Inawahusu Wananchi mzinduke.....

Mohammed Hamad

JF-Expert Member
Jan 17, 2011
3,988
1,304
Kwenye majukwaa wakismama wanatutia morali
Maneno wanayosema yanachoma kama mbigili
Wananchi tumesimama wanatuona tumbili
Sisi tunakondeana wenyewe wananawiri
Hali zetu ni duni twaishi kwenye makuwiri
Nyuso zetu zimefubaa kwa mishi ya vibatari
Wenye wanavaa makoti ya darizi na hariri

Wengine wabinafsi wamejawa na viburi
Wanataka ukwasi wenzao wapate sifuri
Wanazua ya kuzua na kufanya ukafiri
Wenzao wasiaminike wao wapate kudhihiri
Siku tatu zikipita wanatubeza kunawiri
Waliouwawa hawajaoza wao wanawabeza dhahiri

Sisi hatuelewani tunatukanana hadharani
Wenyewe wanakuta na kula nyama mnadani
Mimi na wewe tunatunguana kwa matusi jamvini
Na picha wanapiga wakazipamba gazetini
Pongezi wakatoa wakahutubua bungeni

Wengine wakanukuu wakapost jamvini
Mwingine akajajuu kukanusha kutoka mjengoni
Sijui alisinzia hamkusikilizaa kwa makini
Au ni upofu hajitambui yu mapenzini????
Hebu tufumbe macho tujitoe ufungwani
Tanzania yetu sote atakaeijenga ni nani?
Mimi nashika fito usinipokonye ramani
Wewe beba zege umimine aridhini
Yule achimbe shimo awafukie kaburini
Mwanakijiji amwagile mche bora wa amani

Wengine hukimbia wanapokosa nafasi
Huvikimbia vyamavyo wakafanya uasi
Juzi alikuwa shubiri leo kawa nanasi
Kesho akivurunda atatukimbi nasisi

Yeye mwasiasa anaganga yake nafsi
Kule watampokea kwa matarumbeta na brass
Kisha atawageukia kwa matusi na visasi
Agekuwa na uwezo angewamaliza kwa risasi
Hawa tumeshawajua wasijifanye bunuwasi
 
Waeshi kutudhikali na wingi wa ulaghai
Wakipata wakitakacho hutona hatufai
Ahadi watazitoa zenye wingi wa matumaini
Kisha wakifanikiwa wanakimbilia mijini
Chaguzi zikiwadia wanataka waongezewe muda
Kwa uchungu huongea na hiyo ni kawaida
Hutupa fulana bila tai tusahau uduni wetu
Kakatuhada na vitembe tukauza utu wetu
 
Back
Top Bottom