Inawezekana Mh. Ndalichako hakufuata taratibu kurudisha mfumo wa division kutoka GPA

Abunuas

JF-Expert Member
Apr 8, 2011
8,812
1,824
Nimeshangazwa sana na hoja dhaifu za waziri wa elimu juu ya kurudisha utaratibu wa mfumo wa matokeo ya sekondari ya division kutoka GPA. Alipohojiwa na mtangazaji wa TBC Marine Hasan Marine kwa kweli majibu yake yalikuwa yakuungaunga. Kwa bahati mbaya zaidi kwake Marine alimwekea clips zake alizoongea akiwa Dar na Dom ambazo kiuhalisia alikuwa akijichanganya na kile alichokieleza. waziri aliyetangulia alizingatia maoni ya wadau katika hilo. sio suala alilokurupuka tu overnight na kubadilisha. kwa maana ingine hilo ni suala la kisera. lilitakiwa lifuate mfumo uleule wa kisera kuliko mtu mmoja tu kuamka asubuhi na kuyaona maoni ya watu mbalimbali sio chochote ila yake yeye. Kama mtakumbuka pia joseph mungai waziri kipindi cha mkapa aliunganisha masomo ya sayansi na kufuta masomo ya biashara, kilimu na michezo mashuleni bila kushirikisha wadau wa elimu kitu kilichomuwezasha mh. margaret sitta kuyaondoa kwa mfumo ule ule.
Bila kuathiri umuhimu wa maamzi yenyewe, ipo haja ya sisi kama watanzania kufuata taratibu kuliko kuyaona maamzi yangu omega.
 
Back
Top Bottom