda kama wanandoa,yani mkaishi wote kwa kigezo kwamba kuna sababu tu iliwafanya mkaishi wote ila mmoja wenu hampendi mwenzie hata kidogo yani yupo tu kwa vile imembidi,hii kitu inawezekana kweli watu watu wangu wa nguvu!
Kabisa inawezekana maana hata mie naishi tena kwa ndoa na mtu ambae simpendi
 
Back
Top Bottom