Inawezekana kuvusha gari eneo la barabara lililofunikwa na mafuriko?

wakupampu

Member
Jul 30, 2013
28
41
Hivi unaweza kuvusha gari eneo la barabara lililofunikwa na mafuriko ilihali barabara haionekani? Au hasa ukiwa umesomea usalama wa barabarani?
 
Unaweza ila usiwe wa kwanza wacha gari lingine likutangulie mbele liwe kama chambo ukiona limepita poa na wewe unapita...Ila usijaribu wewe kuwa tester ni kichaa fulu.....Si kila kitu utafundishwa darasani.
 
Simama,angalia kwa mvali wingi na speed ya maji,mara nyingi maji ya mvua yanavyopita kasi haitazidi dk 50 yatapungua kabisa hapo utavuka salama
 
Kanyaga mafuta kwa nguvu zote pindisha sterling kushoto rudi reverse then utakuwa umepita
 
Vuka tu na kigari chako cha mlipo naona mleta kada una hamu ya kwenda mbinguni hauna jingine
 
unaweza mkuu! apo inabidi uendeshe kama semi tela zinavyoendeshwa kipindi inarudishwa nyuma, inakua hivi gari ikihama nyuma inaenda kushoto wewe kata upande wa kulia(sterling) hivo hivo ikipelekwa kulia wewe ipeleke kushoto kwa nguvu wakati huo accelarator uwe umekanyaga vya kutosha apo chuma lazima itoke ikumbukwe pia na speed ya maji iko vipi mana maji ni kitu ingine kabisa na pia uwe mwepesi kwenye mikono ili kuweza kuimudu stelingi. kila la kheri.
 
Toa upepo matairi yote Ili kuiwezesha gari kushikana na lami vizuri baada ya hapo weka gia namba 1/2 utapita kwa raha zako kama wewe ndiye umeumba maji.
 
nazan ulisikia ule mkasa uliyempata yule mpambe wa IGP Gerald Ryoba na familia yake?
kwa evidence zaid jaribu
 
Hamna kitu kibaya kuendesha gari kwenye mkondo wa maji hasa yakiwa speed. Ni bora usubiri.
 
Back
Top Bottom