Kupima wanafunzi wa kidato cha pili kwa kutumia division ni kuharibu mfumo wa elimu

Konseli Mkuu Andrew

JF-Expert Member
May 10, 2013
740
855
Kwa miaka kadhaa sasa baraza la mitihani ya taifa linatoa matokeo ya kidato cha pili kwa kutumia mfumo wa division tofauti na ule wa miaka ya nyuma wa wastani.Hii tasfiri yake kuwa mwanafunzi akiwa amepata D mbili na F saba au 9 basi anakuwa amefaulu kuendelea na kidato cha tatu na hatimae kuja kuhitimu kidato cha nne, tofauti na miaka ya nyuma ambapo mwanafunzi alitakiwa kupata walau wastani wa D ambayo ilikuwa ni wastani wa 30 ndipo aweze kuendelea na kidato cha tatu.

Sijui ni nani alishauri matumizi ya mfumo huu, kiukweli kuendelea kutumia mfumo huu ni kuandaa wanafunzi watakao kuja kupata division sifuri nyingi katika matokeo ya kidato cha nne, inawezekana vipi mwanafunzi apate D mbili na F zote maana yake anakuwa na division 4.33 akafanana na yule wa miaka ya nyuma aliyepata wastani wa 30? Nini chanzo cha matumizi ya division kwa mitihani ya kidato cha pili? au ndio mpango wa BIG RESULT NOW? au ni ni ile program ya EDUCATION FOR ALL iliyohasisiwa huko Indonesia iliyopelekea kuanzishwa kwa shule za kata?

Waziri wa Elimu Prof Adolf Mkenda najua upo makini ni vyema sasa ukaanza na ili kwanza, hawa ni watoto wetu/wadogo zetu kuwapima kwa mfumo wa division ni kujidanganya sisi wenyewe ni heri wafaulu wachache ila matokeo yawe katika ubora unaotakiwa.Tusiogope wanafunzi kukariri madarasa kwa kuhofia kushuka kwa ufaulu wakati tunaharibu mfumo wa elimu kwa kuweka vitu visivyo hakisi maendeleo ya elimu.

Kuandika hapa haitoshi nitakupigia simu na kukuandika ujumbe mfupi Mh Waziri wa Elimu Prof Adolf Mkenda na kukueleza hili ,najua fika mtalifanyia kazi.

#ElimuNiYetuSisi
 
Na huko shule za msingi watoe mitihani ya kujibu kavukavy ili kuchangamsha akili.
Hesabu mnaweka maswali ya kuchagua!
Vi woonder
 
Mifumo ya Cambridge na IB tunayosagia kunguni ni ya kimataifa siyo kisiasa, wanasiasa wengi wanasomesha watoto wao huko wanajua kule maisha ni zaidi ya A kuna personal development ya mtoto.
 
Hili ndo limeshindikana kabisa au tusubiri Zitto Kabwe atakapokuwa Waziri wa elimu? Yaani Tangu mwanafunzi anaanza la 1 mpaka form 6 Hakuna mahali anapimwa personal development mpaka afike chuo?
 
Siamini mkuu kuwa Zitto ndio atakayekuja kutibu mfumo wetu wa kielimu.Ni sisi tulie nje ya mfumo wa serikali ndio tuna wajibu wa kutoa maoni na kushauri pale tunapoona inafaa
 
Kwa miaka kadhaa sasa baraza la mitihani ya taifa linatoa matokeo ya kidato cha pili kwa kutumia mfumo wa division tofauti na ule wa miaka ya nyuma wa wastani.Hii tasfiri yake kuwa mwanafunzi akiwa amepata D mbili na F saba au 9 basi anakuwa amefaulu kuendelea na kidato cha tatu na hatimae kuja kuhitimu kidato cha nne, tofauti na miaka ya nyuma ambapo mwanafunzi alitakiwa kupata walau wastani wa D ambayo ilikuwa ni wastani wa 30 ndipo aweze kuendelea na kidato cha tatu.

Sijui ni nani alishauri matumizi ya mfumo huu, kiukweli kuendelea kutumia mfumo huu ni kuandaa wanafunzi watakao kuja kupata division sifuri nyingi katika matokeo ya kidato cha nne, inawezekana vipi mwanafunzi apate D mbili na F zote maana yake anakuwa na division 4.33 akafanana na yule wa miaka ya nyuma aliyepata wastani wa 30? Nini chanzo cha matumizi ya division kwa mitihani ya kidato cha pili? au ndio mpango wa BIG RESULT NOW? au ni ni ile program ya EDUCATION FOR ALL iliyohasisiwa huko Indonesia iliyopelekea kuanzishwa kwa shule za kata?

Waziri wa Elimu Prof Adolf Mkenda najua upo makini ni vyema sasa ukaanza na ili kwanza, hawa ni watoto wetu/wadogo zetu kuwapima kwa mfumo wa division ni kujidanganya sisi wenyewe ni heri wafaulu wachache ila matokeo yawe katika ubora unaotakiwa.Tusiogope wanafunzi kukariri madarasa kwa kuhofia kushuka kwa ufaulu wakati tunaharibu mfumo wa elimu kwa kuweka vitu visivyo hakisi maendeleo ya elimu.

Kuandika hapa haitoshi nitakupigia simu na kukuandika ujumbe mfupi Mh Waziri wa Elimu Prof Adolf Mkenda na kukueleza hili ,najua fika mtalifanyia kazi.

#ElimuNiYetuSisi
Ndiyo maana watawala watoto wao wanasoma Ulaya
 
Back
Top Bottom